• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DC GONDWE APONGEZA UFAULU ,ALISISITIZA UMALIZIAJI MIRADI VIPORO

Posted on: January 24th, 2025


Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe, ameipongeza Wilaya ya Singida, hususan Halmashauri ya Manispaa ya Singida, kwa mafanikio yaliyopatikana katika matokeo ya Kidato cha Nne, ambapo Manispaa ya Singida imefanikiwa kupata ufaulu wa asilimia 91.7.

Mhe. Gondwe amesisitiza pia umuhimu wa kumalizia miradi ya viporo kwa ubora ili kuendelea kuleta maendeleo katika eneo hilo hii baada ya kupitisha mpango wa rasimu ya bajeti 2025/26.


Mhe. Gondwe aliyasema hayo Januari 24, 2025, wakati akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichojadili utekelezaji wa mpango wa bajeti wa mwaka 2023-2024 na mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha 2025-2026.


Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Maktaba ya Mwenge Sekondari, na kilihusisha Halmashauri mbili za Wilaya ya Singida, yaani Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Singida (Singida DC).


Mhe. Gondwe alieleza kwamba mafanikio hayo ya ufaulu ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa na maafisa elimu wa wilaya hiyo. Aliongeza kuwa, ingawa ufaulu wa Manispaa ya Singida umefikia asilimia 91.7, ni muhimu kuchukulia hatua za kuhakikisha kuwa kiwango hicho kinaendelea kuongezeka.


“Pongezi kwa maafisa elimu wa Wilaya ya Singida wamefanya kazi kubwa sana, tutatangaza rasmi, ila kwa Manispaa najua wana ufaulu wa asilimia 91.7. Huu si jambo dogo, nakumbuka mwaka jana ilikuwa asilimia 84.”


Aidha, Mhe. Gondwe alisisitiza kwamba mafanikio haya yanatokana na juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameongeza mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi. Aliongeza kuwa ni muhimu kumaliza miradi ya viporo ili kuhakikisha kwamba miundombinu ya elimu inaendelea kuboreshwa kwa ubora unaohitajika.


Hata hivyo, licha ya mafanikio hayo, Mhe. Gondwe alikumbusha halmashauri zote mbili kuhakikisha kwamba suala la lishe linaendelea kutiliwa mkazo katika bajeti yao. Alieleza kuwa ni muhimu kuhakikisha kwamba bajeti inaendelea kubaini na kuzingatia masuala muhimu kama lishe, ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MEI MOSI - MAJALIWA

    April 30, 2025
  • KIKWETE AFUNGA MICHEZO UWANJA WA CCM LITI

    April 30, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.