• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WALIMU NA WAZAZI WATAKIWA KUPANDA MBEGU BORA KWA WANAFUNZI ILI WAPENDE SHULE

Posted on: May 10th, 2025

Walimu na wazazi wametakiwa kupanda mbegu bora kwa watoto wao ili kuwawezesha kupenda shule na kudhibiti utoro  shuleni, mimba za utotoni, na hivyo kuzuia mdondoko wa wa elimu kwa kuwa na mahudhurio mazuri shuleni.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joanfaith Kataraia, leo 10 Mei, 2025 katka kongamano la wadau wa elimu lililofanyika katika ukumbi wa chuo cha uhasibu Singida ambapo wadau walipata nafasi ya kubaini changamoto na kushauri namna bora ya kuzitatua lakini pia kupongeza mafanikio yaliyopatikana katika elimu.

Mkurugenzi Kataraia alichukuwa nafasi hiyo pia kuwapongeza wadau kwa kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo ambapo waliweza kushauri namna bora ya kuinua kiwango cha elimu katika Manispaa ya Singida.

Amesema kazi ya kuboresha elimu siyo ya serikali peke yake bali ni jukumu la kila mtu kwa nafasi yake, na kuwataka wadau hao kutoa ushauri wenye kujenga utakaotoa mwelekeo katika kuinua elimu ndani ya Manispaa ya Singida na pia mkoa wa Singida.

Kuhusu suala la kuzuia mdondoko wa elimu, Kataraia amesema ipo haja ya walimu na wazazi/walezi kupanda mbegu bora kwa watoto ili kuwafanya kupenda shule na masomo wanayofundishwa.

“….tupande mbegu bora kwa watoto zitakazo wafanya kupenda shule na hivyo kuzuia utoro, mimba za utotoni na mengine membi ambayo yanamfanya mtoto kuchukia shule”, ameasa Kataraia.

Aidha Mkurugenzi huyo ametumia fursa hiyo kuwataka walimu kusimamia na kutunza miundombinu ya kufundishia na kujifunzia iliyojengwa kwa gharama ili iweze kutumika na kizazi cha sasa na hata kizazi kijacho.

Pamoja na hayo ameutaka uongozi wa shule kufanya vikao  na wazazi  ili kuwaelimisha juu ya suala zima la elimu bure lakini pia kusisitiza umuhimu wa kuchangia chakula kwa wanafunzi wawapo shuleni.

Akizungumzia suala la ulinzi kwa watoto, Mkurugenzi Kataraia amewataka wadau hao wa elimu kuunga mkono juhudi za serikali katika kuzuia ukatili kwa watoto, ndoa za utotoni, mimba katika umri mdogo haliitakayowafanya  watoto kuwa na utulivu ili kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

“fanyeni vikao vitakavyo wawezesha kukumbushana wajibu wa kumlinda mtoto  na pia jukumula kuwajengea watoto misingi mizuri na bora ya maelezi” amesisitiza.

Kataraia pia amewataka viongozi wa dini kuwakumbusha wazazi kujenga ukaribu na watoto wao ili kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitatua mapema ili kuepusha madhara kwa watoto hao.

Amesema , watoto wanakutana na changamoto mbalimbali na ngumu, hivyo ni jukumu la wazazi kuwaweka watoto karibu nao ili kuweza kuzibaini  kwa upole na kuzitatua kabla ya kuleta madhara kwa watoto hao.

“viongozi wa dini muwapo katika nyumba za ibada, endeleeni kuwakumbusha wazazi umuhimu wa kuwa karibu na watoto wao ili kubaini changamoto zinazo wakabili tena kwa upole na kuzitatua.  ….watoto wanakutana na changamoto nyingi na nyingine ni ngumu sana wanahitaji ukaribu wa wazazi” amesisitiza

Amesema wazazi wanapaswa watambue kuwa hakuna urithi uliobora kwa watoto  kama elimu hivyo pamoja na majukumu mengine , wasisahau jukumu la malezi kwa watoto hao kwa kuwapa misingi iliyobora ambayo hawataicha hata wanapokua.

Kongamano hilo la wadau lilijumuisha viongozi viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, waheshimiwa madiwani, walimu wakuu na wakuu wa shule, maafisa elimu wa kata, viongozi ngazi ya vijiji , mitaa na kata, viongozi wa kimila, wafanya biashara na taasisi mbalimbali.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.