• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERUKAMBA: PONGEZI MKUU WA WILAYA, MSTAHIKI MEYA NA MKURUGENZI WA MANISPAA SINGIDA KWA UBORA WA KIWANGO CHA JUU MRADI YA BOOST

Posted on: July 18th, 2023

Mkuu wa Wilaya Singida, Mstahiki Meya na Mkurugenzi wa Manispaa wamepongezwa kwa utekelezaji mzuri na wa kiwango cha juu wa miradi ya Boost na kusema kazi iliyofanyika ni kubwa sana inayostahili pongezi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ametoa pongezi hizo leo tarehe 18 Julai, 2023 baada ya kukamilisha ziara yake katika Halmashauri za Iramba, Mkalama, Singida Vijijini na Manispaa ya Singida , lengo likiwa ni kujiridhisha na hali ya ukamilishaji wa miradi hiyo kabla ya kukabidhiwa rasmi kwake Jumamosi  wiki hii. Ziara kama hiyo imefanywa pia katika Wilaya za Ikungi na Manyoni na Katibu Tawala wa Mkoa Singida Dkt. Fatma Mganga

“ Nia ya ziara ni kujiridhisha na hali ya ukamilishaji wa miradi hasa zile shule mpya lakini pia ujenzi wa madara. niwapongeze wenzangu wote  wa mkoa mzima, tumefanya vizuri sana…..” amesema Serukamba

Serukamba amesema miradi mingi imekamilika kwa aslimia 100 wakati michache ikiwa katika asilimi 95 na hivyo kutoa muda hadi Jumamosi tarehe 22 Julai, 2023 miradi yote iwe imekamilika tayari kwa kukabidhiwa.

Ametoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhadisi Paskasi Muragili, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulidi Kiaratu na Mkurugenzi wa Manispaa Jeshi Lupembe kwa kazi kubwa iliyofanyika ya ujenzi wa shule mpya mbili pamoja na vyumba vya madarasa katika shule za msingi ambapo amesema ujenzi umekamilika kwa asilia 100.

Aidha pongezi nyingine zimeelekezwa kwa wasimamizi na watekelezaji  wote wa miradi hasa ya BOOST katika ngazi ya mkoa na halmashauri na kuongeza kuwa bila wao miradi hiyo isingefikia kiwango hicho.

Mkuu wa Mkoa amewataka madiwani katika kata zenye miradi ya Boost kuwahamasisha wananchi  kushiriki  katika zoezi la  usafi wa mazingira pamoja na  vyumba vya madarasa katika shule hizo  tayari kwa kukabidhiwa.

Pamoja na hayo, Mkuu wa Mkoa Serukamba ameagiza zoezi la upandaji wa miti kuzunguka shule mpya zilizojengwa kufanyika kwa ajili ya vivuli lakini pia kupendezesha mandhari ya shule hizo.

Serukamba amesema makabidhiano kimkoa ya Mradi mkubwa wa Boost yanatarajiwa kufanyika katika shule mpya ya msingi  Imbele           (Minga) mapema wiki kesho.

Mkuu wa Mkoa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza na kuwekeza katika  maisha ya watu kupitia sekta ya elimu, afya, maji, umeme  na barabara.

Kwa namna ya kipekee amewapongeza wakuu wa wilaya katika Mkoa wake kwa usimamizi na ufuatiliaji wa kina wa miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya zao.

Amesema miradi hii ya uboreshaji wa miundombinu ya shule kwa kiasi kikubwa itapunguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuongeza usikivu kwa wanafunzi pia kuwawezesha walimu kuwafikia wanafunzi wote katika darasa na hivyo kuongeza ufaulu.

Amesema Mkoa wa Singida una vijiji 441 na kwamba ifikapo Juni 2024 kila kijiji katika Mkoa wa Singida kitakuwa na umeme

 “ ….mimi na wakuu wa wilaya kazi yetu ni moja, kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kiwango chenye ubora wa juu, sio boost peke yake bali miradi yote kuhakikisha inaenda vizuri”, amesema Serukamba

Zaidi ya Tshs. Bilioni 9 zimetumika kutekeleza Mradi wa Boost katika mkoa wa Singida

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.