• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YAKABIDHI VYUMBA 50 VYA MADARASA NA SAMANI

Posted on: December 23rd, 2022

Halmashauri ya Manispaa ya Singida leo tarehe 23 Desemba, 2022 imekabidhi vyumba 50 vya madarasa vikiwa na viti na meza 2500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba aliyewakilishwa katika hafla hiyo ya makabidhiano, na Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandis Paskasi Muragili.

Kwenye makabidhiano hayo imeelezwa kuwa kukamilika kwa vyumba hivyo, kutaondoa adha waliyokuwa wakipata wanafunzi kutokana na upungufu mkubwa wa madarasa na samani uliozikabili shule nyingi za Manispaa ya Singida.

Akisoma taarifa fupi ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba 50 vya madarasa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023, Kaimu Afisa Elimu wa sekondari, Aminieli Mfinanga, amesema vyumba hivyo  vitapunguza changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa ambapo mahitaji yalikuwa vyumba 114 huku mahitaji  viti na meza yalikuwa 3100 ambapo 2500 yamepatikana kupitia mradi huo.

Afisa elimu huyo amefafanua Zaidi kuwa uwepo wa vyumba hivyo vipya 50 kutaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, kuinua ufaulu wa wanafunzi Pamoja na kupunguza tatizo la utoro. Amezitaja faida zilizopatikana kuwa ni pamoja na

ajira ya muda kwa wananchi takribani 300 wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi.

Amesema mradi huo utawezesha kusajiliwa na kufungiliwa kwa shule mpya ya sekondari ya Manga ambayo ilipata fedha za ujenzi wa vyumba 04 vya madarasa na vyoo matundu 10 yakiwemo matundu 02 ya vyoo vya walimu. Shule ya sekondari Manga ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi vyumba 02 madarasa

Akizungumza na wananchi wakati wa makabidhiano ya vyumba hivyo 50 vya madarasa, Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amepongeza kazi nzuri ya usimamizi wa mradi iliyofanywa kwa ushirikiano baina ya wananchi na wataalam iliyowezesha ukamilishaji wa mradi  kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

“ Kwa namna ya pekee niwapongeze wananchi wote, wataalam na hasa wakuu wa shule waliotekeleza huu mradi kwa kazi nzuri ya usimamizi iliyokuwa shirikishi….mmeitendea haki fedha mliyopewa kwa kazi hii”, amesema Muragili na kuongeza kuwa kazi waliyofanya ni kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  ya kutatua changamoto  mbalimbali na hasa katika sekta ya  elimu.

Pamoja na pongezi hizo, Muragili amewataka wananchi na wataalam kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali huku akisema kuwa Mheshimiwa Rais amedhamiria kutatua kero katika sekta ya elimu ambapo kwa mwaka 2023 mradi mkubwa wa uboreshaji miundombinu ya shule za msingi (BOOST) utatekelezwa nchi nzima.

“ niwasihi wananchi kujitolea nguvukazi  wakati wa utekelezaji wa miradi hii ili kuiwezesha manispaa kupata fedha zaidi kwa kuwa mradi huo hupewa fedha kulingana na matokeo ya utekelezaji”

Aidha Mhandisi Muragili amewaelekeza wakuu wa shule kuhakikisha wanapanda miti mingi katika maeneo ya shule ili kuhifadhi na kupendezesha mazingira. Agizo hili amelielekeza pia kwa wananchi wote kuhakikisha wanapanda miti isiyopungua 04 katika kaya zao na kusema kuwa miti hiyo inafaida nyingi kijamii na kimazingira.

Akihitimisha Halfa hiyo ya makabidhiano Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Maulid Kiaratu, aliishukuru serikali kwa kutatua changamoto za miundombinu ya elimu na kuwataka wananchi na hasa wanafunzi kuilinda na kuitunza kwa vizazi vya baadae.

Amesema Miradi hiyo ni matokeo ya jitihada za wananchi katika kuboresha elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa kwa nguvu zao na Rais kutambua jitihada hizo na kuona umuhimu wa kuwatua wananchi mzigo mkubwa waliokuwa nao.

“Leo Rais wetu ameona jitihada za wananchi za kuinua elimu na ameamua kuwatua mzingo, tumuunge mkono kwa kushiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa miradi hii” amesema Yagi

Jumla ya shule za sekondari 16 kati ya 19 za Manispaa ya Singida zimenufaika  na mpango wa ujenzi wa vyumba 50 vya madarasa uliyogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni moja kutoka serikali kuu.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.