• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SERUKAMBA ARIDHISHWA NA KAZI YA UKAMILISHAJI WA MIRADI YA AFYA MANISPAA YA SINGIDA

Posted on: October 25th, 2023

Serikali Mkoani Singida imeridhishwa na shughuli ya ukamilishaji miradi ya afya na kuwataka watumishi wa sekta ya afya waliopangwa kutoa huduma katika vituo hivyo, kuhakikisha wanatoa huduma stahiki kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa  wa Singida Peter Serukamba amesema hayo Oktoba 25, 2023 katika ziara yake ya kutembelea miradi ya sekta ya afya iliyokuwa katika hatua mbalimbali za ukamilisha na ambayo kwa sasa imekamilika na kutoa huduma.

Serukamba, amewataka watumishi waliopangwa kutoa huduma katika vituo vipya vya afya na zahanati kuhakikisha watatoa huduma bora kwa wananchi na kukaa vituoni muda wote wa kazi  na kwamba hatomvumilia ambaye atashindwa kutekeleza majukumu yake ya kazi.

Aidha Serukamba pamoja na  kuridhishwa na kufurahishwa na kazi ya ukamilishaji miradi ya afya, amemtaka mhandisi wa Manispaa kusimamia miradi na kuhakikisha inatekelezwa  kwa kiwango cha ubora kulingana na thamani halisi ya fedha ( Value for Money).

Serukamba pia ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Manispaa Jeshi Lupembe na timu ya menejimenti ya kutembelea miradi mara kwa mara pindi inapotekelezwa pamoja na kukagua mpango kazi wa mafundi ili kuhakikisha kasi ya ujenzi inaendana na mpango kazi wao na kuweza kukamilisha kazi kwa wakati.

“…… mafundi ambao kazi zao zinasuasua, na kasi ni ndogo sitisha mkataba wake, tunataka mafundi wanaoendana na kasi lakini pia wanazingatia ubora”, amesisitiza Serukamba.

Akihitimisha ziara yake katika kituo cha Afya Mandewa, Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba amesema anatarajia kuanza ziara kwenye halmashauri zote saba za mkoa wa Singida lengo likiwa ni  kukagua miradi yote inayotekelezwa katika kila halmashauri ili kubaini mapungufu lakini pia kuona wapi wamefanya vizuri.

Jumla ya Vituo vya kutolea huduma (4) vimeweza kutembelewa katika Manispaa ya Singida  vikiwemo vituo 02 vya afya vya Mandewa na Mtipa na zahanati 02 za Ititi na Unyianga. Vituo vyote 04 vimekamilika kwa ubora na vinatoa huduma kwa wananchi

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.