• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VYANZO VIPYA VYA MAPATO KULETA TIJA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Posted on: February 2nd, 2023

Halmashauri ya Manispaa ya Singida imeibua vyanzo vipya vya mapato, vinavyotarajiwa kuanza kutumika mwaka wa fedha 2023/2024 ili kuiwezesha Manispaa kukusanya mapato na kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Akiwasilisha Mpango na Bajeti ya zaidi ya Shilingi Bilioni 33.4 kwa mwaka wa fedha 2023/2024, mbele ya Baraza la Madiwani, Mchumi wa Manispaa, Selestine Massawe, amevitaja vyanzo hivyo kuwa ni mradi wa matofali, uendelezaji wa vitegauchumi katika Kituo kikuu cha mabasi, ujenzi wa soko la kisasa la vitunguu, ujenzi wa maegesho ya magari makubwa lenye vitegauchumi mbalimbali ndani yake, ujenzi wa jengo la kitegauchumi eneo stendi ya zamani, vyote hivi vikitarajiwa kutoa ajira kwa wananchi wengi na hasa  vijana.

Wakitoa michango yao katika Bajeti hiyo, Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Madiwani, wameunga mkono uanzishwaji wa mradi huo wa matofali kama chanzo kipya cha mapato ambapo wamesema, mradi huo uliotengewa kiasi cha shilingi takribani milioni 50, wenye tija kwa jamii, ni matokeo ya ziara za mafunzo walizofanya katika Halmashauri zingine, walizotembelea.

Meya wa Manispaa ya Singida, Mstahiki Yagi Kiaratu, akichangia Bajeti hiyo amesema , Bajeti ya mwaka ujao wa fedha inatoa nafuu kwa Wananchi, kutokana na  shughuli za kawaida kushushwa kutoka asilimia 60, hadi asilimia 46 kwa mwaka wa fedha 2023/2024

MKUU wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragili, akiongea katika Baraza hilo maalum la kupitisha bajeti, amepiga marufuku watoto wa umri chini ya miaka 18 kuingia kwenye maeneo yanayochezeshwa Kamari, maarufu kama ‘Play station’, kufuatia watoto wengi na vijana kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.

Sambamba na hilo , Muragili amewataka wale wote wanaoiendesha michezo hiyo kukata leseni, kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Singida ili iwe rahisi kufuatilia kazi zao.

Aidha Mkuu wa Wilaya, Mhandisi Muragili amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumpa nafasi nyingine ya kuitumikia serikali katika Wilaya ya Singida na kuahidi kutomwangusha kwa kuwa aiamini timu ya viongozi iliyopo na kwamba wako tayari kutekeleza majukumu na maagizo mbalimbali hasa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Bajeti ya Mwaka ujao wa fedha 2023/2024 ya shilingi Bilioni 33.4/= imeshuka, ikilinganishwa na bajeti  ya mwaka wa fedha wa 2022/23, ya zaidi ya shilingi Bilioni 37.8, kutokana na sababu kadhaa, ikiwemo mishahara ya watumishi kwa mwaka ujao kuandaliwa kwa njia mfumo, badala ya makisio kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • INEC YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI

    May 14, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA VYA SIASA WALA KIAPO CHA UTII

    May 12, 2025
  • MANISPAA YA SINGIDA YATAKIWA KUPIMA MAENEO KABLA YA KUTEKELEZA MIRADI

    May 09, 2025
  • “PONGEZI KWAKO, RC HALIMA DENDEGO”

    May 09, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.