• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MARUFUKU KUTUMIA ZANA HARAMU KWA SHUGHULI ZA UVUVI KWENYE ZIWA KINDAI NA SINGIDANI, YALIYOPO KATIKA MANISPAA YA SINGIDA

Posted on: August 2nd, 2023


MKUU wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragiri, amepiga marufuku shughuli za uvuvi haramu unaotumia nyavu zisizokuwa na kiwango, kwenye ziwa Kindai na Singidani, yaliyopo katika Manispaa ya Singida, na kuonya kuwa wote watakaobaniska, watakamatwa na watafikishwa mahakamani.

Mhandisi Muragiri alitoa onyo hilo, wakati akipokea taarifa ya zoezi la  uteketezaji wa nyavu haramu, zilizotumika kwenye shughuli za uvuvi katika ziwa Kindai na Singidani, kipindi cha mwaka wa fedha Julai 2022 hadi juni 2023.

Amesema , maziwa hayo ni muhimu katika kuoingezea pato Manispaa, kutokana na shughuli za uvuvi, pamoja na  kuwaingizia wananchi kipato cha kutosha katika kumudu maisha ya familia zao lakini pia lishe kutokana na samaki wanaovuliwa.

“ natoa agizo wavuvi kusitisha matumizi ya zana haramu katika shughuli za uvuvi na wananchi wasisite kuwaripoti wale wanaoendeleza hujuma kwenye maziwa haya ili wafikishwe kwenye  vyombo vya sheria wafunguliwe mashitaka, badala ya kuteketeza tu zana zao pekee,”alisema.

Kutokana na uvuvi huo usiozingatia taratibu, Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa kuna hatari ya kuua kizazi cha samaki na kuvua vifaranga, jambo linatishia uwepo wa samaki kwenye mziwa hayo.

“Samaki ni muhimu kwa ajili ya lishe bora inayoshauriwa na wataalamu wa afya, hivyo ni jukumu letu wote kuanzia walaji, wajasiriamali hadi wavuvi kuhakikisha tunalinda kitoweo hiki kisitoweke,”amesisitiza.

Awali akitoa taarifa ya zoezi hilo, Mkuu wa idara ya Kilimo na Mifugo, Dk. Kalekezi, amesema kwa kipindi hicho, Manispaa ya Singida, iliendesha oparesheni mbalimbali za uvuvi katika mamlaka yake, ikiwemo maziwa ya Kindai na Singidani.

Alisema oparesheni hizo, zililenga kukamata zana haramu zinazotumika kwenye uvuvi, kutoa elimu juu ya uharibifu unaosababishwa na wavuvi, hasa matumizi ya zana za uvuvi zilizopigwa marufuku na serikali.

Kwa mujibu wa Dk. Kalekezi, oparesheni hizo zililenga kukamata zana haramu ili kuziteketeza, na lilifanikiwa kwa kukamata nyavu haramu zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni 7.2/-, zikiwemo Kokoro 06, nyavu za matundu madogo 25 na nyavu aina ya Monofilament 17.

Kuhusu utoaji elimu, Dk. Kalekezi amesema, kipindi hicho wameweza kufanya mikutano 25 kwenye mialo mbalimbali kuwaelimisha wavuvi na wananchi juu ya madhara ya uvuvi haramu, utumiaji wa vifaa vya kujikinga na majanga majini, utunzaji wa mazingira kwenye mialo na kuhimiza ukataji leseni za uvuvi.

Dk.Kalekezi amesema pia kwa kipindi hicho, mafanikio mkubwa yamepatikana ikiwemo kilo 3,227 za samaki kuvuliwa katika kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 zenye thamani ya Tsh. 16,135,000/=, katika maziwa hayo mawili.

Amesema kiasi kingine cha Tsh.14,300,000/= kilikusanywa na Manispaa, zikiwa ni tozo za leseni na ushuru wa samaki katika masoko mbalimbali ya Manispaa ya Singida, kwa kipindi hicho.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.