• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATENDAJI SINGIDA WATAKIWA KUELIMISHA WAKULIMA JUU YA UBORA WA MBEGU YA RUZUKU YA ALIZETI AINA YA RECORD

Posted on: January 5th, 2024


Watendaji Singida wametakiwa kuitisha mikutano ya hadhara Ili kutoa elimu Kwa wananchi juu ya matumizi bora ya mbegu ya bora za ruzuku aina ya record Ili waweze kuzitumia katika msimu huu wa kilimo.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Singida, Moses Machali ametoa maagizo kwa Watendaji Vijiji na Mitaa wa wilaya ya Singida yenye halmashauri mbili za Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Singida na kuwataka wakulima katika halmashauri hizo kujiandikisha katika daftari kupitia watendaji wa vijiji vyao.

Machali amesema hayo katika Kikao kazi maalum kilichofanyika leo Januari 5, 2024, katika Ukumbi wa shule ya sekondari Mwenge ambapo alisisitiza pia mbegu hizo zitauzwa kwa fedha taslim na sio mkopo.

Kikao kazi hicho kiliwahusisha Madiwani wa halmashauri hizo mbili, Maafisa Tarafa, Maafisa Ugani, Watendaji wa Kata na Vijiji.

Machali amesema Watendaji hao wanatakiwa kuwaelimisha wananchi na kuwaeleza ubora wa mbegu za record kwa kilimo chenye tija.

Katika kuhakikisha mbegu zinawakifikia wakulima kiongozi huyo amesema, kwenye mikutano hiyo itakayofanyika katika vijiji na mitaa, Watendaji wafikishe ujumbe kwa wananchi jinsi gani serikali ya awamu ya sita inavyowathamini wakulima Kwa kuwaletea mbegu za ruzuku.

Aidha amewataka watendaji hao kupitia mikutano hiyo, kuwaorodhesha wakulima watakaotumia mbegu za ruzuku za record na kiasi cha tani za mbegu kitakachitumika.

Machali amesema mkoa wa singida umepatiwa zaidi ya Tani 700 na kwamba endapo patatokea upungufu mawasiliano ya haraka yafanyike Ili kupata nyongeza ya mbegu kutoka kwa Wakala wa Kilimo (ASA).

Mkuu huyo wa wilaya ameagiza kupatiwa taarifa ya wakulima waliojiorodhesha ifikapo Januari 9, 2024 Ili kuweza kupata takwimu ya kiasi cha tani za mbegu zitakazoagizwa.

Hata hivyo, Machali alisisitiza kuwa :"Mbegu hizi zinauzwa (Mbegu za Alizeti Record) na hazikopeshwi na zitauzwa katika maeneo husika kama ilivyokuwa mwaka jana".

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.