• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAZIWA KINDAI NA SINGIDANI KATIKA MANISPAA YA SINGIDA KUINUA MAPATO KUPITIA UVUVI

Posted on: February 19th, 2022

Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kipindi cha Januri hadi mei,2022 imeweka utaratibu wa kusitisha shughuli za uvuvi ili kuruhusu Samaki kuzaliana na kulinda Mazingira ya majini.

Hayo yameelezwa leo tarehe 18 February, 2022 na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Ndg. Jeshi Lupembe  ambaye alisema pindi maziwa hayo mawili Kindai na  Singidani yatakapofunguliwa  Manispaa inatarajia kuvua kiasi cha tani 35 za Samaki zenye thamani ya Tshs. Milioni 280.

Alisema kwa tani hizo 35 sio tu Manispaa itakayokuwa imenufaika kwa kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya ndani bali pia wavuvi na wananchi wa kawaida kwa kukuza uchumi wao na kujipatia lishe kutokana na Samaki bora watakaopatikana.

Aliendelea kufafanua kuwa katika kipindi hiki ambacho uvuvi umesitishwa Manispaa kupitia wananchi na viongozi wa vijiji na mitaa inayozunguka maziwa hayo, wanaendelea kuhakikisha fukwe zinakuwa safi na kulinda Mazingira yake dhidi ya matumizi mabaya hasa ya uchugaji holela kando kando ya maziwa hayo.

Kaimu Mkurugenzi ameendelea kufafanua kuwa tayari Ofisi yake kupitia Idara ya Mifugo na Uvuvi imeshafanya mawasiliano na Mamlaka ya Bonde la kati ili kupatiwa boti ya doria kwa ajili ya kudhibiti uvuvi  haramu na kwamba katika hatua ya awali Manispaa inatumia migambo kwa ajili ya ulinzi.

Naye Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dr. Adrianus Kalekezi alisema, lengo la kufunga maziwa hayo sio kuwanyima fursa wavuvi bali kuwatengenezea mazingira ya kufanya shughuli za uvuvi zenye tija kwa kupata Samaki wakubwa ambao pia thamani yake ni kubwa.

 Alisema kwa sasa Manispaa imeunda kikosi kazi kwa ajili ya kuwadhibiti wavuvi wanaokaidi agizo la kutovua kwa kipindi hiki ambacho kinahusisha polisi, mgambo na wataalamu wa Idara.

Amewaasa wavuvi kutumika kipindi hiki kwa kujiandaa kukata leseni, kununua zana bora za uvuvi hasa nyavu zinazokubalika kwa shughuli za uvuvi , mavazi ya kujiokoa na ajali za majini ( life jackets) pia kujiunga na umoja wa wavuvi ili kuweza kutambulika na kufikika kirahisi .

Dr. Kalekezi pia alisema kwa sasa Idara yake imeainisha mialo 02 tu ikiwa ni moja ya mkakati wa kudhibiti  mianya ya kupoteza mapato lakini pia kudhibi wavuvi wanaotumia nyenzo haramu ( makokora) wanaopolekea kuharibu mazalia ya Samaki pembezoni mwa maziwa.

“Mialo hii 02 inadhibiti ukwepeshaji wa mapato pia uvuvi haramu unaomaliza samaki wakubwa ambao wanatarajiwa kutaga pembezoni mwa ziwa katika kipindi hiki ” alifafanua Dr. Kalekezi

Halmashauri ya Manispaa ya Singida ina jumla ya wavuvi 150 wanaotambulika na waliojisajili katika umoja wao ambapo mitumbwi ipatayo 42 hutumika kwa ajili ya shughuli za uvuvi katika maziwa Kindai na Singidani ambayo ni maziwa makubwa katika Manispaa ya Singida.

Aidha katika kipindi cha Julai  hadi Desemba 2021, wavuvi 22 wameweza kukata leseni ambapo kiasi cha fedha Tshs. 550,000 zimeweza kukusanywa. Zoezi la kuhamasisha  wavuvi kukata leseni linaendelea hasa katika kipindi hichi ambapo shughuli za uvuvi zimesitishwa.


Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Ndg. Jeshi Lupembe

Matangazo

  • MAPOKEZI YA FEDHA MRADI WA BOOST NA FEDHA KUTOKA SERIKALI KUU May 04, 2023
  • MAPITIO YA BAJETI 2022/2023 February 21, 2023
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA KWA SHULE 2021 November 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOFAULU MITIHANI (2022) KWA KIWANGO CHA JUU NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE MAALUM ZA VIPAJI. February 21, 2023
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MANISPAA YA SINGIDA YANG’ARISHA WATUMISHI

    May 23, 2023
  • VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KUPITIA UFUGAJI WA NYUKI

    May 21, 2023
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA NYUKI DUNIANI YATUMIKE KUJIFUNZA NA KUBADILISHANA UZOEFU

    May 19, 2023
  • WAFANYABIASHARA WATAKIWA KULIPA KODI NA ADA KUPITIA MIFUMO YA ULIPAJI YA KIELETRONIKI.

    May 16, 2023
  • Tazama Zote

Video

Waziri Jafo atoa maagizo mazito kwa ma-RAS, ma-DED, Wakuu wa idara na maasifa mawasiliano serikalini
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.