• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA YAWAKARIBISHA WAHESHIMIWA MADIWANI NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA UYUI MKOA WA TABORA KWA ZIARA YA MAFUNZO.

Posted on: December 28th, 2022

Waheshimiwa madiwani Pamoja na wataalamu mabalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora wamepokelewa Manispaa ya Singida kwa lengo la kujifunza namna bora ya ukusanyaji mapato,kilimo cha alizeti na Ufugaji nyuki.

Naibu Meya wa Manispaa ya Singida Hassan Mkata,amewakaribisha wageni hao kufanya ziara yao,huku akiwataka wajisikie huru na amani kwa sababu Manispaa ya Singida ni salama na kuna mambo mengi ya kujifunza hususani katika masuala mazima ya ukusanyaji mapato, ufugaji wa nyuki na kilimo cha alizeti.

 “……Karibuni sana Manispaa ya Singida,tumefurahishwa sana na ujio wenu,tunafahamu mmekuja kujifunza naamini na sisi kuna vitu tutajifunza kutoka kwenu……….”amesema Naibu Meya

Kwa upande wa Utumishi na Utawala, Afisa Utumishi na Utawala, Kulanga Kanyanga ameleza mafanikio mbalimbali katika suala zima la utawala, ikiwa ni utoaji wa motisha kwa watumishi bora zoezi linalofanyika kila mwezi,kuwatembelea na kutatua kero za watumishi wa ngazi za chini na kuanzisha uvaaji T-shirt za Manispaa kwa watumishi  inayovaliwa kila Ijumaa.

Katika suala la mapato, Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu wa Manispaa Revocatus Mohabe ametaja vyanzo mbalambali vya ukusanyaji mapato ikiwa ni Pamoja na ushuru wa huduma, ushuru wa mazao,ushuru wa vituo vya magari Pamoja na maegesho na hivi ni vyanzo vikuu vya mapato kwa Manispaa ya singida na mapato haya yanasaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo wa Manispaa ya Singida, Dr.Adrianus Kalekezi amesema kuwa kilimo cha alizeti kwa Manispaa kimechochewa kwa kuwa na viwanda vingi vinavyofikia 36 vikijumuisha viwanda vikubwa,vya kati na vidogo vinavyosaidia kukamua mafuta ya alizeti, na kusema kuwa Manispaa inategemea sana malighafi ya alizeti kutoka Halmashauri nyingine za mkoa wa Singida  na mikoa ya Jirani kama Iringa na Dodoma, kwani uzalishaji wa alizeti  kwa Manispaa ni mdogo.

Afisa Misitu na Maliasili wa Manispaa, Jacob Chibuga amesema kuwa Manispaa ya Singida ni moja ya Halmashauri zinazofanya vizuri katika uzalishaji wa asali nyingi,  asali hiyo imekuwa ikitumiwa na wenyeji Pamoja na wageni mbalimbali ,imekuwa ni moja ya uwekezaji mzuri na wenye faida, pia imekuwa moja ya vivutio vya utalii hasa uwepo wa mradi mkubwa wa ufugaji nyuki unaoitwa Kijiji cha nyuki  uliopo   kata ya Kisaki, wageni na wenyeji wamekuwa wakifika katika eneo hilo ili  kujifunza mengi kuhusu ufugaji wa  nyuki na uzalishaji wa asali.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Uyui,Said Ntahonda ameishukuru Manispaa ya Singida kwa Mapokezi mazuri,na kusema wamejifunza mengi na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi ipasavyo ili  waweze kupiga hatua Zaidi katika suala la ukusanyaji mapato,kilimo cha alizeti na ufugaji wa nyuki.

Waheshimiwa madiwani na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Uyuwi Pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida wakimsikiliza Mkurugenzi wa mradi wa Kijiji cha Nyuki.Waheshimiwa madiwani na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida wakisikiliza maelezo kuhusu mchakato mzima wa ukamuaji wa mafuta ya Alizeti katika kiwanda cha Kilimo Kwanza.


Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.