• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Mipangomiji
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu
      • Idara ya Maji na Usafi wa Mazingira
      • Idara ya Utumishi na Utawala
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC: SINGIDA AAGIZA TAKUKURU KUSHIRIKIANA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KUONDOA RUSHWA ZA AINA ZOTE KATIKA HALMASHAURI NA TAASISI ZA UMMA

Posted on: May 1st, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Binirith Mahenge ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kuhakikisha rushwa za aina zote zinakomeshwa katika Halmashauri na Taasisi mbalimbali za Umma.

Dr. Mahenge ameyasema hayo katika maadhimisho ya Sherehe ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) zilizoadhimishwa kimkoa katika uwanja wa Namfua Mkoani Singida.

Alisema amefarijika kusikia katika risala iliyosomwa na Mratibu wa TUCTA mkoa kuwa rushwa ya ngono imepungua kwa kiasi kikubwa katika Taasisi za umma hivyo kutoa agizo kwa TAKUKURU kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kuondoa rushwa zote makazini.

Aidha amesema waajiri na waajiriwa kwa Pamoja wanapaswa kuzingatia sheria Na. 6 ya mwaka 2004 ili kuhakikisha uadilifu na haki vinazingatiwa katika utoaji huduma katika taasisi zote.

Kuhusu suala la waajiri kuchelewesha michango ya Watumishi katika mifuko ya hifadhi ya ya Jamii, Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ,ameiagiza TUCTA kuwasilisha kwake orodha ya waajiri wanaochelewesha michango ya waajiriwa sambamba na madai ya waajiriwa ili aweze kushughulikia nao.

Amewaasa Watumishi kujenga utamaduni wa kutembelea mifuko ya hifadhi ili kujua taarifa za michango yao badala ya kusubiri muda wa kustaafu unapofika ili kuepuka usumbufu.

Pamoja na masuala mengine ya Maendeleo Dr. Mahenge ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa miradi ya Maendeleo katika nyanja za elimu, afya, barabara na TASAF ambapo kwa mkoa waSingida kiasi cha takribani Tshs. Bilioni 232 zimepokelewa kwa ajili ya miradi ya Maendeleo

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bi. Doroth Mwaluko amewapongeza watumishi kwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuwataka kufuata taratibu za kiutumishi kwa umakini zaidi ili kuhakikisha shughuli za maendeleo na huduma kwa wananchi hazikwami.

“nimeona mnacheza vizuri mziki wa kwaito kwa kufuata step barabara, vivyo hivyo mfuate step za kiutumishi katika utekelezaji wa majumu yenu” alisisitiza Bi. Mwaluko.

Mratibu wa wa TUCTA Bi. Susan Shashi kupitia risala amepongeza watumishi wote kwa utekelezaji mzuri wa majukumu na hasa Wakurugenzi waliotoa kipaumbele kwa mabaraza ya wafanyakazi kufanyika katika kipindi cha bajeti na tahmini ya utekelezaji wa shughuli za Maendeleo kwani yameleta ufanisi mkubwa katika utekelezaji shughuli za Maendeleo.

Aidha Bi Suzan amewataka Wakurugenzi kuhakikisha wanalipa kwa wakati fedha za uhamisho wa watumishi pindi unapofanyika ili kuepuka kuleta usumbufu kwa mtumishi/Watumishi waliohamishwa. Pamoja na malipo ya uhamisho ametaja masuala mengine ambayo yanaleta usumbufu kwa Watumishi kuwa ni Pamoja na madai mbalimbali ya shahiki zao na adhabu zinazotolewa kwa Watumishi bila sababu za msingi.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa dini mbalimbali katika mkoa wa Singida Mwenyekiti wa Dini Mbalimbali ambaye pia ni Diwani wa kata ya Misuna Mhe. Hamis Momahed Kisuke amewataka watumishi kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuepuka dhuluma ili haki itendeke na amani itawale.

“Ndugu zangu watumishi jitahidini kuepuka dhuluma ili haki itendeke kwani bila haki amani inatoweka na hivyo migogoro kuibuka”, aliasa Mhe. Kisuke

Watumishi wa Idara ya Afya katika Manispaa ya Singida wakipita kwa madaha mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Binirith Mahenge katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani


Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Ndg. Kulaga Kanyanga ( Mwenye Miwani) akisikiliza kwa makini risala iliyosomwa na Mratibu wa TUCTA mkoa wa Singida

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO March 14, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI March 07, 2022
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA KWA SHULE 2021 November 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA KWA KATA 2021 November 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • BASHUNGWA AAGIZA MAKATIBU WAKUU WA WIZARA TATU KUANDAA TARATIBU ZA UENDESHAI KITENGO CHA MAAFISA HABARI

    May 14, 2022
  • RC: SINGIDA AAGIZA TAKUKURU KUSHIRIKIANA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KUONDOA RUSHWA ZA AINA ZOTE KATIKA HALMASHAURI NA TAASISI ZA UMMA

    May 01, 2022
  • WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA MKOA WA SINGIDA WAPEWA SIKU 2 KUHAKIKISHA VIBAO VYA ANWANI ZA TAASISI VINASIMIKWA

    April 27, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA MUUNGANO: RC SINGIDA APIGA MARUFUKU VIFUNGASHIO VYA VITUNGUU VISIVYOTHIBITISHWA NA SERIKALI

    April 26, 2022
  • Tazama Zote

Video

Waziri Jafo atoa maagizo mazito kwa ma-RAS, ma-DED, Wakuu wa idara na maasifa mawasiliano serikalini
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.