• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAYA 5,396 MANISPAA YA SINGIDA ZIMENUFAIKA NA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF) DIRISHA LA SEPTEMBA - OKTOBA, 2023

Posted on: March 22nd, 2023

Kaya 5,396 za Manispaa ya Singida zimenufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini (TASAF), kwa kuwezeshwa rasilimali fedha zaidi ya Sh. Milioni 420.3/=, ikiwa ni malipo ya dirisha la Septemba-Oktoba 2022, yaliyofanyika Mwezi March, 2023.

Kaimu Mratibu wa Tasaf, Manispaa ya Singida, Yahaya Fotta, amesema, fedha zilizotolewa kwa walengwa ni nyingi kwani ni za miezi miwili ya Septemba na Oktoba, 2023, hivyo kuwaasa walengwa , kutumia vyema malipo yao ili kuwanufaisha kwa kuwaimarisha kiuchumi.

Fotta amewataka walengwa hao kujikita zaidi kwenye miradi ya uzalishaji mali hasa katika msimu huu wa kilimo lakini pia  miradi ile ya kukuza uchumi wa kaya kama ufugaji ili kuiwezesha kaya kuondokana na umaskini.

“ wahakikishe wanajikita zaidi kwenye miradi ya uzalishaji mali kupitia fedha za ruzuku wanawzozipata….mfano msimu huu ni wakili basi fedha wanazozipata ziweze kusaidia katika kilimo na pia miradi ile ya kuinua uchumi wa kaya kama ufugaji” ameasa Fotta.

Baadhi ya wanufaika wa Mfuko huo, wamelalamikia kuchelewa kutolewa kwa fedha za Septemba na October na kusema kuchelewa huko kumepelekea baadhi yao kushindwa kuwahi msimu wa kilimo kwa kukosa fedha za kununua mbegu

Mzee Iddi Kiemi , Mkazi wa Irao , Manispaa ya Singida amesema fedha hiyo ingetolewa kwa wakati, wangeweza kuwahi msimu wa kilimo na kujipatia chakula kitakacho wa kimu  kwa muda mrefu

“ nimeshachelewa msimu wa kilimo, nitanunua debe mbili za mahindi lakini nitalima viazi viazi ambavyo vitahimili msimu wa kiangazi” amesema Mzee Iddi.

Pamoja na malalamiko hayo walengwa walio wengi wameishukuru serikali kwa kutoa malipo hayo kwani wameweza kununua chakula na kulipa ada za shule kwa watoto wao.

Bi Neema Ghandya mkazi wa Kisaki B, Kata ya Kisaki Manispaa ya Singida, anasema ameweza kununua mbegu na kulima pamoja na kuikimu familia yake na kwamba ana matumaini makubwa ya mavuno kwani hali ya mazao shambani ni nzuri.

“ Nimelima nimenunua mbegu kwa kweli hali ya shamba ni nzuri tu, ….watoto wangu wanachakula kwa kweli tunaishukuru Serikali”, amesema Bi Neema

 Naye Bwana Raphael Senge Mkazi wa Kisaki A , Kata ya Kisaki, amesema, kwa fedha alizopata ameweza kununua chakula hali inayomwezesha kufanya kazi za kilimo kwa uhakika, kununua mahitaji ya shule ya watoto wake  pamoja na mahitaji mengine madogomadogo, ikiwa ni pamoja na kufanya vibarua kwa kuwa uhakika wa chakula anao.

Wananchi 5,396 wanaolipwa fedha  kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini (TASAF), wanatarajiwa kuimarika zaidi kiuchumi, kutokana na malipo waliyopata kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi, ikiwemo ile ya kilimo.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.