• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ELIMU YA SENSA YA WATU NA MAKAZI , YAZAA MATUNDA MANISPAA YA SINGIDA

Posted on: August 23rd, 2022

ZOEZI la Sensa ya Watu na Makazi katika Manispaa ya Singida limeendelea vizuri katika maeneo yote ya Manispaa ambapo makarani walianza kazi ya kuhesabu watu katika maeneo maalum kama nyumba za kulala wageni na vituo vya mabasi na kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kuhesabiwa, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amesema kutokana na uhamasishaji wa kutosha uliofanyika wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri kwa makarani wa sensa.

"Maeneo ambayo yalikuwa na changamoto kidogo kama Wilaya ya Singida vijijini, mpaka wa Mkoa wa Manyara na mpaka wa Mkoa wa Dodoma tumeongea na wananchi na wamekubali kuhesabiwa," alisema.

Mkuu wa Mkoa  ameendelea kuwasisistizia wananchi kuacha namba za simu na taarifa sahihi majumbani mwao pindi wanapotoka kwenda kwenye shughuli zao ili makarani watakapofika waweze kuwasiliana nao na hivyo kuwawezesha kuhesabiwa.

Naye  Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri, ametoa wito kwa wananchi kutambua kuwa mipaka ya sensa si mipaka ya kiutawala na kwamba mipaka hii imetengwa kwa ajili ya maeneo ya sensa ambayo watu wa takwimu wanaitumia kujua idadi ya watu.

 Mhandisi Mulagiri ameyasema hayo kufuatia  changamoto ilijitokeza katika baadhi ya maeneo katika Halmashauri ya Singida ambapo wananchi waligoma kuhesabiwa kwa madai kuwa mipaka ya sensa haiendani na mipaka ya kiutawala.

Alisema kutokana na changamoto hiyo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ilishughulikia tatizo hilo kwa kutembelea eneo husika kuzungumza na wananchi ambao wameelimishwa na kukubali kuhesabiwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Godfrey Lupembe ambaye amekuwa akitembelea maeneo mbalimbali ili kujionea hali ya uhesbabuji inavyoendelea, amesema, mwitikio wa wananchi katika maeneo ypte aliyopita kata, vijiji, mitaa na vitongoji ni mzuri hali inayoonesha elimu kwa wananchi kuhusu zoezi la Sensa iliwafikia wananchi vyema.

“Zoezi la sensa ya watu na makazi limeanza saa sita na dakika moja usiku kwa makarani kupita katika nyumba za kulala wageni na vituo vya mabasi, walipewa ushirikiano mzuru” alisema Kaimu Mkurugenzi.

Jeshi amesema hadi sasa hakuna changamoto iliyojitokeza ambayo ingehatarisha utekelezaji wa zoezi la sensa ya watu na makazi na amewashukuru wananchi kwa ushiriiano na kuwataka kuendelea kujitokeza ili kupata haki ya kuhesabiwa.

 Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Killimbah, amesema wananchi watakapojitokeza kuhesabiwa watakuwa wameisaidia serikali inayoongozwa na CCM kupanga mipango yake ya maendeleo.

"Sisi CCM huwa tunatengeneza ilani ya chama kulingana na idadi ya watu kwa hiyo tunawaomba wananchi wajitokeze kuhesabiwa na kwa jinsi serikali ya Mkoa wa Singida ilivyofanya uhamasisha mkoa utafanikiwa katika zoezi hili," alisema.

Maeneo mengi ya Manispaa ya  Singida wananchi wameonekana wakiwa majumbani mwao kusubiri makarani ili kuweza kuhesabiwa sambamba na  maeneo ya biashara ambapo wafanyabiashara wameonesha ushirikiano kwa makarani hali iliyopelekea zoezi la sensa ya watu na makazi katika maeneo hayo kufanyika kwa amani na utulivu.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.