• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

PELEKENI TABASAMU KWA WANANCHI KIUTENDAJI – PROF. SHEMDOE

Posted on: November 18th, 2025





Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewataka watumishi na viongozi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa upendo, amani na mshikamano ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa ubora na kuachiwa tabasamu kupitia huduma zinazotekelezwa na Serikali.


Akizungumza mara baada ya kupokelewa na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI katika makao makuu ya wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma, Prof. Shemdoe amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuwaachia Watanzania tabasamu ifikapo mwaka 2030, na kusisitiza kuwa TAMISEMI ina jukumu la moja kwa moja katika kutimiza azma hiyo.


Amesema watumishi wanapotekeleza majukumu yao katika ngazi ya mikoa, wilaya, halmashauri, kata, vijiji, mitaa na vitongoji wanapaswa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazoendana na mahitaji yao na kwamba tabasamu linalotarajiwa kwa wananchi linapaswa kuanzia kwa watumishi wenyewe kupitia utendaji uliokamilika na wa kuheshimu utu.


Aidha, Prof. Shemdoe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua kuongoza wizara hiyo, pamoja na wananchi wa Lushoto waliompa ridhaa ya kuendelea kuwatumikia kama Mbunge wa Jimbo hilo.


Kwa upande wa Naibu Waziri anayeshughulikia afya,Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe.Reuben Kwagilwa amesema wizara itaendelea kuongeza ushirikiano na ufanisi ili kuhakikisha sekta hiyo inatoa huduma bora zinazochochea maendeleo na kuongeza tabasamu kwa wananchi.


Naye Naibu Waziri wa anayeshughulikia masuala ya Afya TAMISEMI, Mhe.Dkt. Jafar Seif, amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano ili kuboresha huduma za Afya hususan katika ngazi ya Afyamsingi ambazo zinawagusa wananchi moja kwa moja.


Mapema leo, Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka mawaziri wote wateule kutekeleza kwa kasi ahadi 100 za Serikali ya Awamu ya Sita ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za uhakika na kwa wakati.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • WAZIRI MKUU AWATAKA WANANCHI WA MANISPAA YA SINGIDA KUTOCHOCHEA VURUGU

    November 21, 2025
  • DONDOO YA YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO WA HADHARA WA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA, ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA BOMBADIA, SINGIDA

    November 21, 2025
  • ELIMU YA LISHE YATOLEWA MANISPAA YA SINGIDA

    November 21, 2025
  • UKATILI NI CHANZO CHA UMASIKINI

    November 20, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.