• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI KUU YA CHAMA YAFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KATIKA MANISPAA YA SINGIDA

Posted on: July 14th, 2023

Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini wameeleza kuridhishwa na kufurahishwa na utekelezaji mzuri wa ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025 katika Manispaa ya Singida.

Hayo yameelezwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Singida Mjini jana tarehe 13 Julai, 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) mjini Singida.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragili amesema, Manispaa ya Singida kupitia Idara zake zote na Vitengo, imeweza kutekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa kipindi cha Januari- Juni  2023 kwa ufanisi huku akiitaja Miradi ya maendeleo kutekelezwa kwa kiwango chenye ubora na kukamilika kwa  wakati.

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za msingi, ujenzi wa shule mpya 02 kupitia mradi wa BOOST , ujenzi na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa pamoja na vyoo na ujenzi wa jengo jipya la Utawala la Manispaa ya Singida kwa fedha za serikali kuu. Uwezeshaji wa wananchi kupitia TASAF ni moja ya miradi iliyowasilishwa.

Miradi mingine ni pamoja na  ujenzi wa kituo kipya cha afya Mtipa, Ujenzi wa machinjio mapya, ununuzi wa malori 02 ya ubebaji taka, ununuzi wa kifaa cha kisasa cha upimaji ardhi yote ikitekelezwa kupitia fedha za  Mapato ya ndani.

Mhandisi Muragili aliitaja miradi ya taasisi za serikali kuwa ni pamoja na mradi wa mabwawa ya maji taka unaotekelezwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Singida (SUWASA), Mradi wa Umeme vijijini (REA),  na Uboreshaji wa miundombinu ya barabara (TARURA).

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Mjini, Bi. Lucia Mwiru, amepongeza utekelezaji wa Ilani katika Manispaa na kusema yote yamewezekana kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Serikali na Chama.

Mwenyekiti huyo ametoa msisitizo katika suala la usafi na mazingira lakini pia kwa idara ya Ardhi kuongeza bidii katika kuhakikisha wanaondoa kero zinazowakabili wananchi.

Mwenyekiti Mwiru amehimiza ushirikiano wa vingozi wa chama na serikali katika ngazi zote na kusema kwa njia hii, uwazi utakuwepo na hivyo kuondoa dhana zisizo sahihi hasa katika utekelezaji wa miradi.

Mwiru ameagiza watendaji wa Kata na mitaa kutoa taarifa za utekelezaji wa ilani kwa wananchi kwa kuwashirikisha viongozi wa chama ngazi ya kata na matawi.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Maulid Kiaratu, amewataka wataalamu katika ngazi zote kutumia matokeo ya sensa ili kufanya mtawanyo wa rasilimali kwa usahihi na kuhakikisha wananchi wananufaika nazo.

Meya Kiaratu amewataka Madiwani kuondoa matakwa binafsi na kuzingatia matokeo ya sensa 2022 katika kutetea Kata zao ili  kunufaisha wananchi wao .

Mstahiki Meya ametumia fursa hiyo pia kuwataka watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa kuweka kumbukumbu sahihi za maeneo ambayo yalitolewa na jamii ama watu binafsi kwa ajili ya taasisi kwa maendeleo ya wananchi ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea hapo baadae.

Naye Mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima, pamoja na kupongeza utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi, ameziomba taasisi za serikali kuandaa semina kwa ajili ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama ili waweze kuwa na uelewa mpana wa miradi wanayoitekeleza ili waweze kuisemea vyema kwa wananchi.

Aidha Mhe. Sima, amechukuwa fursa hiyo kuwaelimisha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya juu mijadala inayoendelea kuhusu Mkataba wa Bandari ili kuwawezesha kuelewa kuhusu maamuzi yaliyofikiwa na serikali na hivyo kupeleka elimu hiyo kwa wananchi.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • VIKUNDI 55 VYAPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPOKEA MIKOPO YA 10%

    June 29, 2025
  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • USAFI WA NGUVU KUELEKEA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA WAFIKIA ASILIMIA 80

    June 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.