• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAAFISA MIFUGO KATA ZA MTIPA, UHAMAKA NA MTAMAA WAPATIWA PIKIPIKI

Posted on: December 15th, 2023


Halmashauri ya Manispaa ya Singida imepokea pikipiki 03 kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya maafisa mifugo ngazi ya kata ili kuboresha huduma za mifugo katika kata zilizopata pikipiki na maeneo ya pembezoni.

Akikabidhi pikipiki hizo leo Desemba 15, 2023 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Maulid Kiaratu, amewataka maafisa mifugo waliokabidhiwa pikipiki hizo kuzitumia kwa malengo kusudiwa na sio vinginevyo.

Makabidhiano hayo yamefanyika Makao makuu ya ofisi za Manispaa ya Singida na kushudiwa na wakuu wa Idara na Vitengo, maafisa Ugani, watendaji wa kata, mitaa na vijiji, maafisa elimu kata, maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata na watumishi wote wa makao makuu ya Manispaa.

“Ninaamini huduma za mifugo katika kata zenu na kata jirani zitaimarika na wananchi watanufaika kwa elimu ya ufugaji bora pia huduma za dawa za mifugo”, amesema Mstahiki Meya.

Pikipiki hizo zimepelekwa katika Kata za Uhamaka, Mtipa na Mtamaa ambapo pia maafisa hao watatoa huduma kwenye kata jirani baada ya kuwezeshwa vyombo hivyo vya usafiri.

Mstahiki meya amewataka maafisa ugani kushirikiana katika kuhakikisha huduma za ugani zote zinaimarika ikiwa ni pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato yatokanayo na mifugo na kilimo katika kata zao.

Awali kabla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe, amekuwa na kikao na watumishi ngazi ya kata akihimiza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na usimamizi shirikishi wa miradi pamoja na kubaini vipaumbele vya kata hizo, masuala ya usafi na mazingira, ukusanyaji mapato pamoja na kuwakumbusha wajibu wa kila mmoja katika eneo lake la kazi.

“Shirikianeni wote katika katika kusimamia miradi ya maendeleo, kuainisha vipaumbele vya kata, pia suala la usafi na mazingira na ukusanyaji wa mapato sitakuwa tayari kuwajibishwa kwa ajili ya uzembe wa watu wachache mimi najituma na nyinyi mjitume”, amesisitiza Jeshi.

“Himizeni wananchi kusafisha maeneo kuzunguka nyumba zao na mitaro pamoja na barabara mbele ya nyumba zao ni jambo la aibu kukuta takataka zinatupwa katika mitaro/ mifereji wakati viongozi mpo”, amesema Jeshi.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.