• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

UVCCM TAIFA WAHIMIZA UTEKELEZAJI WA ILANI KWENYE NYANJA ZOTE KATIKA MANISPAA YA SINGIDA

Posted on: December 20th, 2022

 Umoja wa Vijana  wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (VCCM) umeipongeza Serikali ya Mkoa wa Singida, kwa kusimamia vyema mkoa huu hasa katika kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo na hasa miradi ya vijana

Katika ziara yake kwenye mkoa wa singida Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohammed Kawaida ambaye aliongozana na Makamu wake Bi. Rehema Sombi Pamoja na wajumbe wengnine wa Chama,pamoja na masuala mengine wamehimiza suala la utunzaji mazingira kwa kupanda miti eneo la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.

Mwenyekiti huyo amesema, Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa fedha kwa ajili ya kuongeza majengo ya kutolea huduma za afya katika Hospitali hiyo ya Rufaa na kutoa rai kwa wasimamizi na watendaji katika hospitali hiyo kuhakikisha wanazitumia kwa umakini kulingangana na maelekezo ili  kukamilisha mradi huo.

Aidha Kawaida, amewapongeza  wauguzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwa huduma nzuri wanayoitoa kwa wagonjwa  na kusema kuwa kazi ya uuguzi ni wito na inahitaji kujitoa kwa hali na mali.

“Afya ni wito. Tunawashukuru sana wauguzi wetu kwa kujitoa nguvu kazi zenu katika kusaidia Maisha ya watu wengine,…….,” amesema Kawaida

Makamu M/Kiti wa UVCCM Taifa,  Bi. Rehema Sombi ambaye pia ni mbobezi wa Afya ya Jamii , amesisitiza kuwa wao kama vijana jukumu lao kubwa ni kusikia, kuona, kunusa na kuhakikisha ILANI ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa katika Nyanja zote ikiwamo Afya.

“Hospital hii ndipo nilipofanya mafunzo yangu ya vitendo nilipokuwa mwaka wa pili Chuo Kikuu…….., Najivunia sana leo hii na mimi kuwa sehemu ya Mafanikio ya Hospitali hii. Tunaijenga nchi kwa Pamoja”. Amesema Sombi.

Akisoma taarifa fupi ya maendeleo ya hospitali ya Rufaa, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Bi. Fatma Sita, amesema kuwa hospitali hiyo ina idadi ya madaktari bingwa 13,  Madaktari watatu (3) wa Program ya Mama na Mtoto, na Watumishi 376 sawa na 48% ya mahitaji huku upungufu ukiwa ni 57%. Amefafanua kuwa jumla ya watumishi 57 katika hospitali hiyo wanalipwa kwa mapato ya ndani ya Hospitali .

“Moja kati ya Mafanikio tunayojivunia katika hospitali yetu ni Pamoja na basi la watumishi, kulipa stahiki za watumishi wote. Hatuna mtumishi anayedai mshahara kwa sasa. Nikiri tu ya kwamba, Sera ya Wizara ya Afya inayosimamiwa na CCM inatoa huduma bora kwa Mama Wajawazito”. Amesema Sita.

Ugeni huu wa UVCCM ngazi ya taifa ulipata fursa pia ya kutembelea miradi ya vijana iliyonufaika kwa fedha za maendeleo za 10% ya mapato ya ndani ya Manispaa kikiwamo kikundi cha vijana cha Chipukizi katika Kata ya Mitunduruni.

Mstahiki Meya Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu,aliyeambatana na ugeni huo  amesifu Sera Mpya ya Serikali ya Mikopo ya 10% ya Mapato ya ndani ya Halmashauri kwenda kwa vijana kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi, na kutoa rai kwa maafisa maendeleo ya Jamii, kuendelea kuwaelimisha vijana kuhusu  fursa zinazotolewa na Serikali ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kukuza pato la nchi.

“Mama na Serikali yake wamejipanga vizuri. Mngekuja Singida miaka mitano nyuma, maendeleo haya tuliyofikia hayakuwepo. Tunaishukuru Sera Mpya ya 10% Mapato ya ndani kutoka kwenye mfuko wa Waziri Mkuu umepelekwa kwa vijana kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi. Ambapo 4% inaenda kwa vijana, 4% kwa Wanawake na 2% kwa Walemavu”. Amesema Kiaratu

Katika ziara hiyo ya siku moja katika Manispaa ya Singida, UVCCM wameshiriki katika zoezi zima la upandaji miti katika maeneo ya Hospitali ya Rufaa, kutembelea miradi mbalimbali katika Manispaa ya Singida ukiwemo mradi wa kikundi cha mafundi Seremala kiitwacho CHIPUKIZI, Mitunduruni, Pamoja na mradi wa Ufugaji Nyuki, Kisaki, na kutoa zawadi kwa Kina Mama Waliojifungua katika hospitali ya Rufaa.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAABARA YA KISASA SHULE YA SEKONDARI KINDAI

    June 19, 2025
  • SHULE MPYA YA SEKONDARI YA MUSSA SIMA

    June 17, 2025
  • WATOTO WATAKIWA KUWA WAZI WANAPOFANYIWA UKATILI

    June 16, 2025
  • NIMESAINI NOTISI ZA KUVUNJA MABARAZA YA MADIWANI - MCHENGERWA

    June 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.