• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAKUU WA SHULE, WALIMU WAKUU NA MAAFISA ELIMU KATA WASAINI MKATABA WA UBORESHAJI USIMAMIZI WA ELIMU

Posted on: January 12th, 2023

Wakuu wa shule, walimu wakuu na Maafisa elimu kata katika Manispaa ya Singida , wametakiwa kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoeya ili kuweza kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu.

Hayo yameelezwa leo na Afisa elimu wa Shule za Msingi, Omar Maje, wakati akiongea na wakuu wa shule, walimu wakuu na Maafisa Elimu Kata kwenye  kikao cha kupitia  mikakati ya uboreshaji na usimamizi wa elimu katika Manispaa ya Singida kulichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwenge.

Maje alisema Utaratibu huu wa ujazaji mikataba kwa viongozi wa shule  umelenga katika kuwafanya viongozi hao kuachatabia ya  kufanya kazi kwa mazoea na kujikita katika kuboresha elimu ili kuleta matokeo chanya.

“ Serikali inataka matokeo chanya ambayo tutayapata kupitia result oriented leaders na sio business as usual leaders” amesisitiza maje.

Maje  ameendelea  kufafanua kuwa  kupitia utaratibu wa mkataba, wakuu wa shule, walimu wakuu na Maafisa elimu Kata, wataweza kusimamia maeneo yao ipasavyo na hivyo kuweza kufanya mabadiliko makubwa katika eneo yao ya kazi.

Aidha amewaagiza Maafisa Elimu Kata kukaa vituoni mwao na kusimamia shughuli za elimu  na kuwataka kupanga siku moja katika wiki ya kuwasilisha taarifa ofisi za elimu za Manispaa

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe, akizungumza na viongozi hao kabla ya kufungua kikao, aliwataka waalimu  kutekeleza majukumu yao ili kuitendea haki serikali iliyowapa madaraka na kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo.

Alisema nidhamu ya mtu binafsi pia katika  kazi ,ndiyo msingi wa mafanikio katika uboreshaji elimu ambayo itachangia  katika kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi mashuleni.

‘’Tuibebe Singida kwa kila mmoja kutimiza wa jibu wake na hili litaweza kutimia kupitia nidhamu’’amesema Jeshi

Jeshi amehimiza pia kwa walimu kuwa na usimamizi mzuri wa fedha pamoja na miradi huku akiweka msisitizo katika  suala la usafi kwa mtu binafsi,wanafunzi pamoja na mazingira ya shule ili iweze kuwasaidia wanafunzi kujisomea katika hali ya utulivu lakini pia kupendezesha madhari ya shule.

Sambamba na hilo ametoa wito kwa waalimu kujali na kutumia vizuri muda hasa muda wa ziada baada ya kazi kwa kufanya shughuli mbalimbali ili kujiandalia mazingira mazuri baada ya kustaafu.

Kaimu Mkurugenzi huyo ametumia nafasi hii kuelezea baadhi ya mafanikio ambayo Manispaa ya singida imeweza kuyapata kwa mwaka 2022 ikiwa ni pamoja na kusajili shule mpya 5 za Msingi, Kujenga shule 03 za sekondari moja ikiwa ni kuanzisha kidato cha 5&6, kujenga na kukamilisha kwa wakati vyumba 50 vya madarasa kwa Tsh. Bilioni moja fedha za serikali kuu  na Ujenzi wa kituo kipya cha afya Kata ya Mtipa kwa fedha za Mapato ya ndani Tsh. 250,000 zimepelekwa kutekeleza ujenzi huo unaoendelea.

Mafanikio mengine ni pamoja na ujenzi wa machinjio  mpya Tshs. 72,000,000/-, Ujenzi wa dampo  Tshs. 75,000,000/- shughuli zote zikiwa zinatekelezwa kwa fedha za  mapato ya ndani.

Akielezea baadhi ya mipango ya baadae Jeshi amesema, Manispaa ya Singida imepanga kujenga kituo cha Malori ( packing site) ambayo itawekwa vitegauchumi mbalimbali lengo likiwa ni kukuza uchumi wa wananchi katika Manispaa ya Singida pia kuweka Manispaa ya Singida safi kwa kununua gari kubwa la kuzoa taka taka .

Jumla ya washiriki 111, wakiwemo wakuu wa shule 29, Maafisa Elimu Kata 18, walimu wakuu 55, maafisa kutoka idara ya Elimu Msingi na Sekondari 9, Mwakilishi wa Tume ya Utumishi ya walimu 01 na ofisi ya Mthibiti Ubora wa Elimu 01, wameweza kushiriki kupitia mikakati na vigezo na kisha kujaza mikataba

Baadhi ya wakuu wa shule, walimu wakuu na Maafisa Elimu Kata wakimsikiliza Mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Jeshi Lupembe ( hayupo pichani) katika kikao kazi cha kupitia mikakati ya uboreshaji usimamizi wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa Mwenge Sekondari

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.