• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Maendeleo ya Jamii


                             HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA

                                                                                                                 

                                    IDARA YA MAENDELEO YA JAMII

 SHUGHULI ZA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII.

  • 1.0.UTANGULIZI. 
  • Idara inao watumishi  20 ambao wanafanya kazi makao makuu na kwenye ngazi ya kata .kati yao watumishi 4 wako ngazi ya Manispaa na Watumishi 1 wapo ngazi ya Kata,Watatu 3 wapo idara ya maji na Mtumishi 1 masomoni.Kata 4 hazina watumishi.

1.2.MAJUKUMU YA IDARA.

Kuunganisha nguvu za Jamii na serikali ili kuondoa fikra tegemezi.

Kutoa elimu kwa vikundi vya kijamii na kiuchumi vya wanawake na vijana ili waweze kubuni miradi yenye tija na endelevu.

Kufanya tafiti shirikishi za kijamii na kiuchumi ili kubaini fursa na vikwazo katika kujiletea maendeleo.

Kuimarisha demokrasia ili kuongeza kasi ya maendeleo ya watu.

Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango na miradi ya maendeleo.

Kuwezesha viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali kutengeneza ratiba za utekelezaji wa mpango/miradi endelevu ya maendeleo.

Kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kutunza takwimu na kumbukumbu mbali mbali kwa ajili ya matumizi ya jamii/serikali na Halmashauri.

Kusimamia na kuratibu shughuli za maendeleo, jinsia na watoto.

Kuratibu masuala ya UKIMWI na athari zake katika jamii.

Kusimamia utekelezaji wa miongozo na sera mbali mbali.

Kuweka mipango mizuri ya watoto kuhusu haki na wajibu wa wazazi kwa watoto, na watoto kwa wazazi na jamii nzima hasa wale wanaoishi mazingira magumu.

Kushikiana na Jamii kujua rasilimali zilizopo ili zitumike kwa manufaa ya Jamii nzima.

Kuwasiliana na mashirika yasio ya kiserikali ili kuunganisha mipango yao na serikali.

Kuelimisha Jamii madhara ya matumizi mabaya ya mila potofu na kudumisha mila zilizo nzuri kwa Jamii.

3.0.MGAWANYO WA MAJUKUMU.

  • Idara imegawanyika sehemu NNE kuu ambazo ni
  • i.Uratibu wa UKIMWI,
  •  ii.Uratibu wa mashirika yasio ya  kiserikali(NGOs,CBOs,FBOs),
  •  iii.Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi,
  •  iv.Uratibu wa Wanawake na Vijana.
  • i.Uratibu wa UKIMWI, Sehemu hii kuna mratibu wa UKIMWI wa Manispaa ambae majukumu yake  ni kuhakikisha Jamii inapata uelewa wa kutosha kuhusu athari za ugonjwa huu kwa Jamii.Shughuli hii hufanyika kwa kushirikiana na watumishi wa idara waliopo kwenye kata na idara ya afya kinga.
  •  NINI KIFANYIKE;
  • i.Wazazi wawe waalimu wa kwanza kutoa elimu ya maadili ngazi ya familia,kama kila mzazi atatimiza wajibu wake hata idadi ya watoto waliopo mtaani itapungua.
  • ii.Wafanyabiashara waache tabia ya kuwaajiri watoto kwenye biashara zao mfano kufanya usafi kwenye mabaa,mahotelini, mighahawani huu ni ukiukwaji wa haki za mtoto na sheria ya mtoto ya mwaka 2009.Sheria hii inaweka wazi haki za watoto ikiwa ni pamoja na stahili zao na adhabu mbalimbali kama sheria hii itakiukwa.(sheria ya mtoto ya mwaka 2009 imeambatishwa kwenye taarifa hii)
  • iii.Viongozi wa dini  pasipo kuficha wahubiri kwenye nyumba za ibada na misikitini kuwa  UKIMWI unaua watu wachukue tahadhari.
  • iv.Swala la UKIMWI ni agenda ya kudumu kwa kila kikao au mikutano kwa ngazi zote kuanzia Halmashauri,Kata,mitaa,vijiji ,na vitongoji hivyo,viongozi wazingatie hilo ili kuwakumbusha watu mara kwa mara.
  • v.Vikundi vya wanaoishi na virus vya UKIMWI (WAVIU) vitumike kutoa shuhuda na elimu kwa wananchi, vikundi hivi vinawezeshwa na Manispaa kupitia mfuko wa TACAIDS, kila kata vikundi kama  hivi vipo wasiliana na idara kupata kikundi kilichopo karibu na eneno lako. 
  • ii.Uratibu wa mashirika yasio ya  kiserikali(NGOs,CBOs,FBOs)

Idara inaratibu mashirika yasiyo ya kiserikali lengo ni kuunganisha nguvu za serikali na wadau wengine wa maendeleo.Pia idara imekuwa ikitambua vikundi vya kijamii vinavyofanya kazi katika Manispaa ya Singida kwa kutumia utaratibu ufuatao

Taratibu za kusajili kikundi

  • Katiba ya kikundi iliyosainiwa na wanachama wote wa kikundi
  • Muhtasari wa kikundi ukiomba kusajili  kikundi na mahudhurio ya kikundi.
  • Barua ya kuomba kusajiliwa kwenda kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Singida
  • Kupitia kwa Mtendaji wa Mtaa na Mtendaji wa Kata.
  • Gharama za utambuzi ni Tshs 10,000/= Fedha hizo zitalipwa benki Acc Na. 50810001458 NMB .Jina la Akaunti Mkurugenzi wa Manispaa.
  • Kwa Manispaa yetu ya Singida idara inafanya kazi na mashirika yafuatayo;

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YALIYOPO MANISPAA YA SINGIDA.

NA 
JINA LA SHIRIKA
LENGO LA SHIRIKA
NAMBA ZA SIMU/EMAIL
1.
Demitrial Ministries International (DEMI)
Kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
0758465663
Beju56@yahoo.com
2.
SAHOTA FOUNDATION
Kuondoa umaskini na kuwawezesha wasiokuwa na sauti kuwa na sauti
0754807848
sahotaminja@yahoo.com
3.
TIENAI
Kupambana na kupunguza maambukizi ya UKIMWI
0754544108/0763336664
 
4.
Save the Mother and Children of Central Tanzania(SMCCT)
Kujenga uwezo kwa akina mama ili waweze kuwa na mazingira mazuri ya kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya kijamii na kiuchumi pamoja na kuwaanzishia kuweka na kukopa ili kujiendeleza kiuchumi.
0765470611
evalinelyimo@gmail.com
mcctngo@gmail.com 
5.
SINGIDA NUTRITION COALITION
Kuelimisha jamii kuondokana na upatiamlo
0765470611
evalinelyimo@gmail.com
6.
COMMUNITY INITIATIVES PROMOTION TRUST FUND (CIP TRUST)
Kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii jamii  zenye hali duni
0766186673
singidacip@yahoo.com
 
7.
SINGIDA (UPENDO) HOME FOR STREET CHILDREN
Kuwasaidia watoto wa Mitaa  kujikwamua kiuchumi na kijamii.
0766186673
upendo.home@yahoo.com
 
8.
YOUTH MOVEMENT FOR CHANGE (YMC)
 
Kujenga uwezo kwa vijana washiriki katika maamuzi ya kijamii,kiuchumi,kisiasa, na kiutamaduni.
0755516482
youthmvmnt@yahoo.com
 
9.
NEW HOPE PARALEGAL CENTRE SINGIDA(NNPC)
Kuelimisha jamii juu ya sheria na haki za Binadamu
0766305655
salumuh@yahoo.com 
10.
SINGIDA PARALEGAL AID CENTRE(SIPACE)
Kuelimisha jamii juu ya sheria na haki za Binadamu
0784293202/0763861819/0755300535
Sipace84@yahoo.com 
11.
THE  AGAPE ORPHANS CHILDREN CARE SUPPORT(AOCCAS)
Kuwahudumia na kuwasaidia watoto wa mazingira hatarishi
0754432903
12.
YOUTH EXTENDED FOUNDATION(YOEFO)
Kuhakikisha vijana kutoka kwenye fikra tegemezi
0766471358
Yoefo2013@yahoo.com 
13.
AFRICA LULU NJEMA DEVELOPMENT ORGANIZATION(ALNDO)
Kuona jamii iliyowezeshwa na kufanikiwa kimaisha katika kutatua changamoto kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa usahihi na endelevu
0762233677
africalulunjema@gmail.com
14.
WAZEE NA UKIMWI SINGIDA (WAUSI)
Kutoa elimu ya maambukizi mapya ya UKIMWI na huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi
0755083268
15.
FARAJA CENTRE CBHC
Kuinua hali ya afya za wanawake na wanaume ,watoto na vijana hasa walio kwenye mazingira hatarishi.
02622502641
farajacentre.cbhc@yahoo.com
 
16.
SICD
Kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
0769736770
Sicd2006@gmail.com
17.
FPTC-CAMPASSION INTERNATIONAL TANZANIA
Kuwawezesha watoto na vijana kumudu changamoto za maisha kama kupata elimu ya malezi na maadili
0758388153/0622388153
tz813@icptz.org
johnfredie@yahoo.com
 
18.
ADESE
Kuhifadhi na kuboresha mazingira
0769380960
19.
SINGIDA EDUCATION FOUNDATION
Kuhamasisha na kusaidia kutoa elimu mkoani Singida
0764084006
sefsingida@gmail.com
jmahumbi@yahoo.com
20.
SINGIDA DEVELOPMENT ASSOCIATION(SIDAs)
Kuhamasisha jamii kutumia rasilimali zilizopo kuboresha maendeleo kijamii na kiuchumi
0758206784/0754270906
sidasdev@gmail.com 
21.
SIPHA
Mapambano ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI
0752274700
siphagroup@yahoo.com
22.
FPTC
Kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
0767904093/0784904093
Fptcstcc.proj@yahoo.com
23.
SingidaChildren and  Community centre
Kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
0763775124
minjasarah@yahoo.com
24.
Safina  Street Children Network
Kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
0754977859
25.
Amani Children Centre
Kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
0757973690
26.
TUSIFO
Kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
 
27.
SEMA
Kupunguza umaskini na kuboresha mazingira
0754595638
28.
HAPA
Kupunguza umaskini na kuboresha mazingira
0768163761
29.
REFORMED STREET KIDS OF AFRICA-(KIDS OF AFRICA)
Kuhudumia watoto wa mitaani
0762368010
info@kidsofafrica.org
www.kidsofafrica.org 
30
MAMAS &PAPAS COMMUNITY REFORM
Kutoa ushauri kwa watuamiaji wa madawa ya kulevya na matibabu
0754454113/0678296881

3.Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Idara ya Maendeleo ya Jamii inaratibu vikundi vya ujasiriamali  pamoja na wadau wengine ambao wanatoa fursa za mikopo kwa wajasiriamali na vikundi vya kijamii katika kuhakikisha jamii inajikwamua na umasikini kama ifuatavyo:-

1.Mfuko wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi(MEF)

1.1     Historia ya Mfuko

MEF  iko chini ya usimamizi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) , ambalo ni wakala wa Serikali  ilioanzishwa mwaka 2005 kwa sheria ya 16 ya mwaka 2004 ikiwa na jukumu la kusimamia na kufuatilia jitihada zote za uwezeshaji wananchi kiuchumi.

2.1.2  Madhumuni ya Mfuko

Madhumuni ya MEF ni kuwawezesha Wananchi Kiuchumi kupitia njia zifuatazo:-

  • Kukuza na kuhimiza uelewa mpana kwa watanzania kuhusu usawa katika umiliki wa uchumi
  • Kuchangia katika kuibua fursa za ajira
  • Kuwa kiunganishi baina ya asasi na taasisi zilizndikishwa chini ya ya sheria ya uwezeshaji namna 16 ya mwaka 2004
  • Kufuatilia shughuli za kiuchumi zinazofanywa na asasi na taasisi hizo na kutoa msaada au huduma za kitaalamu pale inapohitajika kwa lengo la kuimarisha na kuboresha shughuli za kiuchumi.
  • Walengwa wa Mfuko
  1. Wajasiriamali katika VICOBA
  2. Wajasiriamali katika SACCOS
  3. Wajasiriamali katika vikundi vingine vya kiuchumi na taasisi mbalimbali.
  • Vigezo vya Utoaji Mikopo
  • SACCOS
  • SACCOS iwe imesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya ushirika
  • Iwe na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia na kupata mafunzo kuhusu uendeshaji wa SACCOS
  • Iwe na kamati ya mikopo iliyopata mafunzo ya namna ya kujadili, kutoa, kusimamia na kufuatilia mikopo yote inayotolewa na chama.
  • Iwe na katiba na sera zinazisimamia uendeshaji wa shughuli za chama kama mikopo n.k
  • Iwe na Kamati ya Usimamizi iliyopata mafunzo ya namna ya kusimamia SACCOS.
  • Iwe na uzoefu wa kukopeshana usiozidi mwaka mmoja na kuwa na kiwango kizuri cha marejesho kisichopungua asilimia 95.
  • Mkopaji atajidhamini mwenyewe kwa kuweka akiba ya asilimia 30 ya mkopo anaoomba katika akaunti ya muda maalumu kwenye benki itakayotoa mkopo.
  • Iwe na mfumo mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu za kiuhasibu za chama.
  • Iwe na Ofisi inayotambulika.
  • Utoaji wa mikopo uzingatie taratibu za ushirika kama kuwa na hisa na akiba zinazotosha mkopo unaoombwa na mwananchama.
  • Muda wa marejesho ya mkopo hautazidi miaka miwili
  • Riba ni asilimia 13
  • SACCOS lazima ifungue akaunti benki
  • Mikopo yote itakayodhaminiwa na Baraza itakatiwa pia bima ya maisha ya mkopo.
  • VICOBA NA VIKUNDI VINGINE
  • Kikundi cha VICOBA Kiwe kimesajiliwa aidha Ofisi ya Maendeleo ya Jamii au Brella
  1. Kiwe na uongozi uliopatikana kidemokrasia na pia kupata mafunzo kuhusu uendeshaji wa VICOBA na vikundi vingine.
  2. Kiwe na kamati tendaji iliyopata mafunzo ya namna ya kujadili, kutoa, kusimamia na kufuatilia mikopo yote inayotolewa na kikundi.
  3. Kikundi kiwe chini ya asasi/Taasisi inayotambulika.
  • Kiwe na Katiba na sera zinazosimamia uendeshaji wa shughuli za kikundi kama vile mikopo n.k
  1. Kiwe na uzoefu wa kukopeshana usiopungua mwaka mmoja na kuwa na kiwango kizuri cha marejesho kisichopungua asilimia 95.
  2. Kiwe na mfumo mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu za kiuhasibu za kikundi
  3. Kiwe na sehemu maalum inayotambulika ya kufanyia shughuli zao.
  • Mkopaji atajidhamini mwenyewe kwa kuweka akiba ya asilimia 30 ya mkopo anaoomba katika akaunti ya muda maalumu kwenye benki itakayotoa mkopo.
  • Utoaji wa mikopo uzingatie taratibu kama vile, mkopo utakaotolewa usizidi mara 3 ya hisa ya mkopaji.
  1. Muda wa marejesho ya mkopo hautazidi miaka miwili.
  2. Riba 13%.
  3. Kila kikundi cha VICOBA kitatakiwa kufungua Akaunti Benki.
  4. Mikopo yote itakayodhaminiwa na Baraza itatakiwa kukatiwa bima ya mkopo

2.Mfuko wa  Misitu Tanzania (TaFF) 

Historia ya Mfuko

Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) ni Mfuko upo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii na umeanzishwa chini ya Sheria ya Misitu Sura ya 323 ya mwaka 2002 kama njia endelevu ya kuwezesha uhifadhi, usimamizi na uendelezaji wa rasilimali misitu hapa nchini. Lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kukabiliana na changamoto za usimamizi wa rasilimali ya misitu hasa katika kuimarisha utekelezaji wa Sera na Sheria ya Misitu. Mfuko huu ambao Mfuko wa Misitu Tanzania unatekeleza shughuli zake upande wa Tanzania Bara, ulizinduliwa kupitia Waraka wa Hazina Na. 4 wa mwaka 2009 na ulianza rasmi shughuli zake Julai 2011.

Majukumu ya mfuko wa misitu tanzania

  1. Kuhamasisha jamii kupitia elimu na mafunzo kuhusu umuhimu wa kuhifadhi, kuendeleza na kutumia rasilimali ya misitu kwa njia endelevu;
  2. Kuhamasisha na kusaidia uendelezaji wa misitu ya jamii kwa kutoa misaada na ushauri kwa vikundi vinavyojihusisha na uhifadhi wa misit

Aina za uwezeshaji zinazotolewa na Mfuko

Mfuko utatoa aina tatu za uwezeshwaji kulingana na mahitaji ya walengwa. Uwezeshaji huoni:  

Msaada wa fedha;

Msaada wa vifaa; na

 Stadi/Utaalam.

 

Aina za Ruzuku Zinazotolewa na Mfuko wa Misitu Tanzania

Mfuko wa Misitu Tanzania unatoa aina tatu za ruzuku ambazo ni:

Ruzuku ndogo:  kiasi cha fedha kisichozidi shilingi milioni 5, na inatolewa kwa watu binafsi na vikundi ili kugharimia utekelezaji wa miradi midogo;

Ruzuku ya kati: kiasi cha fedha kinachozidi shilingi milioni 5na kisichozidi shilingi milioni 20; na

Ruzuku kubwa:kiasi cha fedha kinachozidi shilingi milioni 20 na kisichozidi shilingi milioni 50 na hutolewa ili kugharimia miradi inayochukua muda mrefu.

 Vipaumbele vya Mfuko wa Misitu Tanzania Mfuko

Mfuko unatoa ruzuku katika maeneo matatu ya kipaumbele ambayo ni:

  • Uhifadhi, Uendelezaji na Usimamizi wa Rasilimali Misitu kupitia shughuli za upandaji miti, uhifadhi wa misitu ya asili, uhifadhi wa vyanzo vya maji na matumizi ya nishati mbadala;
  • Uboreshaji wa Maisha ya Jamiizinazoishi pembezoni mwa misitu kupitia shughuli kama za ufugaji nyuki, ufugaji samaki nk.; na
  • Utafiti ulengao kuboresha uhifadhi na usimamizi wa rasilimali misitu

Walengwa wa Mfuko wa Misitu Tanzania

Mfuko unakaribisha maandiko ya miradi ya kuomba ruzuku kutoka watu binafsi, vikundi vya jamii, asasi zisizo za serikali, jumuiya/taasisi za kidini, asasi/taasisi za mafunzo, asasi zisizo za mafunzo, taasisi za utafiti, wizara, idara, na wakala za serikali, pamoja na mamlaka za serikali za mitaa. Hata hivyo, vikundi/asasi/taasisi zote zinatakiwa kuwa zimesajiliwa na mamlaka zinazotambulika kisheria, wakati waombaji binafsi wanatakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika/wanaoaminika.

3.0. MFUKO WA RAIS WA KUJITEGEMEA (PTF) 

Historia ya Mfuko

Mfuko wa Rais wa kujitegemea ulianzishwa 1983 chini ya sheria ya Tanzania ya “TRUST INCORPORATION ORDINANCE CHAPTER 375”. Wazo la kuanzisha kwa mfuko lilitoka kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wakati ule marehemu Edward Moringe Sokoine.Shughuli rasmi za kuanzishwa kwa mfuko huu zilianishwa rasmi mwaka 1984 na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 

Madhumuni ya Mfuko

Madhumuni ya kuanzishwa kwa mfuko wa Rais ni kuwa chombo mahsusi cha kutia msukumo wa maendeleo katika jamii hasa ya wale wenye kipato cha chini, waakina mama na Vijana, na wafanyabiashara ndogondogo waweze kujiajiri wenyewe hatimae waweze kujitegemea.

Walengwa wa Mfuko 

  • Vijana na ambao wamehitimu mafunzo mbalimbali ikiwemo ufundi stadi unatambuliwa na VETA,SIDO na vyuo vingine vya ufundi sanifu
  • Wanawake wajasiriamali walio katika sekta ya uzalishaji.
  • Kundi maalum la Vijana walemavu

Vigezo vya mikopo

1. Mikopo ya vijana

  • Uwe mkazi wa eneo lililolengwa wenye umri miaka 18-45
  1. Uwe na shughuli ya ujasiriamali inayoendana na fani uliyosomea
  2. Ujiunge katika kikundi cha watu watano waliotimiza masharti kwa Mikopo ya UMOJA na VIFAA.
  3. Uwe mhitimu katika chuo kinachotambulika na VETA, NACTE, ama umepata mafunzo ya ujasiliamali toka SIDO ama Taasisi za kijasiriamali.
  4. Uhudhurie mafunzo ya Mikopo na Ujasiriamali yatolewayo na Mfuko wa Rais kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali.

2. Mikopo ya akina mama

  • Uwe mkazi wa eneo lililolengwa
  1. Uwe  mjasiriamali katika sekta ya uzalishaji
  2. Ujiunge katika kikundi cha watu 5 hadi 20 waliotimiza masharti Kwa Mikopo ya UMOJA na VIFAA.
  3. Uwe na biashara ya uzalishaji na sio ya uchuuzi na/ama umepatiwa mafunzo ya ujasiliamali toka SIDO, VETA au Taasisi inayotoa mafunzo ya ujasiriamali, na Wana VICOBA wajasiriamali

Uhudhurie mafunzo ya Mikopo na Ujasiriamali yatolewayo na Mfuko wa Rais ikishirikiana na wadau mbalimbali.

4.0. MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE (WDF)

 Historia ya Mfuko

Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ulianzishwa kutokana na Azimio la Bunge lililopitishwa Agosti, 1993 na kwa mujibu wa kifungu 17 (1) cha Sheria ya Exchequer and Audit Ordinance (Cap 439) ya mwaka 1961 ambapo ulianza kufanya kazi mwaka 1993/94. Serikali ilianzisha Mfuko huu Kama mojawapo ya mikakati yake ya kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi kwa madhumuni ya kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili kulingana na nafasi katika familia na jamii.          

Lengo la Mfuko

Lengo kuu la Mfuko ni kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wanawake au vikundi vya wanawake wajasiriamali wadogo itakayowawezesha kuanzisha na kuendeleza miradi ya kilimo, biashara na viwanda vidogo ili kuongeza kipato, ajira na kupunguza umaskini     

Walengwa wa mfuko

Walengwa wanaotarajiwa kunufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ni kama ifuatavyo:

  • Wanawake wenye umri wa miaka 18 na kuendelea au wanawake walio chini ya umri huo ambao wana watoto;
  1. Kikundi, Kampuni ya wanawake au mwanamke mmoja mmoja; na
  2. Wanawake wajasiriamali waliojiunga katika vikundi, VICOBA au SACCOS wanaofanya shughuli za kiuchumi zikiwemo; kilimo, biashara, madini, ufugaji, usafirishaji, uvuvi na viwanda vidogo.

Vigezo vya wanufaika wa mfuko.

Fedha za Mfuko ni fedha za Umma, kwa misingi hiyo fedha hizo zinafuata Taratibu, Kanuni na Miongozo mbalimbali ya matumizi ya fedha za Umma. Baadhi ya taratibu za kuzingatia ni kama ifuatavyo:

Kila mwombaji wa mkopo lazima awe mwanachama hai wa Kikundi/VICOBA/SACCOS;

Waombaji wa mkopo watatakiwa kuhudhuria mafunzo yatakayotolewa na wataalam kabla ya kupata mkopo na wathibitishe kuwa waombaji wameelewa yote waliyojifunza;

Waombaji wa mkopo wanatakiwa kuwa na vitambulisho vitakavyowatambulisha kama vile kitambulisho cha mpiga kura, makazi na cha Taifa;

Kamati ya mikopo ya Kata, SACCOS na Halmashauri zinatakiwa kuthibitisha uwepo wa wanachama na shughuli za kiuchumi za kikundi katika eneo husika;

Fomu ya uthibitisho wa udhamini kutoka kwa wanakikundi au wanachama wa SACCOS iwepo kwa ajili ya kudhaminiana; na

Fomu ya maombi iambatane na utambulisho kutoka Serikali ya Kijiji au Mtaa kwa ajili ya utambuzi na ufuatiliaji

5.0.MFUKO WA KUTOA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI WADOGO WADOGO (SELF Microfinance Fund) 

Historia ya Mfuko

MFUKO wa SELF ni muendelezo wa majukumu yaliyokuwa yanafanywa na Mradi wa SELF baada ya Mradi kufikia ukomo wake Juni 2015. Mfuko  huu umesajiliwa kwa Sheria ya Makampuni ya mwaka 2002 chini ya Udhamini wa Serikali ‘Company Limited by Guarantree’ tarehe 4Septemba 2014 kwa namba ya usajili 112091.

MADHUMUNI /LENGO LA MFUKO

Lengo kuu la Mfuko wa SELF ni kukuza na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wa vijijini na mijini, na hivyo kuwapa fursa ya kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kujiongezea kipato ili kuondokana na umaskini. Majukumu ya Mfuko wa SELF ni kama yafuatavyo:

  • Kutoa mikopo kwa asasi ndogo za Kifedha zilizoko vijijini na mijini ili asasi hizo ziweze kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo wenye shughuli za kiuchumi;
  • Kutoa mafunzo kwa watendaji wa asasi ndogo za kifedha ili waweze kutoa huduma bora na endelevu kwa wananchi wa vijijini na mijini;
  • Kutoa mafunzo kwa wajasiriamali yahusuyo taaluma za uendeshaji miradi, kujiwekea akiba, na namna ya katambua fursa za kibiashara (business opportunities);
  • Kutoa mafunzo kwa maafisa Ushirika ili waweze kuekeleza kwa ufanisi usimamizi wa asasi ndogo za fedha hususan SACCOS;

Walengwa

Kutokana na Mfumo wa Huduma za Mfuko wa SELF; walengwa wamegawanyika katika makundi mawili (2) ambayo ni;

  • Asasi (zinazopeleka huduma ya mikopo)
  • Wajasiriamali wadogowadogo (ambao hujumuisha wanawake, wanaume na vijana wote wenye shughuli za uzalishaji).

Mfuko katika hili husisitiza wakopeshaji wawe na shughuli za uzalishaji kwa lengo la mkopaji kuwekeza katika shughuli za kuongeza kipato na kupunguza umaskini pamoja na kulipa mkopo.

6.0.MFUKO WA UTT-MFI Plc

Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo (UTT Microfinance Plc - UTT MFI) ilisajiliwa na BRELA mnamo tarehe 28 Juni 2013, chini ya sheria ya makampuni ya sheria za Tanzania (Companies Act, Cap 212, R.E 2002) na kuanza rasmi shughuli zake mnamo tarehe 1 Julai, 2013 ili kutekeleza Sera za Serikali za uwezeshaji wananchi kiuchumi hususan wenye kipato cha chini na cha kati kwa kutoa huduma shirikishi za kifedha ikiwemo mikopo yenye mashariti nafuu.

 Malengo ya Mfuko

Kutoa huduma shirikishi za kifedha na mikopo midogo midogo kwa Wananchi - mmoja mmoja, vikundi, SACCOS, NGOs, wajasiriamali wenye mitaji midogo na ya kati, na Taasisi zenye kutoa huduma kwa wananchi wenye vipato vya chini.

Kutoa huduma za Kibenki na za Kifedha kupitia miamala ya mitandao na wavuti,

Kuhamasisha na kujenga tabia ya kujiwekea akiba na kuwekeza katika mifumo rasmi ya masoko ya fedha na mitaji miongoni mwa wananchi wenye vipato vya chini,

 Kupokea amana, hati fungani, "debentures", Kuhamasisha rasilimali za ndani, kupokea na kutunza amana / dhamana na bidhaa mbali mbali za kifedha,

Kutoa huduma shirikishi za kifedha (financial inclusive services) kama vile; uwakala wa bima, uwakala wa benki, uwakala mkuu wa miamala ya fedha kupitia mifumo ya Tehama

7.0.MFUKO WA PEMBEJEO ZA KILIMO (AGITF)

Mfuko wa Pembejeo (The Agricultural Inputs Trust Fund) ulianzishwa mwaka wa 1994 kwa Sheria ya Bunge Na. 9 ya mwaka wa 1994. Kuanzishwa kwake kulitokana na sababu mbalimbali zilizoathiri upatikanaji wa pembejeo za kilimo, mifugo na Uvuvi, hususani kwa wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo wadogo ikiwa ni pamoja na:

  • Kudhoofu kwa vyama vya ushirika nchini
  • Kubadilika kwa sera ya biashara ambapo uuzaji wa pembejeo ulifanywa kwa utaratibu wa  biashara huria.
  • Mabadiliko ya sera na majukumu ya Bodi za mamlaka za mazao na hivyo kushindwa kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo.
  • Wahisani kuacha kutoa misaada kwa utaratibu wa “Open General Licence”(OGL).
  • Kuondolewa ruzuku ya pembejeo za kilimo, hususani mbolea.

Walengwa wa mikopo ya Mfuko wa Pembejeo

  1. Wakulima /Wafugaji katika vikundi kama vile:-

Mifuko ya Pembejeo ya wilaya.

Vyama vya Ushirika vya Msingi,

Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS),

Vikundi vya uzalishaji katika kilimo na ufugaji vilivyosajiliwa,

  1. Mawakala binafsi wa Usambazaji wa pembejeo za kilimo na mifugo ikiwa ni pamoja na mbolea, mbegu na madawa ya mifugo na mimea.
  2. Watu binafsi wanaotaka kuanzisha vituo vya kukodisha matrekta,
  3. Wakulima wa kawaida pamoja na wale wa kilimo cha mkataba.
  4. Mashirika yanayojishughulisha na kilimo pamoja na Taasisi za dini.

8.MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA (YDF) 

Historia ya Mfuko

Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) ulianzishwa rasmi na Serikali mwaka 1993 chini ya Sheria ya Fedha (The Exchequer and Audit Ordinance, cap 439), namba 21 ya mwaka 1961 kifungu cha 17 (1).

 Lengo la Mfuko

Lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kuwawezesha vijana kupata mitaji kwa njia ya mikopo yenye masharti nafuu ili kuanzisha au kuendeleza miradi yao ya uzalishaji mali.  Riba ya Mkopo ni asilimia 10 kwa mwaka na muda wa Mkopo ni kipindi kisichizidi miaka miwili.

Walengwa

Walengwa wa mfuko huu ni vijana wote wa Tanzania wanawake na wanaume wenye umri kati ya miaka 15 – 35. Miradi itakayopewa mikopo kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ni ile itakayoidhinishwa kwa pamoja kati ya Wizara, Mkoa na Halmashauri.

9.0.MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF)

Utangulizi

Ni Mpango wa kuwezesha kaya maskini kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu. Utekelezaji unahusisha halmashauri zote za Tanzania Bara na Unguja na Pemba. Muda wa utekelezaji ni miaka 10 iliyogawanyika katika miaka mitano kila moja.

Mpango una sehemu kuu nne:

  • Uwasilishaji fedha kwa kaya maskini: Kutoa ruzuku kwa kaya maskini sana hususan zenye watoto ili ziweze kukidhi mahitaji muhimu yakiwemo huduma za elimu na afya. Pia kutoa ajira za muda kwa kaya maskini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi wakati wa kipindi cha hatari.
  • Kuongeza kipato kwa kaya maskini kupitia uwekaji akiba na kukuza kiuchumi ili kuimarisha kaya za walengwa kwa kuwa na vyanzo vingi vya kuzalisha kipato kwa kutumia utaalamu na teknologia za kisasa.
  • Kuongeza kipato na kuboresha miundombinu inayolenga sekta za elimu, afya na maji.
  • Kujenga uwezo katika ngazi zoteza utekelezaji. Kaya iliyoandikishwa itapata huduma zitolewazo na vitengo vyote.
  •  

Walengwa wa Mpango

Ni kaya maskini Sana zinazoishi katika mazingira duni na hatarishi zilizoorodheshwakwenye daftari la mpango.

Vigezo vya kaya maskini ni:

  • Ina kipato cha chini sana na si cha uhakika ukilinganisha na kaya zingine za kijijini, mtaani au katika shehia.
  • Haiwezi kumudu au haina uhakika wa kupata milo mitatu kwa siku.
  • Inaishi kwenye makazi duni sana.
  • Kaya yenye watoto wenye umri wa kuwa shule lakini hawajaandikishwa au wameacha shule kwa kushindwa kumudu mahitaji muhimu.
  • Ina watoto ambao hawaendi kliniki kupata huduma za afya.

10. MFUKO WA KUENDELEZA WAJASIRIAMALI WANANCHI (NEDF) 

 

Historia ya Mfuko

Mfuko wa kuendeleza Wajasiriamali Wananchi (NEDF) ulianzishwa mwaka 1994 kwa Azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mfuko huu unaendeshwa na shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) chini ya Makubaliano maalumu na Serikali Kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara, Masoko na Uwekezaji.

Madhumuni na Walengwa wa Mfuko

Madhumuni ya Mfuko ni kutoa mikopo kwa wenye viwanda vidogo na wafanyabiashara wadogo Tanzania Bara kwa lengo la kuondoa umasikini kwa kuanzisha na  kuendeleza miradi yao katika sekta ya uzalishaji inayohusika na viwanda vidogo, kilimo na kusindika vyakula (matunda na mboga), ufugaji na madini, sekta ya biashara inayohusika na uuzaji wa vyakula na vinywaji, maduka ya bidhaa mchanganyiko.Sekta nyinginezo ni kama vile afya (maduka ya dawa  baridi), huduma za uchapishaji, ujenzi, utalii na uchukuzi.

Masharti/Vigezo vya utoaji Mikopo chini ya mfuko huu

  • Muombaji awe ni raia wa Tanzania
  • Mradi/Biashara unaoombewa mkopo uwe umeasajiliwa kihalali na wenye uwezo wa kukopesheka
  • Makazi ya Muombaji yawe ya kudumu na yanatumbulika na kiongozi wa serilali za Mitaa
  • Muombaji wa mkopo awe nie mmiliki halali wa Mkopo
  • muombaji awe na uwezo na nia ya kurejesha mkopo kwa muda uliopangwa
  • Muombaji wa mkopo awe tayari kufungua akaunti ya Benki kwa jina la biashara yake
  • Kwenye mikopo ya mtu mmoja mmoja  muombaje awe na wadhamini wawili wenye dhamana
  • Kwenye Mikopo ya  Vikundi muombaji awe tayari kujiunga kwenye vikundi vya  mshikamano na kuweka akiba ya mkopo kama dhamana ya mkopo

Muundo wa Mkopo

  • Muda wa Marejesho ni kuanzia miezi 6-36 kulingana na kiwango cha Mkopo
  • Kwa mikopo ya Vikundi marejesho ya mikopo hufanyika kwa wiki au Mwezi
  • Riba ya mkopo ni asilimia 18% kwa miradi ya uzalishaji na asilimia 22% kwa miradi ya biashara
  • Kiwango cha mkopo ni hadi hadi shilingi milioni tano kwa miradi ya uzalishaji.

gsi-shirika la serikali linalotoa elimu ya kuweka barcode katika bidhaa za wajasirimali ili kuweza kutanua soko kwa wajasiriamali na bidhaa zinazozalisha nchini.

USHAURI/MAPENDEKEZO

ELIMU YA MIFUKO HII IWASILISHWE KWA JAMII KUPITIA WATENDAJI WA KATA ,MAAFISA UGANI ,WATENDAJI WA MITAA NA VIJIJI ILI JAMII IWEZE KUPATA FURSA HII NA KUWEZA KUITUMIA KATIKA KUJIENDELEZA KIUCHUMI

  • 4.0.UTAFITI WA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU.

Manispaa ya Singida  inalo jukumu la kuwawezesha watoto wanaoishi mazingira magumu  kupata mahitaji muhimu kama watoto wengine.

Utafiti ulifanyika kila kata kupata idadi ya watoto wanaoishi mazingira magumu nyumbani, wanaoishi mtaani mchana na jioni wanarudi nyumbani,na watoto wanaoishi maisha yao yote mtaani.

Matokeo ya utafiti huo ni kama ifuatavyo;

TAKWIMU ZA WATOTO WANAOISHI MITAANI MANISPAA YA SINGIDA

NA

 

KATA

UMRI-JINSI ME

UMRI-JINSI KE

JUMLA

5-7

8-10

10-13

13-15

16-18

5-7

8-10

10-13

13-15

16-18

1

IPEMBE

-

-

-

18

10

-

-

-

-

-

28

2

MAJENGO

-

-

6

12

-

-

-

-

-

-

18

3

KINDAI

-

-

-

5

16

-

-

-

-

-

21

4.

MUGHANGA

6

4

5

-

-

-

-

-

-

-

15

5

MISUNA

-

-

95

26

-

-

-

-

-

-

121

6

MITUNDURUNI

-

-

-

14

-

-

-

-

4

-

18

7

MINGA

-

-

16

-

-

-

-

4

-

-

20

8

UTEMINI

-

-

-

14

-

-

-

-

1

-

15

                                                                                  JUMLA

256

 

 

TAKWIMU YA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU MAJUMBANI.

No.
Kata
Idadi ya watoto
Umri 
Jinsia
Me     ke 
Sababu za kuishi mazingira magumu.
Mahitaji yanayotakiwa.
Maoni/ushauri.
1
Ipembe
37
1-18
23
14
Wazazi kutengana, Vifo,na umaskini.
Sare za shule, michango ya shule,na
chakula.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
2
Kindai
105
1-18
54
51
Ulevi, wazazi kutengana,umaskini,Vifo,na mimba za utotoni.
Chakula, malazi,mavazi,huduma za Afya,
sare za shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
3
Majengo
111
2-18
55
56
Kutelekeza watoto,umaskini na ulevi.
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare za
 shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
4
Mandewa
130
1-18
64
66
Wazazi kutengana, Vifo,na umaskini
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare
za shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
5
Minga
149
1-18
78
71
Kutelekeza watoto,umaskini na ulevi.
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare za
 shule,na  michango ya shule.

6
Misuna
173
1-18
85
88
Ulevi, wazazi kutengana,umaskini,Vifo,na mimba za utotoni.
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare
za shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
7.
Mitunduruni
186
1-18
102
84
Wazazi kutengana, Vifo,na umaskini.
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare za shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
8.
Mtamaa
185
1-18
108
77
Uvivu,wazazi kutengana, umaskini na vifo.
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare za
shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
9
Mughanga
117
1-18
66
51
Wazazi kutengana, Vifo,na umaskini
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare
 za shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
10.
Mtipa
284
1-18
137
147
Ulevi, wazazi kutengana,umaskini,Vifo,na mimba za utotoni
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare
 za shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
11
Mungumaji
173
1-18
103
70
Wazazi kutengana, Vifo,na umaskini
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare za
shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
12
Mwankoko
142
1-18
124
103
Umaskini,kutengana ,uzazi mwingi.
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare
za shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
13
Uhamaka
269
1-18
128
141
Wazazi kutengana, Vifo,na umaskini
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare za
shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
14
Unyambwa
82
1-18
55
27
Wazazi kutengana, ndoa za wake wengi,Vifo,na umaskini
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare
 za shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
15
Unyamikumbi
114
1-18
97
113
Ulevi, wazazi kutengana,umaskini,Vifo,na mimba za utotoni
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare za
 shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
16
Utemini
76
1-18
37
39
Umaskini,kutengana ,uzazi mwingi.
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare
 za shule,na  michango ya shule.
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
17
Kisaki
96
1-`18
58
38
Wazazi kutengana, ndoa za wake wengi,Vifo,na umaskini.
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare za
 shule,na  michango ya shule
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.
18
Unyianga
85
1-18
42
43
Wazazi kutengana, Vifo,na umaskini
Chakula,mavazi,huduma za Afya,sare
 za shule,na  michango ya shule
Kamati za kata na mitaa kuwawezesha  watoto.

5.0.KAMATI ZA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO NA MALALAMIKO

Kamati hii iliundwa kwa ajili ya kushughulikia  migogoro na malalamiko  chini ya mpango wa uboreshaji Miji  18 hapa nchini. Ambapo kamati hizi zimeundwa kwa kila Kata, Mitaa na Vijiji katika Manispaa ya Singida.

Majukumu ya Kamati kama ifuatavyo: 

  • Kubaini utaratibu uliowekwa chini ya Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, Sheria ya Barabara 2007, Sheria ya MipangoMiji 2007, wakati wa kufanya uthamini na uhamishaji wa wanachi kwa mujibu wa Sheria ya uchukuaji Ardhi na Fidia 2001.
  • Kuhakikisha kuwa Mamlaka za Miji katika Serikali za Mitaa inayoshiriki zinaweka nakala kwenye majalada kwa uthibitisho wa jina na nyaraka muhimu za waathirika kwa kila mradi. Nakala za nyaraka hizo kutumwa kwa ngazi ya Mtendaji Kata
  • Kutathimini usalama wa kijamii, kiafya kabla ya kukabidhi eneo la mradi kwa wakandarasi na kufuatilia endapo patakuwa na malalamiko mapya yanayojitokeza.
  • Kufuatilia shughuli za fidia zilizobaki
  • Kupata mrejesho na kupatia ufumbuzi wa malalamiko ya usimamizi wa utunzaji mazingira
  • Kufafanua na kuweka bajeti ya shughuli za kujenga uwezo wa Halmashauri katika utekelezaji wa usimamizi wa utunzaji wa mazingira kila mwaka
  • Kuangalia na kutiliamana ni maendeleo ya usimamizi wa utunzaji wa mazingira dhidi ya usimamizi wa vigezo vya utunzaji mazingira
  • Kufahamu na kusimamia tarehe za miradi yote
  • Kuhakikisha kuwa kanuni kuu za Benki ya Dunia juu ya mfumo wa usimamizi wa utunzaji na usimamizi wa mazingira zinazingatiwa.

Majukumu haya yatatekelezwa kwa kuweka kumbukumbu za malalamiko yote kwenye rejesta ikionyesha namba ya lalamiko, lalamiko kwa ufupi, hatua lilipofikia na jinsi yalivyotatuliwa.

Malalamiko haya pia yatatakiwa kuwasilishwa kwa Ngazi ya Kata au kwa Ngazi ya Mtaa.

iii)UWEZESHAJI WA VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA

Manispaa ya Singida kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo  wamekuwa wakiwasaidia wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi.Kwa kuhamasisha wananchi kujiunga kwenye  vikundi kwa lengo la kupeana ujuzi wenyewe kwa wenyewe na kukuza mitaji yao,juhudi za vikundi zimeungwa mkono kupitia Mapato ya ndani, Serikali kuu,na Wadau mbalimbali wa Maendeleo.

 

MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE  NA VIJANA


Mwaka
Idadi ya Vikundi
Idadi ya wanachama 
Kiasi kopeshwa
Kiasi pokelewa toka Wizarani
Jumla


2016/2017

15

280

8,000,000

33,700,000

41,700,000


2017/2018

7

107

7,000,000


7,000,000


Jumla

22

767

15,000,000
33,700,000
59,850,000


   

 

 

 

        


 

             

MCHANGANUO WA IDADI YA ASASI NA VIKUNDI VYA MANISPAA  YA SINGIDA


NA

KATA

NGOs

CBOs

FBOs

VICOBA

VIKUNDI VYA WANAWAKE

VIKUNDI VYA VIJANA

SILC

VIKUNDI VYA WAVIU
MAKUNDI MAALUMU
JUMLA

1

Utemini

1

18


17

10

3


2


51

2

Majengo

2

23

1

16

5

7

4

5


63

3

Ipembe

11

25

1

7

7

4

3



58

4

Minga

1

14


6

12

3

3

4


43

5

Mughanga

10

13


10

4

3




40

6

Misuna

2

27

1

3

10

7

14

2


65

7

Mwankoko

1

11

1

1

4

3

1



22

8

Unyamikumbi

11



4

3

6



24

9

Mtamaa

11



3

1

4



19

10

Unyambwa

9



1

1




11

11

Mitunduruni

6

15

1

14

10

8

5

4


63

12

Mtipa

5


1

3

2

3



14

13

Mandewa

2

16


12

3

8


2


43

14

Kindai

29

3

9

13

4


5

1

64

15

Mungumaji

6



5

1

1

1


14

16

Uhamaka

4



1


3



8

17

Uyianga

1

3


1






5

18

Kisaki

1

11


5

3

2




22

Jumla

38

251

8

102

98

60

47

25

1

630

    

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.