• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TAASISI ZASHAURIWA KUWASILISHA MIPANGO YA SHUGHULI ZA MAENDELEO KATIKA KIJIJI/KATA MIRADI INAPOTEKELEZWA

Posted on: December 12th, 2023


Taasisi za umma zinazotekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ndani ya Manispaa ya Singida, zimeshauriwa kuwasilisha mipango yao ya utekekezaji wa miradi kwenye Kijiji/kata miradi inapotekelezwa ili iweze kufahamika vyema kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Singida Mjini , Bi Lucia Mwiru ametoa ushauri huo katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya Singida Mjini uliokaa kujadili utekelezaji wa ilani ya uchaguzi 2020/2025, uliofanyika katika ukumbi wa chou cha Maendeleo ya Wananchi (FDC), Manispaa ya Singida.

Mwiru amesema, wananchi wanahaki ya kujua kinachoendelea katika eneo lao na kwamba wakijulishwa mapema, kutasaidia kupunguza migogoro wakati wa utekelezaji wa mradi.

Amezitaja taasisi hizo kuwa ni Shirika la umeme nchini (TANESCO), Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (SUWASA), Wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) na Wakala wa barabara nchini (TANROADs) kufanya hivyo kwa kuwa miradi yao inagusa moja kwa moja Maisha ya kila siku ya jamii.

Amesema mipango hiyo ikiwasilishwa katika Kata/ Kijiji ambapo mradi huo unaenda kutekelezwa kutawawezesha wajumbe wa mkutano huu ambao ni wenyeviti na makatibu wa siasa katika kata kuisemea vyema miradi hiyo kwa wananchi na hivyo kuondoa mashaka ama vikwazo wakati wa utekelezaji.

Pamoja na hayo wajumbe wa mkutano huo wamepongeza kazi nzuri zinazofanya na Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili katika kuongoza, kushauri na kusimamia kwa umakini shughuli za maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida .

“ mkuu wetu wa wilaya anastahili pongezi kwani anajituma, anashauri na kusimamia vizuri shughuli za maendeleo katika wilaya yake yenye halmshauri mbili bila kuchoka, si jambo rahisi …” amesema Mwenyekiti Mwiru.

Katika kuthamini mchango wake, Kamati ya Siasa ya wilaya imeweza kumpatia cheti na barua ya pongezi mkuu huyo wa Wilaya kwa mchango wake katika shughuli za maendeleo, utii na uwajibikaji mahiri katika majukumu yake ya uongozi.

Pongezi hizo zilielekezwa pia kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, ambaye pia alitunukiwa cheti kutokana na usimamizi mzuri na kujituma kwake katika shughuli za maendeleo, lakini pia Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe , aliyepatiwa barua ya pongezi kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM kutokana na kujituma kwake na kuwa kiungo baina ya chama na serikali.

Awali kabla ya mkutano kuanza, wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Singida Mjini, walipata nafasi ya kutembelea miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na ile iliyokamilika, jambo lililoamsha hamasa na ari ya kusimamia vyema miradi katika maeneo yao ikiwa ni shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na nia yake thabiti ya kuwaletea wananchi wake Maendeleo ambayo imejidhihirisha katika miradi hiyo waliyoitembelea.

Aidha wajumbe hao wamepongeza matumizi mazuri ya fedha za mapato ya ndani yaliyowezesha kutekelezwa kwa mipango thabiti ya maendeleo ambayo matunda yake yameonekana katika miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa kituo kipya cha Afya kata ya Mtipa.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.