• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RAS SINGIDA: UJENZI WA SHULE MPYA, CHUO MANISPAA YA SINGIDA UWE WA KISASA....

Posted on: January 20th, 2025


Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida (RAS), Dkt. Fatma Mganga, amesisitiza kuwa ujenzi wa shule mpya za Sekondari na Chuo cha Ufundi katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida unapaswa kufanywa kwa viwango vya juu na kuwa na mazingira ya kisasa, kutokana na namna ambavyo Serikali imewekeza fedha katika miradi hiyo.


Dkt. Mganga aliyasema hayo, Januari 20, mwaka huu, alipotembelea na kukagua ujenzi wa shule mbili mpya za Sekondari, Mwaja na Minga, pamoja na kuangalia ujenzi wa awali wa Shule ya Amali (Ufundi). Aidha, alikagua mabweni, madarasa na vyoo katika shule za Sekondari za Mandewa na Mwankonko, ambazo zinatarajiwa kupokea wanafunzi wa Kidato cha Tano ifikapo Julai mwaka huu.


Katika ziara hiyo, Dkt. Mganga alisisitiza kuwa ubora wa miundombinu, viwango vya mazingira safi, na upandaji wa miti vitafanya shule hizo mpya kuonekana za kipekee, jambo ambalo litakuwa na manufaa kwa wanafunzi kwa kutoa mazingira bora ya kujifunzia.


"Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi hii, hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa shule hizi zinakuwa na mazingira bora na ya kisasa," alisema Dkt. Mganga.


Aidha, alieleza kuwa shule mpya zinapaswa kuwa na tofauti kubwa na shule nyingine zilizopo kwa kuboresha mpangilio wa majengo, muonekano na sare za wanafunzi.


 "Kwa kuwa hizi ni shule mpya, tunapata fursa ya kufanya mabadiliko hayo, hivyo mpangilio na muonekano wa shule hizi lazima uwe wa kipekee," alisisitiza.


Dkt. Mganga pia alieleza kuwa ni muhimu kwa shule hizi mpya kuwa na walimu  na bodi za shule kuundwa mapema, ili majukumu ya uendeshaji ya shule hizo yaanze mara moja pindi zitakapokamilika.


Ziara hiyo ya Dkt. Mganga inadhihirisha dhamira ya Serikali ya kuboresha elimu katika Mkoa wa Singida kwa kuhakikisha kuwa shule za kisasa zinajengwa na kuwa na mazingira bora kwa wanafunzi kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikisisitiza na kutoa fedha nyingi.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MEI MOSI - MAJALIWA

    April 30, 2025
  • KIKWETE AFUNGA MICHEZO UWANJA WA CCM LITI

    April 30, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.