• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAMATI ZA SHULE ZATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUHAMASISHA WAZAZI JUU YA HUDUMA YA CHAKULA SHULENI

Posted on: February 7th, 2023

Kamati za shule katika Manispaa ya Singida zimetakiwa kuhamasisha wazazi kuchangia huduma ya chakula kwa wanafunzi shuleni ili kuwawezesha kusoma na kuelewa vyema.

Wito huu umetolewa na wajumbe wa kamati ya lishe Manispaa katika kikao  cha robo ya pili kilichofanyika leo tarehe 07 February 2023 katika ukumbi wa Manispaa, baada ya Afisa Lishe wa Manispaa, Isaac Maseri, kuwasilisha taarifa yake ambayo ilionesha mwitikio usioridhisha wa utoaji huduma ya chakula shuleni.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Dr. Adrianus Kalekezi, amesema ni wakati sasa wa wazazi kuamka na kuunga mkono suala la lishe shuleni ili kumpa mwanafunzi utulivu wa akili na nguvu ya kusoma na kuelewa vyema.

“ Mwanafunzi akiwa na njaa hata akili inadumaa….. ni muda sasa kwa kamati za shule kuhamasisha wazazi waone umuhimu wa jambo hili” amehimiza Kalekezi.

Akitoa mchango, Afisa Afya Kata ya Misuna, Isack Madono amesema, wazazi wakielimishwa na kuhamasishwa zoezi la kuchangia  huduma chakula shuleni litafanikiwa kwa kiasi kikubwa , huku akitoa mfano wa namna wazazi wanajitoa kipindi cha utoaji dawa za minyoo na kichocho shuleni ambapo wazazi huwa na mwamko mkubwa wa kuchangia chakula  kutokana na kuelimisha umuhimu wa zoezi hilo.

“Issue hapa ni usimamizi thabiti kuanzia ngazi ya kata kama ambavyo zoezi la utoaji dawa za minyoo na kichocho linavyofanyika”, amesema Madono

Naye Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa, Cosmas Ngafa, akichangia hoja kuhusu huduma ya chakula shuleni, amesema kamati za shule ni kiungo muhimu sana baina ya wazazi na uongozi mzima wa shule na kata, hivyo ameshauri kamati hizo kutumiwa vyema ili kuhamasisha wazazi na kuwaelimisha ili kutekeleza azma ya kutoa huduma shuleni.

Ngafa ametoa mfano wa shule ya Sekondari Senge ambayo tayari imeanza kutoa huduma ya chakula baada ya kikao baina ya kamati ya shule na wazazi kufikia muafaka wa kuchanga fedha kwa ajili ya chakula, hali iliyotoa nafasi kwa wanafunzi kusoma katika masaa ya ziada kwa kuwa wanakuwa wameshiba.

Aidha Wajumbe wa kamati ya lishe wametoa wito kwa watoa huduma za afya  ngazi ya jamii, kupita katika kaya na kutoa elimu ya umuhimu lishe bora na hasa katika ukuaji wa mtoto ili kuondokana na tatizo la udumavu ambayo ni matokeo ya lishe duni.

Mkuu wa Idara ya  Elimu Msingi Manispaa, Omar Maje, ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo, ameshauri kuwa, mwenyekiti wa kamati ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ahakikishe kipengele cha lishe kinakuwa moja ya agenda za kudumu katika kikao cha kujadili hali ya mapato ambacho hufanyika kila mwanzo wa wiki (Jumatatu) katika Manispaa ya Singida

Amesema, kupitia kikao hicho watendaji wa Kata watapata nafasi ya kutoa taarifa ya utekelezaji masuala ya lishe katika Kata zao pamoja na kuainisha changamoto wanazokutana nazo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.

Maje ameshauri pia walezi wa Kata wafanye ufuatiliaji wa katika kata zao ili kufanikisha zoezi hili huku akiipongeza kata ya Mughanga ambayo imekuwa ikihamasisha wananchi wake katika mitaa na vikao mbalimbali.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.