• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SEKONDARI YA MAHARU YAZINDUA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA

Posted on: April 17th, 2024

Wakazi wa Kijiji cha Manga wameaswa kulinda na kuitunza miundombinu ya shule mpya ya Sekondari ya Maharu ili kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na serikali kwa kuwekeza katika shule hiyo sambamba na michango ya wananchi waliojitolea.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Maulid Kiaratu, amesema hayo leo Aprili 17,2024 kwenye hafla ya uzinduzi wa vyumba 02 vya madarasa yaliyojengwa kwa nguvv za wananchi na kukamilishwa na serikali kupitia mradi wa SEQUIP, katika shule ya mpya ya sekondari ya Maharu iliyopo katika Kijiji cha Manga, Kata ya Mtipa.

Mstahiki amewaeleza wazazi na wanafunzi kuwa ni jukumu lao kuitunza miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu. Aidha amewapongeza wakazi kwa mwamko wao katika kukuza elimu hali iliyowafanya kujitoa kwa hali na mali ili kuhakikisha watoto wao wanapata elimu maeneo ya karibu .

“….ninaijua historia ya shule hii ya Maharu, niwakumbushe tu ilianza baada ya ziara ya viongozi wa jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi na hapo ndipo mwamko wa ushirikishwaji kwa kuchangia elimu ulipopata mwamko. Itunzeni miundombinu hii ili kuthamini mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani , Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na nguvu zenu mlizowekeza hapa” amesema Mhe. Kiaratu.

Mstahiki Meya pia amewapongeza wazazi wenye wanafunzi katika shule ya Sekondari Maharu kwa kuitikia vyema mwito wa kuchangia chakula cha mchana cha wanafunzi ili kuwawezesha kupata utulivu na kuwa wasikivu wawapo darasani.

Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa, Geofrey Mdama, ametoa pongezi kwa Uongozi wa Kata ya Mtipa, pamoja na wananchi wa Kijiji cha Manga kwa kuthamini elimu na kuanzisha taasisi hiyo, na hivyo kuwataka kutoa ushirikiano kwa uongozi wa shule ili kufikia malengo ya kuinua elimu kwa jamii ya kata ya Mtipa na hasa Kijiji cha Manga.

Naye Kaimu Afisa elimu Sekondari, Aminieli Mfinanga amewaasa wanafunzi shuleni hapo kuhakikisha wanasoma kwa bidi na kufaulu kwa kiwango cha juu ili kuheshimisha wazazi pamoja na shule yao.

Afisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Singida, Joseph Ngoseki amepongeza jitihada zinazofanya na serikali ya awamu ya sita na kuwataka wananchi wa Kijiji cha manga pamoja na wanafunzi kuzienzi.

Aidha amepongeza jitihada zinazofanywa na Mstahiki Meya katika kuinua kiwango cha elimu kwa kushirikiana na wataalam kwa kuhakikisha miradi mingi ya elimu inatekelezwa katika Manispaa ya Singida.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Mtipa Mhe. Yusuf Ramadhan, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake za kuinua elimu nchini, pamoja na wasaidizi wake akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mhe. Mussa Sima kwa jitihada zao za kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ubora.

Mkuu wa shule ya sekondari Maharu, Mwl. Renatha Kanani, katika taarifa amebainisha kuwa shule hiyo ilifunguliwa rasmi Januari 2023 ikiwa na jumla ya walimu 06 wakiume wakiwa 04 na wakike wakiwa 02. Kwa mujibu wa Mkuu huyo,  mpaka sasa shule hiyo imeongeza idadi ya walimu na kufikia 09wakiwemo walimu wa kiume 06 na walimu wa kike 03.

Mwalimu Kanani amebainisha kuwa kati ya walimu hao 09 walimu wa Sanaa ni 06 na walimu wa sayansi  ni 03. Aidha amefafanua gharama  za ujenzi wa shule hiyo kuwa nguvu za wananchi ni Tshs.16,880,000.00, wadau wa maendeleo Tshs. 9,294,200.00 na serikali kuu kupitia mradi wa SEQUIP Tshs. 25,000,000.00 ujenzi

Amezitaja faida zilizopatikana baada ya kujengwa kwa shule hiyo kuwa ni pamoja na kupunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu, kupunguza mdondoko wa wanafunzi, kupunguza utoro na pia imewezesha kuinua kiwango cha ufaulu.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.