• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATENDAJI NGAZI YA KATA WAJENGEWA UWEZO WA KIUTENDAJI ILI KURAHISISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU

Posted on: June 7th, 2022

Watumishi katika ngazi ya kata na mitaa waaswa kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao ili kufanikisha azma ya kuleta Maendeleo kwa Jamii wanayoiongoza.

Hayo yameelezwa leo tarehe 07 Juni, 2022 na Diwani wa Kata ya Unyianga Mhe. Geofrey Mdama wakati akifungua kikao kazi cha Watumishi wa Serikali katika kata (3) za Unyianga, Mtamaa na Mwankoko Manispaa ya Singida kilicholenga katika kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma.

Mhe. Mdama amesema Utumishi ni wito hivyo kuwataka watumishi hao kutekeleza majukumu yao pasipo migongano ili lengo la wito wao kutimia. Aidha amewataka kuzingatia mafundisho na maelekezo watakayopatiwa katika kikao kazi hicho kilichoongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Ndg. Kulanga Matia Kayanga pamoja na timu ya menejimenti ya Manispaa ya Singida.

“sisi kama Serikali tumewapa dhamana kubwa watumishi na ndiyo maana ninasema dhamana hiyo ni wito…..” amesema Mhe. Mdama

Akiongea na Watumishi baada ya kikao kazi kufunguliwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Ndg. Kulanga M. Kayanga amesema lengo la kikao hicho ni kukumbusha Watumishi juu ya majukumu na wajibu wa kiutumishi pamoja na kuhimiza ushirikiano baina ya Watumishi katika ngazi ya Kata ili kila mmoja afikie lengo katika kutekeleza majukumu yake.

Amesema Watumishi katika kila sekta hutegemeana katika kutekeleza majukumu yao kiutumishi hivyo hawanabudi kuwa wamoja katika kila hatua hasa ya usimamizi wa miradi, ukusanyaji mapato na usimamizi wa sheria mbalimbali.

“Ni wajibu wa Mtendaji wa kata kutembelea shule, zahanati, vikundi vya Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu, vikundi vya kilimo na ufugaji ili kubaini mapungufu na kushirikiana na watumishi katika sekta hizo kupata ufumbuzi na sio kumwachia mwenye sekta peke yake” amesisitiza Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa Utumishi wa Manispaa ya Singida.

Pamoja na masuala mbalimbali ya kiutendaji Kaimu Mkurugenzi ametumia fursa hii kupitia timu ya menejimenti  kuwajengea uwezo watumishi hao kuhusiana na masuala mbalimbali ya kiutumishi, kuhamasisha shughuli za vikundi na Mikopo ya Vijana Wanawake na watu wenye ulemavu, Sensa ya watu na makazi, anwani za makazi, Afya na Elimu.

Ziara hii ni moja ya mikakati ya Manispaa ya Singida katika kuwajengea uwezo Watumishi wake pia kubaini changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa kila siku wa majukumu yao. Aidha mkakati huu hutoa nafasi kwa watumishi katika ngazi za kata, Vijiji na mitaa kushauri na kutoa maoni yao kwa uongozi hali inayorahisisha utatuzi wa changamoto mbalimbali na kuboresha mazingira ya utendaji kazi.

Jumla ya Watumishi 40 wa kata za Mwankoko, Unyianga na Mtamaa wamejengewa uwezo wa kuimarisha utendaji kazi kwa kusimamia sheria, taratibu na kanuni za kiutumishi pia kujenga ushirikiano baina yao na jamii.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • WATUMISHI MANISPAA WAPEWA ELIMU JUU YA BIMA YA MAISHA YA SANLAM

    August 14, 2025
  • AFISA ELIMU ATAKA UFAULU WA ASILIMIA 100 A- LEVEL MANISPAA YA SINGIDA

    August 12, 2025
  • MANISPAA YA SINGIDA YATINGA TATU BORA NANENANE KITAIFA 2025

    August 08, 2025
  • RAIS SAMIA AZINDUA MAABARA YA KILIMO KILELE CHA MAADHIMISHO YA NANENANE 2025

    August 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.