• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DC GONDWE AENDELEA NA KASI YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MANISPAA YA SINGIDA

Posted on: April 18th, 2024

Mkuu wa  wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, amewataka wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Singida kuitumia mahakama, ili kupata haki zao, ikiwemo migogoro ya ardhi, ambayo tayari mkondo wa sheria ilishahukua hatua.

Gondwe ametoa rai hiyo, leo Aprili18,2024, wakati akitatua mgogoro wa ardhi kwa wakazi wa Kitongoji cha Unyinga, kilichopo Kata ya Mandewa, Manispaa ya Singida, ikiwa ni siku ya pili kwa ratiba yake, aliyojipangia kwa ajili ya kusikila kero za Wananchi.

“Niwaomba tuwe tunaheshimu maamuzi ya mahakama, kwa lengo la kumaliza migogoro kama hii isiyo na faida kwa jamii …yetu, mgogoro kama huu ambao tayari ulishafikishwa mahakamani na kutolewa uamuzi, unapaswa kutatuliwa kwa njia hiyo hiyo ya mahakama…,”amesisitiza Gondwe.

Aidha amewataka wataalam wa Manispaa ya Mingida, kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi wanaokabiliwa na migogoro mbalimbali, ikiwemo ile ya ardhi, ili kuepuka kuyumbishwa, hata kupoteza haki zao, kutokana na kukosa elimu ya kutosha inayohusu masuala ya sheria.

“…nawaomba wataalamu wa Manispaa, nendeni mkawape wananchi elimu ya kutosha, ili wapate uelewa zaidi juu ya haki zao…kinachohitajika hapa ni elimu tu, hii inaweza kupunguza migogoro, ikiwemo ile ya masuala ya ardhi” amesema Gondwe.

Gondwe amesema wananchi wengi wameonekana kudhulumiwa na kupoteza haki zao kutokana na  kukosa elimu na sehemu sahihi ya kutatua  changamoto husika, hata kwa suala dogo tu, hali inayopunguza ufanisi kwao, pia kukosa Imani na serikali yao.

Katika mkutano mwingine alioufanya Mkuu huyo wa Wilaya, katika viwanja vya stendi ya zamani, katika kata ya Majengo mjini Singida, aliweza kusikiliza kero mbalimbali zilizohusisha mashauri ya ndoa, mikopo umiza, mundominu ya huduma za kijamii, ikiwemo barabara na tozo za maegesho ya magari na kuzitolea maelekezo.

Picha za Matukio mbalimbali ya mikutano ya kusikiliza kero za wananchi iliyofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe:


Mkuu wa wilaya ya Singida Godwin Godwe akisikiliza kero za wananchi eneo la Stendi ya Zamani kata ya Majengo


DC Gondwe akizungumza na wananchi wa Kata ya Majengo


Mkuu wa wilaya ya Singida  Godwin Gondweakisikiliza kero ya ardhi inayowakabili wananchi wa Kitongoji cha Unyinga, katika Kata ya Mandewa


Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Unyinga wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe wakati akisikiliza kero za wananchi

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.