• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

INEC YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI

Posted on: May 14th, 2025


Tume Huru ya  Taifa ya Uchaguzi (INEC) leo Mei 14, 2025, katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC)imeendesha mafunzo maalum kwa Waandishi Wasaidizi, Waendesha Vifaa vya Bayometriki vya Uandikishaji (BVR) na Wasimamizi Wasaidizi Ngazi ya  Kata (AROs) katika Jimbo la Singida Mjini.

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi kuelekea zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili, linalotarajiwa kufanyika kuanzia Mei 16 hadi 22, 2025 katika Jimbo la Singida Mjini.

Jumla ya washiriki 108 wameshiriki katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Singida kutoka INEC, Bw. Lazaro Madembwa kwa kushirikiana na Maafisa TEHAMA kutoka INEC, akiwemo Jerry Mhagama, Aziza Mikindo, Mariam Sultani pamoja na Maafisa TEHAMA kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Fadhili Mshamu na Elvis Mkunta.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Bw. Madembwa alieleza kuwa lengo kuu la mafunzo ni kuwawezesha washiriki kupata uelewa wa kina na umahiri wa kutumia vifaa vya BVR, sambamba na kuzingatia taratibu sahihi za uandikishaji wa wapiga kura ili kuhakikisha uboreshaji huo unafanyika kwa ufanisi na kwa kuzingatia sheria.

Hata hivyo,  kabla ya kuanza kwa mafunzo, Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Singida Mjini, Bw. Edward Mboya aliwaongoza washiriki kula kiapo cha  kutunza siri na kujitoa uanachama, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha kwamba watatekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

“Tume inasisitiza uadilifu, uwazi na kufuata sheria katika utekelezaji wa zoezi hili muhimu kwa mustakabali wa demokrasia nchini,” alisema Bw. Mboya.

Zoezi la uboreshaji wa daftari linatarajiwa kuwapa nafasi wananchi ambao hawakujiandikisha awali, waliopoteza kadi au waliohama maeneo yao ya awali, kujiandikisha upya au kufanya marekebisho muhimu ili waweze kushiriki kikamilifu katika chaguzi zijazo.

Hata hivyo zoezi hili litaenda sambamba na zoezi la Uwekaji Wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.