• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZAZI WAASWA KUZUNGUMZA KWA UPOLE NA WATOTO ILI KUBAINI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI

Posted on: March 5th, 2023

Wazazi mkoni Singida wameaswa kutumia lugha laini na ya upole pindi watoto wanapohitaji ushauri wao ili kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Mwalimu Dorothy Mwaluko, ametoa wito huoleo tarehe 5 Machi, 2023 katika mdahalo ulioandaliwa na Shule ya Sekondari ya Wasichana Tumaini,iliyoko Kinampanda wilayani Iramba, uliohusu mtoto wa kike katika ulimwengu wa kidigitali.

Mwl. Mwaluko amesema, kulingana na utandawazi ni vyema wazazi na hasa kina mama kutumia muda mwingi kusema na watoto wao ili kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuchukua hatua mara moja ya namna bora ya kukabiliana nazo.

“ utandawazi ni mzuri lakini unachangamoto katika malezi na makuzi ya watoto…..kinamama tumieni lugha ya upole ili muweze kubaini yanayowasibu watoto na kutafuta ufumbuzi”, amesisitiza Mwaluko.

Katika mdahalo huo uliongozwa na Mwl. Mwaluko akiwa mwenyekiti, mada mbalimbali ziliwasilishwa kumhusu mtoto kike katika ulimwengu wa kidigitali, ambazo ni Mila na Desturi, Uhuru wa kutoa maoni, haki ya kupata elimu, Ulimwengu wa kidigitali, unyanyaswaji wa mwanamke  na mavazi yenye staha.

Wanafunzi hao walipata nafasi ya kujadili mada hizo na mapendekezo kutolewa ikiwa ni pamoja na jamii kuelimishwa kuhusu haki za mabinti / watoto wakike, Kukomeshwa kwa vitendo vya unyayasaji wa wanawake na watoto wa kike, Elimu juu ya haki za wanawake hasa vijijini ambapo ilielezwa kuwa wanawake wengi hushindwa kujieleza kuhusu changamoto zinazowakabili.

Mapendekezo mengine yaliyotolewa na mabinti hao ni suala la usiri katika dawati la jinsia kupewa kipaumbele ili kuepuka kuwadhoofisha wahanga, kutokomezwa kwa ndoa za utotoni na kutolewa kwa elimu ya kujiendeleza kwa mabinti ambao wamekomea elimu ya darasa la saba kutokana na umri wao kuwa bado mdogo.

Pamoja na Mdahalo huo wanafunzi wa shule ya Tumaini waleweza pia kuonesha ubunifu wao katika suala la mafazi ya asili ambayo yalimfurahisha mwenyekiti wa mdahalo huo na kuahidi kuandaa tamasha la mavazi ya asili yenye staha kwa watoto wa kike katika shule za msingi na sekondari Mkoani Singida.

Naye Katibu wa Chama Cha Walimu Mkoa, Bi. Digna Nyaki amesema Mdhahalo huo umekuja wakati mwafaka kwani teknolojia imekuwa ikitumiwa tofauti na malengo kusudiwa na hivyo kuwaharibu vijana wa kike na wa kiume.

Bi. Nyaki amewaasa mabinti hao kelewa wajibu wao na kuheshimu mila na desturi za jamii zinazomlinda mtoto wa kike ili kumwezesha kuwa mama na kiongozi bora hapo baadae.

Mdahalo uliofanyika ni katika mwendelezo wa wiki ya maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani ambapo kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 08/03/2023 kauli mbiu ikiwa Ubunifu wa Mabadiliko ya Teknolojia: Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia

Matangazo

  • MAPITIO YA BAJETI 2022/2023 February 21, 2023
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA KWA SHULE 2021 November 15, 2021
  • KARIBU UWEKEZE KATIKA MANISPAA YA SINGIDA November 15, 2022
  • TATHMINI YA MATOKEO YA MITIHANI YA DARASA LA SABA 2022 KI- SHULE December 23, 2022
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • KAYA 5,396 MANISPAA YA SINGIDA ZIMENUFAIKA NA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF) DIRISHA LA SEPTEMBA - OKTOBA, 2023

    March 22, 2023
  • BOT YATOA ELIMU YA FEDHA BANDIA KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA KIMATAIFA LA VITUNGUU, MISUNA MANISPAA YA SINGIDA

    March 20, 2023
  • TUME YA UTUMISHI YA WALIMU SINGIDA YAWATAKA WALIMU KUZINGATIA SHERIA,KANUNI NA MIONGOZO INAYOTOLEWA NA SERIKALI

    March 20, 2023
  • MIAKA MIWILI YA DHAHABU YA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN YALETA MAPINDUZI YA MAENDELEO SINGIDA

    March 18, 2023
  • Tazama Zote

Video

Waziri Jafo atoa maagizo mazito kwa ma-RAS, ma-DED, Wakuu wa idara na maasifa mawasiliano serikalini
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.