• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAWAKE WA MANISPAA YA SINGIDA WATAKIWA KUMUUNGA MKONO MHE. RAIS MAMA SAMIA KATIKA JITIHADA ZAKE ZA KUILETEA NCHI MAENDELEO

Posted on: March 8th, 2022

Wanawake katika Manispaa ya Singida wameaswa kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan za kuiletea nchi Maendeleo hususan katika nyanja za elimu na afya.

Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Yagi Kiaratu katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoadhimishwa katika ukumbi wa RC- Mission katika Manispaa ya Singida.

Mstahiki Meya amesema Rais Samia amefanya makubwa katika kipindi alichoshika madaraka  ambapo Manispaa ya Singida imenufaika katika sekta ya elimu  na afya  na kuongeza kuwa kupitia fedha za maendeleo za UVIKO -19 madarasa 42 yameweza kujengwa na watoto wanasoma kwa amani .

Amesema kwa ujenzi huo wa madarasa wanawake wameweza kutua mzigo wa kukimbizana na ada pamoja na michango mbalimbali ambayo ingempasa kuchangia ili mtoto wake aweze kusoma katika hali ya utulivu na amani.

Mhe. Yagi pia ameishukuru serikali kwa fedha za ujenzi wa kituo cha afya  kimoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika Manispaa ya singida. Aidha ameiomba Serikali kuongeza kasi katika kukamilisha taratibu za kuhamishia huduma za hospitali ya mkoa katika hospitali ya rufaa ili majengo yake ya sasa yaweze kutumika kama hospitali ya Wilaya.

“Wanawake wenzangu tuna kila sababu za kumuunga mkono Mhe. Rais mama Samia kwa jitihada za kuiletea nchi maendeleo hususan Manispaa ya Singida”, alisema Mstahiki Meya

Amesema kwa kuzingatia kauli mbiu ya Mwaka huu “ kizazi cha haki na usawa kwa Maendeleo endelevu” Jamii inapaswa kuupa kipaumbele  usawa huo kwa kupeleka Watoto wao shule wa kike na wa kiume kwani wote wana haki sawa ya kupata elimu, kucheza na kusikilizwa.

“Jamii yetu ni ya wafugaji isiwanyime watoto wa kike haki ya kupata elimu kwa kufanya kazi za nyumbani  na kuwapeleka watoto wa kiume  kuchunga mifugo, wote wana haki sawa” aliwaasa .

Aliitaka Jamii kutambua nafasi na uwezo wa watoto wa kike kwa kuangalia mifano ya hai ya mihimili mikubwa katika taifa la Tanzania inayoongozwa na wanawake

Aidha amewataka Wanawake kuwa mstari wa mbele katika kutoa ushirikiano katika zoezi linaloendelea  la uwekaji anwani za makazi na postikodi na kuhakikisha linafanyika kwa ufanisi mkubwa kwani lengo la zoezi hilo ni kurahisisha shughuli za kimaendeleo na kiusalama.

Amesema lengo la Serikali ni kuiweka Tanzania katika Mfumo wa kidigitali ili kurahisisha Maendeleo kwa wananchi na pia usalama wao. Aliongeza kuwa kufanikiwa kwa zoezi hili kutarahisisha zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti, 2022 kwani ni vitu viwili vinavyotegemeana.  

Naye kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa akiongea na Wanawake alisema wanawake wanajukumu kubwa  la kujenga taifa lenye maadili mazuri kwani wao ndiyo walezi wa familia na hasa watoto na kwamba taifa lolote lenye amani na utulivu ni matokeo ya wanawake wanaojitambua.

Amewataka Wanawake kusimama imara ili kuilinda Jamii kwa kujenga kizazi chenye maadili ambacho kitakuwa tunu kwa taifa kwa kuzalisha  viongozi bora wa miaka ijayo.

Ameitaka Jamii na hasa wanawake kutumika  vyema dawati la mtandao wa polisi wanawake popote pale wanapopatwa na na matatizo hasa ya unyayaswaji, udhalilishwa na vitendo vya kidhalimu dhidi yao na Watoto ili kupata msaada wa hara.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Mjini Bi Lucia Mwiru, aliipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Singida  kwa kuwezesha vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kupitia asilimia 10% za fedha za mapato ya ndani na kuvitaka vikundi vilivyonufaika kutumika fedha hizo kwa malengo yaloyokusudiwa .

Aliwataka Wanawake kutumia vyema fursa zinazotolewa na taarisi za fedha (banks) kwani zina fursa maalum kwa Wanawake na kuongeza kuwa mikopo inayotolewa sasa hivi kupitia mapato ya ndani haikidhi mahitaji

Naye Jaji Mstaafu Mhe. Fatuma Masenge akitoa salamu kwa Wanawake wa Manispaa ya singida katika maadhimisho ya siku ya wananwake alisema wanawake wanapaswa kutumia vyema sheria zilizowekwa ili kuwalinda pamoja na watoto dhidi ya vitendo vya kidhalimu .

Amesema wanawake wengi hukaa kimya pindi wanapofanyiwa ukatili na udhalilishaji kwa kuwa hawajui wapi pa kwenda na kuwataka kutosita kumtumia kwani bado ananafasi ya kuwasaidia na kuwaelimisha kwani wanajukumu kubwa la kulinda familia na hasa Watoto dhidi  ya vitendo vya kidhalimu bila kujisahau wao wenyewe.

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa Bi. Lupi Mwaikambo akikabidhi hundi za Mikopo kwa mgeni rasmi alisema jumla ya vikundi 26 vitapatiwa hundi zenye thamani ya Tshs. 92,000,000/- kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Kati ya vikundi hivyo 20 ni vya wanawake na 6 ni vya Vijana,

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 29, 2025
  • VIKUNDI 55 VYAPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPOKEA MIKOPO YA 10%

    June 29, 2025
  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • USAFI WA NGUVU KUELEKEA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.