• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI KUUFUFUA MRADI WA UMWAGILIAJI KILIMO CHA MBOGAMBOGA KISASIDA

Posted on: October 7th, 2022

MKOA wa Singida unatarajia kuongeza uzalishaji wa alizeti hadi kufikia tani 492,485 kwa msimu ujao wa kilimo (2022/2023), kutoka tani 260,382, zilizozalishwa wakati wa msimu uliopita (2021/2022), tani zitakazochangia asilimia 44.2 ya mafuta yote ya kula nchini.

Akizungumza kwenye kikao na Waziri wa kilimo Hussen Bashe mkoani Singida, juu ya mkakati wa mkoa katika kuongeza alizeti, mwenyekiti wa kamati maalumu, Justice Kijazi, ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, amesema zinahitajika mbegu tani 2,900 ili kutosheleza ekari 631,391, zinazomilikiwa na wakulima, taasisi, vikundi na vyama vya msingi (AMCOS), kwa msimu ujao wa kilimo (2022/2023).

“Uzalishaji wa miaka mitano iliyopita tangu mwaka 2017-2022 haujawahi kutosheleza viwanda vya mkoa wetu wa Singida, ambao ulikuwa tani 97,757.1 kwa msimu wa 2017/2018, lakini uzalishaji wa juu ni tani 260,382 za mwaka jana, yaani msimu wa 2021/2022,” alifafanua Kijazi.

Kwa upande wake Waziri Bashe, akizungumza juu ya mradi wa umwagilianji kilimo cha mbogamboga uliopo Kijiji cha Kisasida, kata ya Unyambwa Manispaa ya Singida, amepongeza juhudi zinazofanywa na uongozi wa halmashauri hiyo, katika kuhakikisha mradi huo unafufuliwa ili uweze kuleta tija kwa jamii.

Shughuli za mradi wa mbogamboga uliopo katika eneo la Kisasida, kata ya Unyambwa, zimesimama kwa muda mrefu sasa, kutokana na changamoto mbalimbali za kimundombinu, hali iliyoathiri uzalishaji.

Kutokana na changamoto hizo , Waziri Bashe aliridhia ombi la kufufua mradi huo lililowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mhe. Mussa Sima, na kuwaagiza wataalamu wa wizara kukutana na uongozi wa Manispaa, tayari kwa ajili ya utekelezaji.

Waziri Bashe aliyemaliza ziara ya siku tatu mkoani Singida leo oktoba 7, 2022, amesema, pamoja na nia nzuri ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa Watanzania, amepongeza juhudi za kuipatia wizara hiyo fedha za bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023, kwa ajili ya maenndeleo ya kilimo.

Kuhusu mkakati wa kilimo cha alizeti, Bashe ameipongeza kamati ya kuratibu mkakati wa kuongeza uzalishaji wa alizeti 2022/2023, nakuitaka inagalie uwezekano wa kuinua kilimo cha mazao mengine, hasa yale ya chakula, ili yaweze kuleta tija zaidi kibiashara.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, alimshukuru Waziri Bashe na kuahidi kuusimamia vizuri mpango huo, ili taifa liweze kujitosheleza kwa mafuta ya kula yanayozalishwa nchi.

Serukamba amesema kuwa, atasimamia maagizo ya serikali, hasa ya wakulima kupatiwa pembejeo za ruzuku, ikiwemo mbegu tani 1,262.5 za alizeti pamoja na mbolea ili waweze kutekeleza mkakati huo kwa tija.

Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa mitatu nchini, ikiwemo mikoa ya Manyara na Dodoma, iliyopewa kipaumbele katika kilimo cha alizeti ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa mafuta ya kula, hali inayoigharimu serikali  kiasi kikubwa cha fedha, kwa ajili ya kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.