• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ZAIDI YA BILIONI 17 ZA TUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE MANISPAA YA SINGIDA

Posted on: May 10th, 2025

Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kipindi cha 2022/2023 hadi Machi 2024/2025 imepokea zaidi ya Tshs. Bilioni 17 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kwa shule za msingi na sekondari.

Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Singida Athuman Mnyusi, ameeleza hayo leo 10 Mei 2025 katika taarifa aliyoisoma mbele ya wadau wa elimu katika Kongamano la wadau wa elimu lililofanyika katika Ukumbi wa chuo cha Uhasibu Singida.

Katika taarifa yake iliyoelezea Mafanikio katika sekta ya elimu, changamoto, na mikakati ya kuboresha elimu, Mnyusi amesema Halmashauri ya Manispaa ya Singida na wananchi kwa ujumla wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kutolea elimu na hivyo kuwa na mazingira mazuri ya kisasa ya kujifunzia na kufundishia

“……tunamshukuru kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwa katika sekta ya elimu…tuna deni kubwa kwake”, ameeleza Mnyusi.

Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Singida Alhaj Gwae Mbua amepongeza wadau wa elimu kwa kushiriki kongamano hilo na kushauri kufanyiwa kazi kwa changamoto zilizotolewa ili utekeleza wa shughuli za uboreshaji elimu ziweze kufanyika kwa asilimia 100.

Naibu Meya ametumia nafasi hiyo pia kuhimiza suala la uchangiaji chakula ili watoto waweze kupata  mlo  wa mchana shuleni hali itakayowapa utulivu wa kufuatilia masomo

Ameshauri kutungwa kwa sheria ndogo itakayowajibisha wazazi wote kuchangia chakula kwani kinyume cha hapo utoro na mahudhurio duni yataendelea na hivyo kusababisha mdondoko wa elimu katika Manispaa ya Singida.

Akiwasilisha salamu za Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, diwani wa kata ya Kisaki, Moses Ikaku ametoa Pongezi kwa Mheshimiwa Rais kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Amali katika Manispaa ya Singida ikiwa ni jitihada zake katika kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana wanaomaliza kidato cha nne, sita na hata vyuo.

Ameiasa jamii kutumia vyema fursa hiyo kwa kuwapeleka watoto wao kupata ujuzi katika shule hiyo ili waweze kujiajiri na kupata kipato pia kukuza uchumi wa taifa.

Wadau mbalimbali wameshiriki kongamano hilo wakiwemo waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Singida, Viongozi wa Dini, walimu wakuu na wakuu wa shule, maafisa elimu Kata, wafanyabiashara ambao ni wadau moja kwa moja wa elimu na taasisi mbalimbali  za umma na binafsi.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.