• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAKABIDHIANO YA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA SINGIDA YAFANYIKA

Posted on: February 11th, 2022

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Yagi Kiaratu  amemwelezea Mkurugenzi aliyemaliza muda Ndg. Zefrin Lubuva kuwa ni mchapa kazi kwani kwa kipindi kifupi ameweza kuifanya Manispaa Singida ikaonekana kwa mabadiliko chanya aliyoyafanya hasa katika suala zima la ukusanyaji mapato Kutoka nafasi za mwisho hata kufikia nafasi ya nne (4) katika Manispaa 20 kwa kusimamia vyema vyanzo vya mapato.

Mhe. Yagi aliyasema hayo katika hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi baina ya Mkurugenzi aliyemaliza muda na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ambayo pia yalishuhudiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Singida

“Lubuva alisimamia vyanzo 5 kwa umakini vikatufanya Manispaa ya singida tuonekane”, alisisitiza mstahiki meya na kuongeza kuwa ni wakati sasa wa kujipanga vyema ili kukusanya zaidi kupitia vyanzo vyote vya mapato.

Mhe. Yagi amemwagiza Kaimu Mkurugenzi kuhakikisha kila mkuu wa Idara anakuwa na chanzo cha mapato cha kusimamia ili pindi panapotokea ulegevu ajulikane wa kumwajibisha. Pamoja na hayo Mstahiki Meya amehimiza nidhamu kwa watumishi na kusisitiza kuwa nidhamu ni msingi utakaoipeleka Manispaa ya Singida kufikia Maendeleo.

Akitoa neno la shukrani kabla ya makabidhiano, Ndg. Zefrin Lubuva aliwataka Wakuu wa Idara ambao walikuwepo kushuhudia makabidhaino hayo kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao hasa suala la ukusanyaji mapato ili kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo.

Lubuva alipongeza Baraza la madiwani kwa kuwa makini katika kusimamia utekelezaji wa miradi na ukusanyaji wa mapato na kusema ni Baraza lenye umakini linalosimamia haki na kutoa rai kwa Kaimu Mkurugenzi Ndg. Jeshi Lupembe kushirikiana vyema na madiwani ili kufikia malengo kusudiwa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida alimpongeza Mkurugenzi huyo aliyemaliza muda kwa mabadiliko chanya aliyoyafanya katika kipindi cha miezi sita aliyotumikia Manispaa ya Singida.

“Napongeza juhudi kubwa alizofanya ndugu yangu Lubuva katika kipindi kifupi ambazo zimeonesha matokeo chanya” alisema Lupembe.

Aidha amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kubadilika na kufanya kazi kwa malengo ili kuitendea haki Singida. “Sote tumeletwa hapa Manispaa ili kuitendea haki Singida kwa kufanya kazi kwa malengo ili tupate matokeo chanya” Alisisitiza Kaimu Mkurugenzi.

Mwakilishi kutoka Ofisi ya RAS, Bi Masemba Kazeni alimshukuru Ngd. Lubuva kwa kazi nzuri alizofanya kwa kipindi alichokuwepo katika uongozi wake na kumtaka Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa kusimamia vyema utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Manispaa kwani kwa kufanya hivyo atakuwa ameitendea haki nafasi ama dhamana aliyopewa.

Aidha aliwaasa Wakuu wa Idara kutoa ushirikiano kwa Kaimu Mkurugenzi ili kufanikisha azma ya kuiletea Maendeleo Manispaa ya Singida.



Mkurugenzi aliemaliza muda Ndg. Zefrin Lubuva (Kulia) akikabidhi kitabu cha taarifa ya makabidhiano kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Ndg. Jeshi Lupembe ( kushoto) huku wakishuhudiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe. Yagi Kiaratu, Mwakilishi wa RAS, Bi. Masemba Kazeni , Kaimu DAS Ndg. Alli Mwendo na wakuu wa Idara na vitengo  ( hawapo pichani)

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MEI MOSI - MAJALIWA

    April 30, 2025
  • KIKWETE AFUNGA MICHEZO UWANJA WA CCM LITI

    April 30, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.