• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MWENYEKITI WA CCM MKA WA SINGIDA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: February 3rd, 2023

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida, Martha Mlata, amepongeza kazi nzuri ya utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo  iliyofanywa na Manispaa ya Singida na TANROADS na kusema kuwa  ina kiwango cha ubora kinachostahili.

Mhe. Mlata, katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya  miaka 46 ya CCM tangu kuzaliwa amefanyaa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Singida, ambapo  pamoja na masuala mengine  ameweza pia kujionea hali halisi  ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Akikagua mradi wa ujenzi wa kalavati 3 katika barabara ya singida- Tabora inayopita katikati ya ziwa Kindai na Munangi, Mlata alipongeza kazi nzuri ya usimamizi wa mradi inayofanywa na TANROADS huku akiwataka wakandarasi wenginge kuiga kazi nzuri inayofanywa na Mkandarasi Kagwa General Supplies Ltd. Wa Singida

Aidha Mwenyekiti huyo amepongeza pia kitendo la TANROADS kutoa kazi ya mradi huo mkubwa kwa  mkandarasi mzawa na kusema jambo  la kuthamini wazawa linaimarisha uzalendo na kuleta mshikamanao.

 “ niwapongeze kwa kazi nzuri ya usimamizi wa mradi huu…….. nawapongeza pia kuwa kuthamini kazi za wazawa  ni jambo jema linaloleta mshikamano”, amesema Mlata.

Akisoma taarifa ya utekelzaji wa mradi huo, Kaimu Meneja wa  TANROADS Mkoa, Mhandisi Msama Kosan Msama, amesema , ujenzi huo ni matokeo ya mvua kubwa zilizonyesha 2019 zilizopelekea maziwa hayo mawili kufurika na kuungana na kusababisha sehemu hiyo ya barabara kujifunga.

Aidha amesema, eneo la tuta kati ya ziwa Kindai na Monangi lenye urefu wa KM1 ni kiungo muhimu kwa kuunganisha barabara kuu ya manyoni- Itigi- Chaya- Tabora hadi Kigoma.

Mhandisi Msama, amefafanua zaidi kuwa ujenzi wa tuta hilo unaotekelezwa katika awamu mbili, unalenga kuondoa tatizo la maji maji kufurika kutoka katika maziwa hayo  nyakati za mvua kubwa  na hivyo kusbabisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo hasa vijiji  vya Mwankoko, Mtunduru, Ighombwe  na Kintandaa.

Amesema , awamu ya kwanza inatekelezwa katika mwaka huu unaoendelea 2022/2023  ambao unahusisha ujenzi wa makalavati makubwa matatu( Box Culverts) kwa ajili ya kupumulia, upanuzi na unyauaji  wa tuta pamoja na ujenzi wa tabaka la changarawe.

Akielezea awamu ya pili ya ujenzi ambayo itatekelezwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mhandisi Msama amesema,  awamu hii itahusisha uwekaji wa tabaka la kati, tabaka la juu ya lami nyepesi na kazi za upendezeshaji ikiwemo uwekaji wa taa za barabarani, eneo la mapumziko pamoja na maegezo yake.

Hadi kufikia 31 Januari, 2023 kazi zote zilizotekelezwa ambazo ni ujenzi wa makalavati  makubwa matatu (3) ni sawa na asilimia 31 ya utekelezaji, ambapo kiasi cha Tshs. 444,119.150 kimeshalipwa kwa mkandarasi kati ya Tshs. 1,434,775,000 zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huu

Miradi Mingine aliyotembelea Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa, Martha Mlata ni pamoja na Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mandewa, Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Ititi, na Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari kata ya Uhamaka ambako kote aliendesha zoezi la upandaji miti.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.