• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YAZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Posted on: January 15th, 2024


Kampeni ya uhifadhi wa mazingira Kwa mwaka 2024, imezinduliwa Kwa kupanda miti zaidi ya 300 eneo la shule kongwe ya Msingi ya Kititimo katika Manispaa ya Singida.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida, Naima Chondo, amezindua kampeni hiyo Januari 15, 2024 akiungana pamoja na wanafunzi na wananchi wa eneo linalozunguka Shule ya Msingi Kikitimo katika kata ya Mungumaji mjini hapa.


Kiongozi huyo aliongoza zoezi hilo la upandaji miti akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Edward Mboya, Diwani wa Kata ya Mungumaji, Mhe. Hassan Mkata, Maafisa Tarafa Wilaya ya Singida, Wakuu wa Idara na Vitengo, viongozi wa Chama na Dini mbalimbali, wanafunzi na wananchi wa eneo la Kititimo.


Lengo la Serikali ni kuona mazingira yanatunzwa Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambapo kila wilaya nchini inatekeleza lengo hilo Kwa kupanda jumla ya miti milioni 1.5 katika maeneo mbalimbali yakiwemo makazi ya watu, taasisi za umma na binafsi, maeneo ya wazi na pembezoni mwa Barabara.


Kiongozi huyo alisema , kutokana na tabia ya wananchi wa mkoa wa singida ya kukata miti ovyo, kuchoma moto misitu na kuaribu mazingira Kwa namna mbalimbali, mkoa huu umegeuka na kuwa na mazingira ya jangwa hali inayosababisha mabadiliko ya tabianchi Kwa kubadilika Kwa majira / Vipindi vya Hali ya hewa ambavyo huleta mabadiliko ya Vipindi vya mvua na hivyo kuathiri misimu ya kilimo.


Aidha Chondo aliushukuru uongozi wa Shule ya Msingi Kititimo kwa kutoa nafasi ya kuzindua kampeni ya upandaji wa miti katika eneo hilo ambapo miti 300 ya aina tofauti ikiwemo ya matunda, mbao na ile ya vivuli imeweza kupandwa huku akisistiza suala Zima la utunzaji wa miti hiyo Kwa walimu na wanafunzi wa shule ya Kititimo.


Licha ya upandaji huo wa miti, Chondo ametoa msisitizo pia katika suala la usafi wa mazingira na kutaka kupewa kipaumbele Cha kwanza katika shule hiyo pamoja na maeneo yote ya Manispaa ya Singida ilikuepuka magonjwa ya mlipuko.


Zoezi la upandaji miti ni endelevu hasa katika kipindi hiki Cha mvua.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.