• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HONGERA MANISPAA YA SINGIDA KWA KUJALI WATUMISHI

Posted on: May 1st, 2023

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) mkoa wa Singida, limeipongeza Manispaa ya Singida kwa mwenendo wake wa kuwajali Wafanyakazi, kuanzia ngazi yachini mpaka ngazi ya juu.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambayo kimkoa yalifanyika katika uwanja wa Liti ( Namfua) Manispaa ya Singida, Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa, Agnes John, amesema Halmashauri zingine zinapaswa kuiga mfano huo.

Katika maadhimisho hayo, Mwenyekiti huyo aliitaja Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuwa zimefanya vizuri zaidi mwaka huu, kwa kujali watumishi wake, kuanzia wale wa ngazi ya chini, hadi ngazi ya juu.

“Kwa kweli safari hii ndugu mgeni rasmi Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, zimefanya vizuri sana katika kuwajali watumishi wake, naziomba Halmashauri nyingine muige mfano huu,”alisema.

Mwenyekiti huyo amefafanua kuwa, katika kujali wafanyakazi wake, Manispaa ya Singida, tayari imependekeza majina ya watumishi wanaostahili kupandishwa daraja mwakani, jambo ambalo ni nadra sana  kufanywa kwa wakati.

Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti huyo wa TUCTA, amemwomba mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, kukabidhi zawadi maalumu kwa washindi, kama njia mojawapo ya kutambua juhudi zao katika kuwajali watumishi wake.

Awali katika risala ya wafanyakazi, iliyosomwa na Mratibu wa TUCTA mkoa, Maria John Bange, ilisema kuwa pamoja na juhudi kubwa ya watumishi kazini, bado watumishi hao wana madai kadhaa, ambayo yakitatuliwa yataboresha mazingira ya kazi.

Ametaja baadhi ya kero hizo ni mishahara midogo isiyoendana na mahitaji halisi ya sasa, tatizo sugu la rushwa ya ngono katika harakati ya kutafuta ajira, ambalo hata hivyo hivi sasa limepungua, ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Aidha Bange amesema amani na utulivu nchini uliopo unachangia sana katika  kuchochea ufanisi kazini, kwani hivi sasa watumishi wanafanya kazi kwa utulivu na wanapata haki ya kupandishwa madaraja hasa wenye sifa bila usumbufu.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amewapongeza waajiri na wakurugenzi kwa kutambua umuhimu wa vyama vya wafanyakazi hali itakayochochea kasi ya maendeleo nchini.

Pia Serukamba ametumia fursa hiyo kupongeza vyama vya wafanyakazi, kuweza kudhibiti  tatizo sugu la rushwa ya ngono sehemu ya kazi, na akaitaka TAKUKURU, kufuatilia kwa kina ili kukomesha kabisa tatizo hili mkoani Singida.

Pia mkuu wa mkoa amezipongeza Halmashauri zinazowaendeleza kimasomo watumishi wake, kwani huo ni wajibu wao katika kuhakikisha wafanyakazi wanapata ujuzi zaidi kwa ajili ya kumudu utendaji kazi unaoendana na kasi ya maarifa ya Sayansi na Teknolojia.

Siku ya wafanyakazi Duniani huadhimishwa kila mwaka Mei Mosi ikiambatana na shamrashamra za kuwatuniku watumishi hodari kwa tuzo mbalimbali

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.