• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Singida na Dhamira ya Kuondoa Vifo Vya Kina Mama na Watoto Wachanga.

Posted on: October 29th, 2021

Vituo vya vya afya 15 na Hospitali tatu (3) vimejengwa mkoani Singida ili kutoa huduma ya dharula kwa wazazi na watoto ikiwa ni mkakati madhubuti wa kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano..
Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya majengo ya ya kutolea huduma ya afya ya mama na mtoto kuongeza bajeti ya dawa, vifaa tiba, kuboresha maslahi na idaidi ya watumishi lengo likiwa na kuboresha huduma ya afya kwa mama na mtoto.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa kufungua kikao kazi cha kujadili vifo vya kina mama na watoto wachanga vitokanavyo na uzazi, kilchofanyika leo 0ctoba 28 ,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida .
Amesema Mkoa umeendelea kujikita katika kuboresha miundombinu ya kutolea huduma ya afya fedha za serikali na kwa kutumia mapato ya ndani kwa ajili ya kujenga vituo vipya vya kutolea huduma ,kununua vifaa tiba pamoja na gari la kusafirishia wagonjwa.
DC Muragili amebainisha kwamba vifo vya kina mama na watoto wachanga vimeendelea kupungua mkoani hapa kutoka vifo 55 mwaka 2016 mpaka 34 septemba 2021 wakati vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 701 mwaka 2016 mpaka kufikia vifo 508 septemba mwaka 2021.
Aidha DC huyo ametoa wito kwa washiriki wa mkutano huo kuhakikisha idadi ya vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga vinaendelea kupungu ikiwezekana vimalizike kabisa kwa kuwa serikali imeanza kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya.
“Takwimu zinaonesha kwamba bado kazi kubwa inahitajika katika kukabiliana na matatizo yanayojitokeza wakati wa ujauzito,wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua kwa kuwa bado namba ya wanofariki ni kubwa sana”, alisistiza Dc Muragili.
Aidha amesisitiza kwamba wataalamu wa afya kuendelea kuelimisha jamii kuhusiana na lishe bora wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua kama hatua ya kuboresha afya ya mama na mtoto na kuepuka vifo visivyokuwa vya lazima.
Amesema swala la afya ni la watu wote kwenye famililia hiyo kuwataka wanaume kushiriki kikamilifu katika huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kusaidiana na weza wao katika kuyakumbuka maamrisho na makatazo kwa wajawazito.
Hata hivyo Dc huyo amebainisha sababu za kutokea kwa vifo vya akina mama na watoto wachanga kwamba zipo huduma zinazotolewa kwa wakina mama wajawazito ambazo hazikizi viwango kulinga na miongozo mbalimbali ya huduma ya afya.
“Kukosefu wa elimu ya uzazi kwa baadhi ya watu imekuwa ni moja ya changamoto inayosababisha vifo kwa kina mama na watoto wachanga” alisema Mhandisi Muragili.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya ameitaka jamii kuachana na tamaduni na mila potofu zinazo wasababishia kutohudhuria kliniki, kufanya kazi zenye shuruba kwa muda mrefu na kuamini kwamba baadhi ya vyakula hawatakiwi kula kwa Imani wanayoijua wao wenyewe.
Akimalizia hotuba yake Mhandisi Muragili akavitaka vituo vya kutolea huduma kwa wazazi na watoto chini ya miaka mitano kuhakikisha huduma hizo zinatolewa bure kulingana na sera ya nchi inavyoelekeza na kuzitaka Halmashauri kusimamia hilo.
Kwa upande wake Mkurungezi mtendaji Halmashauri ya Singida vijijini Bi. Ester Anania Chaula akimkaribisha Mkuu wa Wilaya amesema kwamba wataalamu hao wanakutana kila baada ya miezi mitatu ili kufanya tahmini ya hali ya kiafya mkoani humo zaidi kwa akina mama wajawazito na watoto.
Amesema kwamba katika Halmashauri hiyo wanaendelea kutoa chanjo mbalimbali kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano ikiwa ni hatua muhimu ya kupambana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito.
Awali Dkt.Erinest Mugetta Akimuwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa amesema lengo la kikao hocho ni kupitia mikakati na maazimio ya kikao kilichopita na kuona namna ya utekelezaji wake na changamoto zilizookea
Amesema kikao hicho pia kimelenga kuweka mikakati na maazimio mapya baada ya kutathimini afya ya uzazi na mtoto pamoja na vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.
Ni mujibu wa kikao hicho kutathimini idadi ya vifo vya akina mama na watoto namna vilivyotokea na sabababu zilizosababisha kutokea alifafanua Dkt. Mugetta.

Kikao hicho kilihudhuriwa na madaktari bingwa wa watoto na akina mama, waganga wafawidhi kutoka Hospitali mbalimbali mganga mkuu wa mkoa pampoja na waganga wakuu wa wilaya.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.