• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAFUNZO KWA WATENDAJI NGAZI YA MKOA KUONGEZA UFANISI WA ZOEZI LA UANDIKISHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Posted on: September 14th, 2024


Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema, mafunzo yanayotolewa kwa Watendaji ngazi ya mkoa, juu ya Maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, yataongeza elimu na ujuzi, wakati kwa kuboresha daftari la wapiga kura, kwa halmashauri za Wilaya, kote nchini.

Akifungua mafunzo ya siku mbili tarehe 14 Septemba, 2024 kwa Watendaji ngazi ya mkoa wa Singida katika ukumbi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) mjini Singida, Mjumbe wa Tume hiyo, Jaji Dk. Zakia Abubakari, amesema mafunzo hayo yatawajengea umahiri wa kufundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata.

Aidha Jaji Dk. Zakia Abubakar, amesema, baada ya elimu hiyo kushuka hadi ngazi ya Kata, wataenda pia kuyatoa kwa Waendeshaji wa Vifaa vya ki-biayometriki na Waandishi Wasaidizi, ambao ndio wahusika wakuu wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni.

"Ni matarajio ya Tume kuwa kutokana na mafunzo haya, kila mmoja atapata elimu na ujuzi wa kutosha,utakaomwezesha kutekeleza majukumu yake vizuri ili kufanikisha Uboreshaji wa Daftari, mafunzo haya yatawaongezea uwezo zaidi," alisisitiza.

Mafunzo haya yanahusisha namna ya ujazaji wa fomu na jinsi ya kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voters Registration System - VRS), ili kuwafanya washiriki wawe na uelewa wa pamoja, utakaowapa fursa ya kutumia vema mfumo, na vifaa vingine vya kuandikishia wapiga kura.

"Nimejulishwa kuwa, baadhi yenu mlibahatika kushiriki katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tume, ikiwemo uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika awamu zilizopita.

"Hivyo kwa kutumia uzoefu mlionao na mafunzo mtakayopatiwa, ninaamini mtafanya kazi zenu kwa weledi mkubwa, bidii na moyo wa kujituma, ili kufanikisha zoezi hili,"alisema Jaji Dk. Zakia Abubakar.

Katika hatua nyingine Jaji Abubakar, amesema, wakati wa uboreshaji wa Daftari, mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa katika vituo vya kuandikisha wapiga kura, Ili kusaidia uwazi wakati wote wa zoezi zima, lakini pia watasaidia kuwatambua waombaji wa eneo husika, hivyo kupunguza kutokea kwa changamoto zisizokuwa za lazima, na kuwataka kutoingilia majukumu ya watendaji, wakati wa zoezi hilo kituoni.

Baadhi ya washiriki, akiwemo Upendo Naftali, Afisa Mwandikishaji Msaidizi Jimbo, kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Singida, amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo na uelewa mkubwa katika kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo.

Kadhalika amesema kuwa, anaamini baada ya mafunzo, wanakwenda kuongeza idadi ya wapiga kura wapya, ambao wamefikisha umri sahihi wa kupiga kura.

Washiriki wa mafunzo hayo ni Mratibu wa Uandikishaji mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.