• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YAPUNGUZA DARAJA SIFURI KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022

Posted on: February 4th, 2023

Manispaa ya Singida imepunguza daraja sifuri kwa matokeo ya kidato cha nne na kulifuta kabisa daraja hilo,kwa baadhi ya shule za sekondari mwaka 2022, kutokana na mikakati iliyojiwekea katika kutokomeza daraja hilo.

Hayo yamebainishwa na afisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Singida, Joseph Ngoseki, ofisini kwake, wakati akitoa ufafanuzi wa hali ya matokeo ya kidato cha nne, kwa mwaka 2022.

Ngoseki amefafanua kwamba, kwa mwaka 2022, Manispaa ya Singida imefaulisha kwa asilimia 81, hivyo kupunguza kabisa daraja la sifuri (“0”), ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2021.

Amesema matokeo hayo yameiwezesha Manispaa kuongoza katika Mkoa na Wilaya pia, kutokana na mikakati ya Idara ya Elimu Sekondari, ya kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka kadri iwezekanavyo.

Ameitaja mikakati hiyo kuwa ni, kuhakikisha Manispaa inafuta daraja la sifuri kwa kufanya Ufuatiliaji ili kupunguza utoro wa walimu na wanafunzi kwa kuweza kusimamia vyema mahudhurio yao darasani.

Mikakati mingine ni kuanzisha kitabu cha mahudhurio kwa walimu (class Journal), kwa kila mwalimu kutakiwa kusaini mahudhurio yake kila baada ya kumalizika kipindi.

Ngoseki, ameitaja mikakati mingine kuwa ni kukagua na kuhakikisha kila mwalimu anakuwa na azimio la kazi, andalio la somo na “class notes” kabla ya kuingia darasani na kufanya tathmini ya uelewa kwa wanafunzi wake pindi anapomaliza kipindi ili kubaini wale dhaifu, kwa ajili ya kupewa mafunzo ya ziada.

Mikakati mingine kwa mujibu wa Afisa Taaluma huyo ni kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mthibiti Ubora wa elimu, kuwatumia walimu mahiri ili kuwafundisha walimu wengine mada ambazo ni ngumu, kufundisha walimu namna bora ya kutunga mitihani na kutumia walimu waliotumika kusahihisha mitihani ya taifa, kwa ajili ya kufundisha namna bora za kujibu maswali.

 “Tumewaelekeza walimu Wakuu na walimu wa taaluma kuingia darasani ili kuhakikisha kile kilichofundishwa na walimu wa masomo husika, ndicho kimefundishwa?!”, amesema Ngoseki

Ngoseki amesema kuwa, pamoja na usimamizi wa karibu  kwa walimu na wanafunzi, Idara yake imejiwekea mkakati wa kila shule kufanya mazoezi ya darasani na mitihani ya majaribio kwa shule zote na pia Ki-wilaya mara kwa mara, ili kuinua taaluma.

“Mwaka jana shule yetu ya Unyianga ilikuwa ya mwisho kwa shule za Manispaa lakini pia katika ngazi ya mkoa ilikuwa ya nne kati ya shule tano za mwisho, lakini kupitia mazoezi na usimamizi wa karibu kwa walimu na wanafunzi mwaka 2022 imefanya vizuri”, amesema Afisa elimu Taaluma.

BOFYA HAPA KUTAZAMA  TATHMINI YA MATOKEO KI-SHULE

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.