• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YAFANIKIWA KUFUTA ALAMA NYEKUNDU KATIKA AFUA ZA LISHE

Posted on: April 29th, 2023

Manispaa ya Singida katika robo ya tatu ( Januari- Machi) 2023 imefanikiwa kufuta alama nyekundu katika afua ya lishe pamoja na kwamba mila na desturi katika baadhi ya maeneo bado ni changamoto.

Afisa Lishe wa Manispaa ya Singida, Isaac Maseri amebainisha hayo katika kikao cha robo ya tatu  cha Kamati ya lishe ya Manispaa, ambapo amesema Halmashauri imepiga hatua katika masuala ya lishe  kwa elimu kutolewa katika kata zote licha ya changamoto katika mapokeo ya elimu hii kwa jamii.

Akizungumzia kuhusu mpango wa utoaji chakula shuleni, Afisa huyo amesema kuwa , kati ya kata 18 za Manispaa ya Singida kata 16 zimefanikisha mpango wa utoaji chakula shuleni na kwamba kata mbili bado hazijatekeleza.

Maseri amesema  utoaji chakula kwa wanafunzi ni muhimu kwani mwanafunzi akipata chakula anakuwa na utulivu wa akili na hivyo kuongeza usikivu wakati wa masomo.

“ hali ya lishe katika halmashauri yetu inaridhisha ukilinganisha na miaka ya nyuma…..robo hii ya tatu tumeweza kuondoa alama nyekundu katika afua ya lishe ….tumeongeza idadi ya shule zinazotoa chakula shuleni” amesema Maseri.

Aidha amesisitizia suala la lishe kufanywa agenda katika kila kikao lengo likiwa kuiwezesha Halmashauri kuondokana na tatizo la utapiamlo kwa watoto na kuitaka jamii kutumia vyakula vinavyopatikana katika maeneo yao ili kupata mlo kamili kama vile mboga mbalimbali za majani, maharage na mboga za jamii ya mikunde.

Naye Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu, Jeremiah Kikonge, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa katika kikao hicho, ameipongeza kamati hiyo kwa kupiga hatua katika masuala ya lishe na kuwataka wajumbe kufanyia kazi makubaliano yanayofikiwa  ili kufikia lengo kusudiwa.

Amesema utoaji chakula shuleni sio ombi ni agizo la kuhakikisha watoto wanapata chakula ili kuwajenga kiakili  na hivyo kuongeza ufaulu, kupunguza utoro lakini kubwa kumfanya mtoto kupenda shule. Pia amezitaka kata ambazo hazijakamilisha mpango huo , kuhakikisha wanautekeleza kabla ya kikao cha robo ya nne, 2023

Katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika Aprili 27, 2023 Mkoani Singida, Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba aliwaagiza wakurugenzi kuhakikisha lengo la utoaji huduma ya chakula shuleni linatekelezwa katika shule zote katika halmashauri zao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alisaini mkataba wa lishe Septemba, 30, 2022, mkataba ambao ulitanguliwa na mikata mingne miwili wa Desemba 2017 na  na Agost, 2021 yote kwa pamoja ikihimiza usimamizi wa afua ya lishe.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • VIKUNDI 55 VYAPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPOKEA MIKOPO YA 10%

    June 29, 2025
  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • USAFI WA NGUVU KUELEKEA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA WAFIKIA ASILIMIA 80

    June 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.