• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TAKUKURU: SIMAMIENI MIRADI KWA UMAKINI NA UADILIFU MKUBWA

Posted on: May 31st, 2023

Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imewataka walimu wakuu, kamati za ujenzi na mafundi kusimamia kwa umakini na uadilifu mkubwa ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi inayojengwa kupitia mradi wa BOOST.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Singida, Mzalendo Udege, amesema hayo katika mafunzo yaliyoandaliwa na ofisi yake yaliyowalenga Walimu wakuu, madiwani, watendaji wa Kata, wajumbe wa kamati za ujenzi za shule na mafundi wanaotekeleza mradi huo wa BOOST.

Mzalendo amesema, lengo la Mafunzo hayo  ni kwa ajili ya kupitishana katika mwongozo wa utekelezaji wa mradi wa BOOST lakini pia walengwa wa mafunzo kuweza kuelezea changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa mradi na kuweza kuzitatua kwa pamoja.

Kamanda huyo amewataka washiriki hao kuzingatia sheria na taratibu za manunuzi ili kuepuka kusababisha hoja na hivyo kuhimiza suala zima la uadilifu na uwazi.

Amesema kamati zilizoundwa zishirikishwe kikamilifu na kila kamati iwajibike katika dhamana waliyopewa na kwa kufanya hivyo kutarahisisha mradi kutekelezeka kwa urahisi na kwa wakati.

“…tuzingatie uadilifu na uzalendo, fedha za mradi sio za kulipana posho…tuwe na uchungu na miradi yetu kwani ni mali ya wananchi..tuache alama nzuri katika miradi tunayoisimamia” amesema Mzalendo.

Pamoja na hayo, Kamanda huyo wa Mkoa pia amewataka washiriki na hasa wahandisi kuhakikisha manunuzi yanaendana na mahitaji halisi ya vifaa, fundi aliyepatikana asiwe na zabuni ya kazi nyingi na usimamizi shirikishi kwa viongozi wa chama na serikali pamoja na wananchi ili kuwezesha utekelezaji wa mradi kulingana na muda.

Halmashauri ya Manispaa ya Singida imepokea zaidi ya Shs. Blioni 1 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa BOOST ambapo shule mpya 2, madarasa  04 ya awali, vyumba 15 vya madarasa,   matundu 13 ya vyoo vinajengwa kupitia mradi huu unaotarajiwa kukamilika Juni, 2023.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.