• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DC SINGIDA ASISITIZA UWEPO WA MKAKATI WA KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO WACHANGA

Posted on: March 30th, 2022

Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Mulagiri amewataka wataalamu wa afya kuhakikisha wanaweka mikakakati mizuri  inayotekelezeka ya kupunguza vifo vya Watoto wachanga kuanzia umri 0 -  28 katika Manispaa ya Singida.

Mhandisi Mulagiri aliyasema hayo katika kikao cha robo ya tatu cha afua za lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida na kuhudhuriwa na wajumbe wote ikiwemo Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Wakuu wa idara, na watendaji wa Kata ambapo mkuu huyo wa wilaya ni Mwenyekiti wa kamati hiyo.

Alisema kuna kila sababu ya idara ya Afya kuweka utaratibu wa kuwafuatilia kinamama wajawazito tangu hudhurio la kwanza la kliniki mpaka hatua ya mwisho ya kujifungua ili kuweza kubaini matatizo yanayojitokeza kwa kinamama hao katika kipindi kizima cha ujauzito.

“ kwa taarifa tulizopitia leo ni wazi kuwa bado kliniki zetu hazina uwezo wa kubaini changamoto mbalimbali za ujauzito nasisitiza pawepo na utaratibu wa kuwafuatilia wajawazito tangu hudhurio la kwanza la kliniki hadi anapoenda kujifungua” alisema Mkuu wa Wilaya.

Aidha aliwaasa kinamama wajawazito na familia zao kwa ujumla kuwa wazi  panapotokea changamoto zozote kutoka na na hali ya ujauzito ili kuweza kupatiwa msaada wa haraka kabla matatizo makubwa hayajatokea.

Mratibu wa huduma za mama na Mtoto Bi. Joyce Muyenjwa alisema sababu ni nyingi zinazopelekea  vifo vya watoto wachanga kabla ya kuzaliwa au pindi wanapozaliwa  na kutaja sababu chache ikiwa ni Pamoja na ukaaji mbaya wa mtoto  tumboni unaopelekea mtoto kujifunga na kitovu kinachomuunganisha na mama , imani za kijamii ya kutumia dawa za kuchochea uchungu, na Jamii kutoona umuhimu wa kuhudhuria kliniki mapema na badala yake hufika katika vituo vya huduma baada ya kutokea changamoto.

Aidha alisema Idara ya afya imeendelea kuwekeza katika kutoa elimu kwa mama mjamzito katika vituo vya kutolea huduma pindi wanapofika kliniki lakini pia kwa jamii nzima juu ya umuhimu wa mke na mume kuhudhuria pamoja kliniki ili kujua kwa pamoja maendeleo ya afya ya mama na mtoto aliyetumboni, pia umuhimu wa kumpeleka mtoto kliniki mara baada ya kuzaliwa mpaka atakapotimiza umri wa miaka 5.

Naye Bi. Aneth Kanywa alitoa wito kwa jamii kuacha kuwaficha ndani watoto wenye utapiamlo  mkali hivyo kushindwa kutolewa taarifa na kupatiwa huduma stahiki kwa  haraka.

AlisemaJumla ya Watoto waliobainika na kutolewa taarifa ni 15 ambao wanapatiwa huduma ya chakula dawa na kwamba kwa sasa wanaendelea vizuri.

Amesema elimu inaendelea kutolewa na watoa huduma ngazi za msingi ili Jamii iweze kuwabaini Watoto hao na kuweza kuwafikisha katika kituo cha huduma na kupatiwa huduma kwa haraka.

“Watoto wengi wenye utapiamlo wamefichwa majumbani ila tunaendelea kuielimisha Jamii ili kuweza kuwabaini na kuwatolea taarifa ili waweze kupata huduma stahiki”, alisema Bi. Aneth.

Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe , Mhandisi Paskasi Mulagiri, Mkuu wa wilaya ya Singida  alihitimisha kikao kwa kuwataka waratibu wa Lishe, mama na mtoto na Mfuko wa Afya ya Jamii kutimiza majukumu yao  kwa umakini ili kuleta ufanisi na kwamba hatomvumilia yeyote atakayezembea katika utekelezaji wa majukumu yake.

Alisema Kamati lishe ni muhimu katika mustakabali mzima wa afya ya jamii kwani lishe ni muhimu kutokana na kwamba inagusa maisha ya kila mwananchi moja kwa moja hivyo kuwataka wasimamizi na watumishi wa sekta ya afya kuwa wazalendo na wenye dhamira ya haki kwa kuwatendea haki wananchi.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • VIKUNDI 55 VYAPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPOKEA MIKOPO YA 10%

    June 29, 2025
  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • USAFI WA NGUVU KUELEKEA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA WAFIKIA ASILIMIA 80

    June 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.