• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AHIMIZA JUU YA LISHE BORA KWA JAMII

Posted on: November 3rd, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragili ameitaka Manispaa ya Singida, kurejesha huduma ya chakula kwenye shule zote za msingi, ili kuimarisha afya ya akili, mwili na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.

Mhandisi Muragili  ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya lishe wilaya amesema hayo kwenye  mafunzo ya siku moja kuhusiana na umuhimu wa lishe bora yaliyojumuisha watendaji wa Kata, Wawezeshaji ngazi ya jamii na Wataalamu kutoka ofisi ya mganga mkuu, juu ya masuala ya lishe.

“Miaka ya nyuma tulikuwa na program ya chakula mashuleni, sasa tunairudisha, kila mwanafunzi atapatiwa chakula shuleni…tunaposema chakula, sio lazima iwe ugali au wali, hata uji wenye viini lishe unatosha,”alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Alifafanua kuwa, kuhusiana na suala hilo, tayari ofisi yake imesaini mkataba wa lishe bora na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, utakaohakikisha jamii na wadau wengine wa maendeleo, wanashiriki kikamilifu katika kutekeleza zoezi hilo.

Licha ya ofisi hizo kuingia mkataba wa lishe, Manispaa ya Singida kwa upande wake nayo imeingia mkataba kama huo na ofisi ya Mkuu wa wilaya na watendaji wa Kata zote 18, kwa ajili ya kutekeleza programu ya lishe shuleni.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe, aliwakumbusha washiriki wa mafunzo hayo, kuhakikisha wanahamasisha  suala la lishe, ikiwa ni pamoja na kuhimiza kilimo chenye kuzalisha na kuzingatia makundi yote matano ya chakula, lengo likiwa ni kuimarisha lishe tangu ngazi ya msingi.

“Lishe ni suala muhimu na ni endelevu kwa ustawi wa afya zetu, tunapozungumzia lishe, tunagusa moja kwa moja afya ya mwili na akili…lazima tujali watoto wetu kwa kuwapatia chakula kinachozingatia viini lishe vyote,”alihimiza Mkurugenzi.

Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Manispaa ya Singida, Joyce Muyenjwa, amebainsha kuwa, mtoto anapopata lishe bora kwenye kipindi cha siku 1,000 tangu kutungwa kwa mimba hadi miaka miwili, inamwepusha na maradhi mbalimbali ikiwemo tatizo la mgongo wazi.

Aidha Joyce amefafanua kuwa, mama mjamzito asipopata lishe bora, itasababisha ubongo wa mtoto kutoumbika vizuri, kupatwa na ugonjwa wa akili, mgongo wazi na hata kuwa na kichwa kikubwa, hivyo kuathiri makuzi yake.

“Mjamzito asipopata lishe bora itamsababishia upungufu wa damu, hna wakati wa kujifungua anaweza kutokwa na damu nyingi hadi kusabaisha kifo, pia asipopata lishe bora itasababisha mtoto asiumbike vizuri tumboni,” alisema Joyce.

Afisa lishe Manispaa ya Singida, Isaac Maseri, amesema hali ya lishe katika mkoa wa Singida kwa utafiti uliofanyika mwaka 2018 ilibainika kuwa  Watoto 78,373 wana udumavu sawa na asilimia  29.8 .

Aidha mesema kuwa, utafiti huo unaonyesha uwepo wa tatizo kubwa la watoto  wenye upungufu wa vitamini A, hali inayo sababisha  udumavu kwa Watoto hao, huku pia ugonjwa wa malaria na minyoo, ukielezwa kuathiri afya zao.

Mafunzo hayo ya siku moja, yaliandaliwa na idara ya afya, ustawi wa jamii na huduma za lishe, katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.