• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

USHIRIKIANO WA WALIMU NA WAZAZI (UWaWa) UMELETA MAFANIKIO KATIKA SHULE NA KWENYE JAMII

Posted on: February 28th, 2023

Washiriki wa mafunzo ya uboreshaji shughuli za maendeleo ya elimu Leo tarehe 28February, 2023, wameeleza kuwepo kwa mafanikio makubwa tangu mafunzo kuhusu ushirikiano wa walimu na wazazi kupitia programu  ya Shule Bora kuanzishwa katika shule za Msingi Manispaa ya Singida.

Akitoa ushuhuda wa namna UWaWa ulivyoweza kuleta manufaa katika shule na jamii kwa ujumla, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mtamaa, Bryson Zera, amesema, kupitia ushirikiano huo wazazi walikubaliana katika kikao ya kwamba kwa kila mtoto atakayekuwa mtoro mzazi atawajibika kulipa faini ya Tshs, 1,000.

Amesema kutokana na makubaliano hayo, wazazi wengi wamewajibika kuhakikisha watoto wanakwenda shule wakati walimu nao wanahakakikisha wanasimamia mahudhurio vyema ili kuwabaini watoro, hali ambayo kwa mujibu wa mwalimu mkuu huyo imepunguza  hali ya utoro shuleni hapo.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi mwankoko amesema kupitia UWaWa jamii imehamasika na kuweza kuchangia ujenzi wa msingi wa chumba kimoja cha darasa shule msingi Mwankoko, msingi wa vyumba 02 vya madarasa na ofisi katika shule ya msingi Makungu. Na kwamba si hayo tu bali pia kwa upande wa taaluma, wazazi kupitia UWaWa, wameweza  kuchangia gharama za uendeshaji wa mitihani ya majaribio kila mwisho wa wiki shuleni hapo.

Mwalimu Hashimu Aladin wa Shule ya Msingi Minga amesema katika shule yake pamekuwa na vitendo vya udhalilishaji wanafunzi hasa watoto wadogo kutokana na uwepo wa mazingira ya vichaka na nyumba ambazo hazijakamilika ( maboma) ambayo yamepakana na shule hiyo.

“ Vitendo vya ulawiti vimekuwa vikifanyika kwa wanafunzi hasa wale wadogo…… UWaWa imeleta mabadiliko… ushirikiano baina ya wazazi na walimu katika kutatua tatizo hili umekuwa ni mkubwa na hivyo kupungua kwa vitendo  vya udhalilishaji watoto”, amesema Mwl. Aladin.

Pamoja naye Mwalimu Mwanamwema Nkhua wa Shule ya msingi Mughanga amesema UWaWa umeleta mwamko mpya kwa wazazi wa kushiriki mikutano ya wazazi na kutoa maoni  tofauti na hapo awali hivyo kuleta wepesi katika kutatua changamoto za wanafunzi za kitaaluma na kimaadili shuleni hapo.

Mwalimu Emmanuel Kimweri wa Unyakumi Shule ya Msingi amesema, UWaWa imekuwa ni daraja kubwa kati ya walimu na wazazi na kwamba kupitia ushirikiano huo, waliweza kuwarejesha wanafunzi watoro na kuendelea na masomo.

“ hatukutumia nguvu kwani wazazi walioko kwenye kamati wanawajua vyema wazazi wa watoto husika hivyo ilikuwa rahisi kuwafikia na kusema nao na mapokeo yakawa mazuri kwani watoto walirudi kuendelea na masomo”, amesema Mwalimu Kimwezi.

Mkufunzi wa mafunzo hayo ngazi ya Halmashauri ya Manispaa, Bi. Salome Kyomo, amesema kwa shule yoyote ile,  ili iweze kufanya vizuri hapana budi kuwepo ushirikiano baina ya walimu na wazazi.

Amesema serikali kwa kuliona hilo, inatoa mafunzo ya UWaWa kwa walimu, wenyeviti wa kamati za shule, na maafisa elimu Kata ili kuweza kuwaimarisha na hivyo kuweza kusimamia shule zao ipasavyo, kwa kuhakikisha mwanafunzi anasoma katika mazingira salama na mazuri kwa kujifunza.

“ UWaWa imeenda mbali zaidi… kamati za shule zipo … UWaWa imejikita zaidi kwenye madarasa kuanzia awali mpaka la saba….”amesema Kyomo.

Jumla ya walimu wakuu 53, wenyeviti wa kamati za shule 53, maafisa elimu Kata 18 na wakufunzi 4 wameshiriki katika mafunzo hayo katika Manispaa ya Singida.

Mwisho

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.