• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YAIMARISHA UNDUNGU NA USHIRIKIANO NA MANISPAA YA SULZBURG, AUSTRIA

Posted on: August 22nd, 2022

MANISPAA ya Singida imefufua undugu na ushirikiano katika masuala ya maendeleo, baina yake na nchi ya Ausria, kupitia mji wa Sulzburg, baada ya uhusiano wa pande hizo mbili kuwa kimya kwa kipindi cha miaka 8 iliyopita.

Akizungumza baada ya kutembelea maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na miradi iliyowahi kufadhiliwa na mji wa Sulzburg, chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (CDTF), Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu, alisema uhusiano baina ya miji dada hii miwili yaani Manispaa ya Singida na Sulzburg una mengi ya kukumbukwa katika maendeleo ya wananchi wa Manispaa ya Singida hasa katika kumtua mama ndoo kichwani kwa kutoa fedha za kuboresha miundombinu ya Maji kupitia Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA).

Mhe. Yagi alimshukuru mwakilishi wa Meya wa Sulzburg, Bi. Martina Berthold, kwa kuonyesha nia na utayari wa kuimarisha ushirikiano huu kwa mara nyingine na kusema kuwa utayari huu ni ishara njema na kwamba utaleta tija kwa wananchi wa manispaa zote mbili katika nyanja mbalimbali za kijamii.

Aidha, amesema kwa niaba ya wananchi wa Manispaa ya Singida anamshukuru Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sulzburg, viongzozi na wananchi wote walioona umuhimu wa kuwanywesha maji safi na salama wananchi wa Singida ambao walikuwa wakikabiliwa na tatizo la maji kwa kipindi kirefu.

“Kwa kuimarisha urafiki na ushirikiano baina ya manispaa zetu kunaenda sambamba na milango aliyofungua Mhe. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ya ushirikiano baina ya nchi mbalimbali duniani” amesema Mhe. Yagi.

Akizungumza kwa niamba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sulzaburg Mhe. Martina Berthold alisema miji hii miwili inachangamoto ambazo kwa namna moja ama nyingine zinafanana ingawa uzoefu unatofautiana  hasa katika masuala ya kimazingira kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, masuala ya kijamii na kiuchumi na kwamba anaamini kwa ushirikiano uliopo baadhi ya changamoto zitaweza kutatuliwa.

Mwakilishi huyo na timu ya wataalamu wakiwemo madiwani kutoka mji wa Salzburg, walifika katika Manispaa ya Singida, na kutembelea miradi mbalimbali iliyowahi kufadhiliwa na taifa hilo kipindi cha miaka ya 2012 na 2014 na kuahidi kuangallia uwezekano wa kuendelea kutoa ushirikiano katika kuboresha miradi hiyo.

Baadhi ya miradi iliyotembelewa ni mradi wa kuboresha huduma ya maji katika Manispaa ya Singida mwaka 1999, uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 600 na ujenzi wa kituo cha polisi katika kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani. Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na kituo cha afya Sokoine, Mradi wa udhibiti taka katika kizimba cha taka katika Kata ya majengo na  eneo la ujenzi wa kitegauchumi lililopo stendi ya Zamani pia katika Kata ya Majengo.

Kwa upande wake kaimu meneja ufundi wa Mamlaka Maji safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA), Mhandisi Richard Kasase, alieleza changamoto zinazoikabili SUWASA kuwa ni Pamoja na ongezeko la watu katika mji wa Singida, hali inayohitaji huduma zaidi ya maji  ikilinganishwa na uzalishaji wa maji uliopo kwa sasa.

Ushirikiano kati ya Manispaa ya Singida na mji wa Sulzburg, inayofahamika kama miji dada, ulianza mwaka 1984 na kuimarika hadi kufikia 2014 ambapo ulianza kufifia, hata hivyo chini ya Mstahiki Meya Yagi Kiaratu urafiki na ushirikiano  umerejea tena  kwa kushirikiana na asasi ya CIP-Trust, Singida.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.