• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC DENDEGO AZINDUA MIKOPO YA 10% KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE MANISPAA YA SINGIDA

Posted on: February 15th, 2025



Leo, Februari 15, 2025, historia imeandikwa kwa mara nyingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida wakati Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, alizindua rasmi mikopo ya asilimia 10 kwa ajili ya vikundi vya wanawake, watu wenye ulemavu na vijana, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 1.1 kitatolewa kwa mwaka wa fedha 2024/25.


Uzinduzi huu ulifanyika katika Ukumbi wa Mabula Social Hall, Manispaa ya Singida, ambapo Mhe. Dendego alitangaza rasmi awamu ya kwanza ya utoaji mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 168.


Mikopo hii ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kutoa mikopo kwa vikundi vinavyohusisha makundi hayo muhimu, huku lengo kuu likiwa ni kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla na fedha hizo za mapato ya ndani ya Halmashauri.


Mhe. Dendego alipongeza Manispaa ya Singida kwa hatua hiyo muhimu na aliwahimiza wanufaika kuhakikisha fedha hizo zinatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuongeza uzalishaji na kuboresha hali ya maisha.


Aliwakumbusha vikundi vyote kuhakikisha kuwa wanatumia mikopo hii kama chachu ya kuboresha maisha yao na kuchangia katika kukuza uchumi wa mkoa.


"Niwapongeza sana Manispaa ya Singida kwa hatua hii ya kutoa mikopo ya shilingi milioni 168 leo, lakini tufahamu kwamba hii ni sehemu ya shilingi bilioni 1.1, fedha ambazo ni mali ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Tushirikiane kwa pamoja ili fedha hizi ziweze kutumika kwa faida ya wananchi wetu na kuongeza pato la mkoa wetu na taifa letu," alisema Mhe. Dendego.


Pia, aliwahimiza watendaji wa halmashauri kuongeza kasi ya utoaji wa mikopo na kushughulikia malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaosema kuwa hawapati huduma za haki. "Tutahakikisha kila mtu anapata huduma bila kubaguliwa, lakini uvumilivu pia ni muhimu katika kufuata taratibu zilizowekwa," alisisitiza Mhe. Dendego.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.