• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DC GONDWE APONGEZA WALIMU KWA MAFANIKIO, AHAMASISHA KUONGEZA UFAULU SEKONDARI

Posted on: November 23rd, 2024



Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe, amewapongeza walimu wa wilaya hiyo kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika kuboresha elimu, huku akisisitiza lengo la kuongeza ufaulu na kuondoa daraja la nne na la sifuri katika matokeo ya shule za sekondari.


Mhe. Gondwe alitoa pongezi hizo leo, Novemba 23, 2024,katika Bonanza la Mwalimu lililofanyika katika Uwanja wa Bombadia, Manispaa ya Singida.


Bonanza hilo lililoshirikisha walimu wa wilaya nzima, lilikuwa na lengo la kutambua na kuwazawadia walimu kwa kazi nzuri wanazozifanya, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha mafanikio zaidi katika sekta ya elimu.


Mhe. Gondwe alieleza kuwa wilaya ya Singida imeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya elimu, ambapo hivi karibuni wilaya hiyo ilishika nafasi ya pili, na Manispaa ya Singida kushika nafasi ya tatu.


"Nawapongeza walimu kwa kazi nzuri mnayoifanya. Mfano hivi karibuni matokeo yametoka kwa wilaya ya Singida, Singida imeshika nafasi ya pili na Manispaa ya tatu, lakini baada ya hili bonanza ninaamini kutakuwa na mabadiliko," alisema Mhe. Gondwe.


Aidha, Mhe. Gondwe alisisitiza kuwa malengo ya mwaka ujao ni kuondoa kabisa daraja la nne na la sifuri katika matokeo ya shule za sekondari.


"Kufika mwakani, tunataka kupata matokeo bora na kufuta yale madaraja ya chini – lile daraja la nne na sifuri. Hii inawezekana kwa kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula shuleni kwa asilimia 100, na juhudi zinaendelea katika hilo,".


Bonanza la Mwalimu lilikuwa pia ni fursa ya kutunukiwa walimu vyeti na zawadi kwa matokeo bora waliyoyapata katika kazi zao.


Mhe. Gondwe alieleza matumaini yake kwamba tukio hilo litakuwa chachu ya mafanikio zaidi katika shule za wilaya ya Singida, na kwamba walimu wataendelea kuongeza juhudi katika kuboresha elimu.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 29, 2025
  • VIKUNDI 55 VYAPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPOKEA MIKOPO YA 10%

    June 29, 2025
  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • USAFI WA NGUVU KUELEKEA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.