• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Maji na Usafi wa Mazingira

HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA


HUDUMA YA MAJI HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA.

Halmashauri ina vijiji 10 kati ya 19 vyenye miradi mikubwa ya maji ambayo tayari ilishakamilika. Pamoja na miradi hiyo, Vijiji vyote 19 vina pampu za mikono (Handpump)178  zinazotoa huduma ya maji. Katika vijiji 10 vyenye miradi mikubwa ya maji kuna vituo 251 vya kuchotea maji vilivyo katika maeneo mbalimbali na taasisi zikiwemo, Taasisi hizo ni Shule na vituo vya afya. Aidha, kuna mifumo kumi ya kuvunia maji ya mvua (RWH) katika majengo ya taasisi za Serikali.

HALI YA HUDUMA KATIKA MANISPAA

A. MAENEO YA MJINI

Huduma ya maji katika maeneo ya mjini hutolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Mjini Singida (SUWASA). Idadi ya watu wanaopata huduma ya maji safi na salama mjini imefikia asilimia 75 (75%) na Mamlaka bado inaendelea kutanua huduma ya maji safi na salama  kwa wateja wapya kwa kumiliki maeneo zaidi yenye vyanzo vya maji kwa kufidia wananchi ili kupisha maeneo hayo. Mfumo wa kudhibiti Maji taka ni moja ya mipango mikubwa ya SUWASA kwa siku zijazo katika maeneo yaliyotengwa na Halmashauri kupitia Mpango Kabambe wa Halmashauri (Master Plan).

B. MAENEO YA VIJIJINI.

Huduma ya maji katika maeneo ya vijijini hutolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kupitia idara ya maji.

Jitihada za kuongeza upatikanaji wa Maji safi na salama katika maeneo ya Vijijini zinaendelea kwa kuendeleza tafiti pamoja na uchimbaji wa visima katika mwaka 20172018, vijiji vinavyo fanyiwa tafiti na uchimbaji ni Mungumaji, Unyambwa, Kisasida na Unyamikumbi.

Pamoja na shughuri hizo Halmashauri inafanya Jitihada za kuendelea kuiomba  Serikali kuu kupata fedha za kuendeleza miradi ya maji. Kwa wakazi wa Vijijini asilimia 48 (48%)  ndio wanaopata huduma ya Maji safi na salama. Miradi ya maji inayotoa huduma katika maeneo ya Vijijini inasimamiwa na Kamati za maji zilizosajiliwa kisheria kwa kushirikiana na Serikali za vijiji husika na kupata mafunzo namna ya kuendesha miradi ya maji na namna ya uaandaaji wa taarifa ya mapato na matumizi na namna ya matumizi ya mapato pamoja na utunzaji wa mazingira.

 

SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA MWAKA 2017/2018.

  • Kusajili kamati za maji (COWSOs) nne.
  • Uandaaji wa michoro kwa ajili ya uchimbaji wa visima vine katika Vijiji vya Mungumaji, Unyambwa, Kisasida na Unyamikumbi. Uchimbaji wa visima hivyo vinne unaendelea.
  • Kutoa mafunzo na ufafanuzi wa sera ya maji kwa kamati za maji namna ya kuendesha miradi ya maji katika vijiji 4.
  • Uhamasishaji wa jumuiya za watumia maji juu ya kuchangia huduma ya maji ili iwe endelevu.
  • Kutoa elimu juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji.
  • Mchakato wa kumpata mkandarasi kwa ajili ya ukarabati wa miradi ya maji saba unaendelea.
  • Kufanya tafiti na uchimbaji wa visima katika vijiji vya Mungumaji, Kisasida, Unyambwa na Unyamikumbi. Mpaka sasa mkandarasi yupo site anaendelea na kazi.

MIKAKATI.

  • Kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji kwa kushirikiana na ofisi ya bonde la kati.
  • Kuendelea na uelimishaji kwa jamii kuhusu Sera ya maji inavyoelekeza.
  • Wananchi na Serikali za Vijiji vyao kuendelea kuhimizwa kuwa waangalizi wa karibu wa miundombinu ya maji na mali zingine za Serikali. Aidha, sheria ndogo za Vijiji zinatumika kikamilifu kuwaadhibu wanaoharibu miundombinu ya maji.
  • Kuendelea kuhamasisha vikundi vya watumia maji kuchangia na kutengeneza miundombinu ya maji mara inapoharibika.
  • Kutoa elimu kwa jamii juu ya teknolojia rahisi ya ujenzi wa matanki ya gharama nafuu kwa ajili ya uvunaji wa maji ya mvua.
  • Kuendelea kushirikiana na Serikali kufanya ukarabati wa miradi ya maji.
  • Kuendelea kuibua miradi mipya ya maji.

MATARAJIO.

Matarajio ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa mwaka 2017/2018 ni kukamilisha ukarabati wa miradi 7 ya maji na kuongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 48 mpaka 72. Jitihada hizi zinalenga kufikia lengo la kupunguza uhaba wa maji na kuhakikisha maji yanapatikana katika umbali usiozidi mita 400 na hivyo kumpunguzia mwananchi umbali wa kutembea kufuata maji.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 29, 2025
  • VIKUNDI 55 VYAPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPOKEA MIKOPO YA 10%

    June 29, 2025
  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • USAFI WA NGUVU KUELEKEA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.