• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MURAGILI: TUMIENI MATOKEO YA SENSA KATIKA KUFANYA MAAMUZI KWA MAENDELEO STAHIKI KWA WANANCHI

Posted on: July 9th, 2023

Viongozi katika ngazi mbalimbali wilayani Singida wametakiwa kutumia matokeo ya sensa katika kufanya maamuzi yanayohusu sera na mipango ya maendeleo katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili  aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba,  wakati akifungua mafunzo ya usambazaji na matumizi ya takwimu za matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Singida Vijijini, yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwenge.

Muragili katika hotuba yake ya ufunguzi, amewataka viongozi hao kutumia matokeo ya sensa katika kufanya maamuzi pia kutathmini utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo kulingana na idadi ya watu kupitia matokeo hayo.

Mkuu huyo wa wilaya ametumia nafasi hiyo kutoa msisitizo kwa waheshimiwa madiwani kutumia matokeo ya sensa katika kutetea kata zao na sio kwa ajili ya matakwa yao binafsi.

Mhandisi Muragili amesema, matokeo hayo ya sensa yataongeza uelewa na uwazi kwa wananchi kutokana na takwimu sahihi zilizopo jambo ambalo litawapa fursa wananchi kuhoji pale maamuzi yatakapofanyika vinginevyo.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga, amepongeza mwitikio mkubwa wa viongozi kuanzia ngazi za vijiji hadi wilaya pamoja na taasisi mbalimbali katika mafunzo hayo , na kuwataka waratibu wa Sensa wa wilaya kusambaza haraka matokeo hayo ya sensa katika ngazi zote ili yaweze kutumika.

Aidha ameagiza watendaji wote wa Vijiji, Mitaa na Kata kuhuisha mara moja taarifa za Sensa katika mbao zao za matangazo ili wananchi waweze kuwa na uelewa na matokeo hayo.

Dkt. Mganga amesisitiza kuwa uwepo wa takwimu hizo ambazo ni matokeo ya sensa 2022 kutarahisisha utekelezaji wa majukumu na hivyo kutoa huduma bora kwa wananchi katika maeneo yote.

Awali akiongea kabla ya mafunzo kufunguliwa Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mussa Sima alisema matokeo ya sensa ni dira kwa mipango endelevu ya Halmashauri ambayo inatoa mwanga wa kufikia malengo kwa maendeleo kusudiwa ya wananchi.

Sima ametoa rai kwa viongozi hao, kutumia fursa hiyo ya mafunzo kwa kukaa na wataalamu katika ngazi za vijiji, mitaa na kata ili kuona namna bora ya kutumia matokeo hayo ili kufikia malengo yao.

Akihitimisha mafunzo hayo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulid Kiaratu amesema ni wajibu wa viongozi kwa kushirikiana na wataalamu kupitia matokeo ya sensa kupanga mipango ya maendeleo yenye kuona mbele ili kuweza kutoa huduma stahiki kwa wananchi kutokana na ongezeko la watu .

Mstahiki Meya amepongeza zoezi la Sensa 2022 na kusema ni sensa ya kipekee na ya kidigitali iliyojumuisha mazoezi matatu kwa wakati mmoja  ambapo ameyataja kuwa ni sensa ya watu na makazi, majengo na taasisi zinazotoa huduma pamoja na anwani za makazi.

Kiaratu amesema kutokana na matokeo ya sensa, imeonekana nguvu kazi ni kubwa hapa nchini na hasa Mkoa wa Singida, hivyo kutoa rai kwa vijana na wote wenye uwezo wa kufanya kazi kujikita katika shughuli za uzalishaji badala ya kujiingiza katika shughuli ambazo ni kinyume cha maadali .

Kwa Mujibu wa Meneja wa Takwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoa wa Singida, Naing’oya Kipuyo, Mafunzo hayo ni mfululilo wa mafunzo ya matumizi na usambazaji wa matokeo ya sensa yanayotolewa kwa makundi mbalimbali ya kijamii na kuendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu pamoja na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema dhumuni la mafunzo hayo ni kusambaza matokeo ya sensa ya watu na kakazo 2022 na  kuwajengea uwezo  wadau wote wa namna ya kutumia matokeo katika kutekeleza majukumu yao kwa wananchi hasa katika utoaji wa huduma za kijamii, tafiti mbalimbali biashara na uwekezaji.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.