• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKURUGENZI MANISPAA YA SINGIDA AHIMIZA USHIRIKIANO ILI KULETA TIJA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU

Posted on: January 18th, 2025

Katika jitihada za kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi wa Umma, Manispaa ya Singida imeahidi kuimarisha ushirikiano, utakaotatua changamoto zinazojitokeza kati ya mwajiri na mwajiriwa, ili kuleta tija na utoaji huduma sawa kwa wananchi.

Akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joanfaith Kataraia amesema kuwa, ni kwa kutumia ushirikiano, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kulipa stahiki za watumishi, ndio njia pekee itakayoweza kuondoa malalamiko na  migogoro, kati ya mwajiri na mwajiriwa.

“Manispaa ya Singida itahakikisha inaweka mazingira bora ya kufanyia kazi, ambayo baadaye yatahamasisha watumishi wetu kuweza kufanya kazi zao kwa bidii na kwa ufanisi mkubwa, ambao utasaidia kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima kwenye maeneo ya kazi, na hivyo kuleta tija...

“Sisi Manispaa tutahakikisha kuwa tunafanya kazi kwa kushirikiana na wafanyakazi wenzetu katika ngazo zote, lakini kwa kuheshimiana, kwa kusaidiana ili kuhakikisha tunaijenga Manispaa ya Singida, kupitia watumishi wenzetu, kwa uwepo wa mazingira ambayo ni mazuri ya kufanyia kazi,”alifafanua Mkurugenzi

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, hatua hizi mpya hazilengi tu kuboresha mazingira ya kazi, bali pia kuinua kiwango cha utoaji huduma kwa wananchi wa Manispaa ya Singida, hali itakayoondoa kero na malalamiko kwa wananchi

Kwa upande wake Mchumi wa Manispaa ya Singida, Jeremiah Kikonge alisema, Halmashauri hiyo inatarajia kukusanya zaidi ya Sh. Bilioni 45.2 kwa mwaka wa fedha 2025/2026, kutoka kwenye vyanzo vyake na, kutumia kiasi hicho, katika kutekeleza miradi yake mbalimbali ya maendeleo na shughuli nyinginezo, ikiwemo zile za utawala.

“Mheshimiwa Mwenyekiti kwenye bajeti hii tumeweza kuweka vipaumbele vifuatavyo, ikiwemo kugharamia ukamilishaji miradi ya viporo, kwa ajili ya huduma za jamii, ikiwemo afya, elimu, na masuala ya mtambuka…kuanzisha miradi ya kimkakati, kulipa stahiki za watumishi na mazingira bora, Pamoja na ukamilishaji jengo la utawala la halmsahuri ili liweze kukamilika,”alifafanua.

Akiongea kwenye Kikao cha Baraza hilo, Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu (CWT) Mkoa wa Singida, Hamisi Mtundua, amepongeza  Bajeti ya Manispaa na kusema ni nzuri, na ameomba ikafanye kazi iliyokusudiwa, ikiwemo stahiki zote za Watumishi, wakiwemo Walimu, pia ikawe chachu ya kuwaletea wananchi Maendeleo.

Naye Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) mkoa wa Singida Deogratius Rugambwa, ameipongeza bajeti ya 2025/2026 na kusema imemjali mfanyakazi kwa sehemu kubwa sambamba na miradi ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAABARA YA KISASA SHULE YA SEKONDARI KINDAI

    June 19, 2025
  • SHULE MPYA YA SEKONDARI YA MUSSA SIMA

    June 17, 2025
  • WATOTO WATAKIWA KUWA WAZI WANAPOFANYIWA UKATILI

    June 16, 2025
  • NIMESAINI NOTISI ZA KUVUNJA MABARAZA YA MADIWANI - MCHENGERWA

    June 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.