• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ZIARA YA MAFUNZO KWA WAHESHIMIWA MADIWANI NA WATAALAMU MANISPAA YA SINGIDA YALETA CHACHU YA MAENDELEO

Posted on: November 1st, 2022

HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida, imefanya ziara ya mafunzo katika Jiji la Mwanza na   mkoa wa Shinyanga, ili kujifunza utekelezaji na usimamizi wa miradi ya Mandeleo, kupitia mapato ya ndani, kwa lengo la kuongeza mapato yatakayochangia utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Ziara hiyo ya siku nane kwa mikoa hiyo miwili, ilihusisha Wakuu wa Idara na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, ikiwa ni azimio la vikao, likiwemo Baraza la Madiwani, kwa ajili ya kujifunza kupitia halmashauri zilizofanikiwa katika ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa usafi na mazingira pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.

Wakiwa Jijini la Mwanza, katika halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Madiwani na Wakuu wa Idara wakiongozwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Singida, Hassan Mkata, walitembelea Mradi wa Ujenzi wa Ofisi mpya wa jengo la Utawala na maendeleo ya ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani, cha Ilemela.

“Tumelazimika kufanya ziara hii ya mafunzo kwa nia njema kabisa ya kufahamu, nini ninyi wenzetu mnafanya katika kusimamia miradi yenu, na kitu gani tunapaswa kwenda kukifanya tukisharudi nyumbani kwa ajili ya maendeleo ya jamii yetu…,” alisema Naibu Meya wa Manispaa ya Singida.

Aidha Naibu Meya huyo, aliushukuru uongozi wa Jiji la Mwanza kwa mapokezi makubwa, na akapongeza juhudi za Jiji hilo katika kubuni na kutekeleza miradi ya maendeleo, ikiwemo pia kuimarisha ukusanyaji wa mapato yake ya ndani.

Katika ziara hiyo, maeneo mengine yaliyotembelewa na msafara huo ni, dampo la kisasa lililopo eneo la Buhongwa ambalo ujenzi wake unatekelezwa na Halmashauri ya Jiji, na pia kujionea maendeleo ya ujenzi wa soko ( Mwanza Central Market) eneo la Pamba Road linaloelezwa kuwa mkombozi kwa wananchi wa Jiji hilo pindi litakapokamilika.

Msafara huo ukiwa Mkoani Shinyanga, ulipata fursa ya kutembelea Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama iliyokamilika na kugharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 1.6.

Akiwa Kahama, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragili, aliipongeza Manispaa hiyo kwa maboresho makubwa,  pia ushirikiano uliopo kati ya wataalamu na madiwani, hali inayochangia kukua kwa kasi kwa Manispaa hiyo.

“Kwa kweli lazima niwapongeze kwa kazi nzuri, hapa naona mmeitendea haki kabisa Serikali yenu…sisi Manispaa ya Singida tumejifunza kitu, ili tukirudi, yote mazuri tuliyoyaona kwenu, basi tukayatumie kwa ajili ya manufaa ya watu wetu,”alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Naye Kaimu Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa, alisema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano baina yao, hali iliyowezesha kuongezeka kwa mapato ya ndani, ambayo yanachangia kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa hospitali ya Wilaya inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 1.6 hadi itakapokamilika.   

Aidha kwa upande wa jingo la ofsi za Manispaa ya Kahama Kaimu Mkurugenzi huyo amesema Mpaka kukamilika Halmashauri imetumia kiasi cha Shilingi 1,663,010,316.28 ikiwa kazi za ujenzi wa jengo, ujenzi wa fensi, ujenzi wa kibanda cha Mlinzi, ujenzi wa meneo ya maegesho ya magari na maeneo ya nje, ununuzi wa samani za ofisi na ufungaji wa  miundombinu ya TEHAMA ikiwa ni pamoja na ufungaji wa Mfumo wa kukusanyia mapato zote zikiwa ni fedha za makusanyo ya ndani.

Waheshimiwa Madiwani na wataalamu wa Manispaa ya Singida wakisikiliza taarifa ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoa wa shinyanga


Diwani wa Viti Maalumu Manispaa ya Singida Mhe. Margreth Malecela akiuliza swali  wakati wa ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.


Naibu Meya, Mhe. Hassan Mkata ( Katikati) wakipatiwa maelezo ya miradi inayotekelezwa katika Jiji la Mwanza. Kushoto ni Mchumi wa Manispaa ya Singida Jeremiah Kikonge na Kulia ni Mhe. Shabani Magwe Diwani wa Kata ya Unyambwa na Mhe. Munjori Kawawa Diwani wa Kata ya Utemini

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.