• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YAKABIDHI VYEREHANI KWA KIKUNDI CHA VIJANA

Posted on: December 30th, 2022

HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida yakabidhi Vyerehani vitatu vilivyo ahidiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kwa kikundi cha vijana kiitwacho Chapakazi Art of Leather wakati wa ziara  yake mkoani Singida mwezi Julai.

Akikabidhi vyerehani hivyo, Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu amewasa wanakikundi kuwa na umoja na uvumilivu katika kufanya kazi ili kufikia malengo waliojiwekea na kupunguza vijana wanaozurura mtaani bila kufanya kazi na kuwa mzigo kwa jamii na serikali.

“Nawapongeza sana vijana kwa hatua nzuri mliyofikia na endeleeni kuchapa kazi kwa bidii ili kupunguza uzururaji mtaani bila kazi na kuwa na wimbi kubwa la vijana kutumia muda mwingi kucheza mchezo wa ‘pool table’ kuliko kufanya kazi zinazoleta manufaa kwa jamii na Taifa kwa ujumla”

Pia amewashauri kutumia fursa za mikopo itolewayo na taasisi mbalimbali za benki zinazotoa mikopo kwa riba nafuu kwa ajili ya kukuza biashara yao ili waweze kujikwamua kimaisha.

Mstahiki Meya amewataka kutumia vizuri mkopo waliopata kutoka mfuko wa asilimia kumi wa Manispaa ya Singida kwa manufaa ya biashara yao na kukumbuka kufanya marejesho kama inavyotakiwa.

Katika kujibu changamoto za kikundi hicho Mheshiwa Yagi Kiaratu amesema kuwa serikali itaendelea kutafuta soko kwa ajili ya biashara yao na wao wajitahidi kutafuta soko bila kutegemea serikali peke yake.

Katika kutatua changamoto ya ukosefu wa eneo la kudumu la biashara yao ambalo litakuwa rahisi kufuikiwa na wateja, Mstahiki Meya amesema kuwa kama wataendelea vizuri na biashara atawatafutia eneo la kudumu la kufanyaia biashara kabla ya kipindi cha uongozi wake kuisha.

 Kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Afisa Utumishi na Utawala Kulanga Kanyanga, aliwaasa wanakikundi watunze vyereheni hivyo, ikitokea mmoja wao amehama wasiuze vyerehani hivyo kwa lengo la kugawana fedha na kuwaomba kuwa na umoja katika kuvitunza.

 Kikundi hicho ni miongoni mwa vikundi vya vijana vilivyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, kata ya Majengo, mtaa wa Mwenge kinachojishughulisha na utengenezaji wa viatu vya Ngozi, pochi za kiume, mikanda na mikoba kilichoanzishwa oktoba 2021, kikiwa na wanachama 5.

Mh Mstahiki Meya Yagi Kiaratu kwenye picha ya pamoja na Kulanga Kanyanga mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, wenye viti wa mitaa, viongozi wa Chama, wataalamu na Wanakikundi cha Chapakazi Art of Leather


Kulanga Kanyanga mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa akimkaribisha Mh Mstahiki Meya kukabidhi vyerehani 3 kwa kikundi cha Chapakazi Art of Leather


Mh Mstahiki Meya Yagi Kiaratu akitoa nasaha kwa kikundi cha Chapakazi Art of Leather kwenye Makabidhiano ya Vyerehani.


Mh Mstahiki Meya Yagi Kiaratu, mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Mtendaji Kata, Ernest Kambona Katibu wa chama cha Mapinduzi kata ya Majengo, afisa maendeleo ya jamii na wanakikundi cha Chapakazi Art of Leather kwenye picha ya pamoja.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SINGIDA KUFANYIKA NOVEMBA 13-14, 2023 November 10, 2023
  • HATUA ZA KUPATA LESENI YA BIASHARA KUPITIA MFUMO WA TAUSI November 01, 2023
  • RAIS SAMIA AWATAKA WANANCHI KUJIELEKEZA KWENYE FURSA October 16, 2023
  • HUDUMA YA MATIBABU YA MACHO HOSPITALI YA MANISPAA YA SINGIDA October 31, 2023
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • ASILIA YA UFAULU DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA WAONGEZEKA

    December 01, 2023
  • IPOSA KUONDOA UNYANYAPAA KWA VIJANA WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA MKOANI SINGIDA

    November 28, 2023
  • UTUMISHI WATOA MAFUNZO YENYE KULENGA UTENDAJI BORA WA KAZI

    November 24, 2023
  • Maafisa Tarafa,Watendaji watakiwa kutojisahau

    November 23, 2023
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.